Dada yangu anapitia mateso makali sana sababu ya kijana wake kushika Dini hadi imemfanya amekuwa mjinga

Dada yangu anapitia mateso makali sana sababu ya kijana wake kushika Dini hadi imemfanya amekuwa mjinga

[emoji1666][emoji1666] Naam ndugu yangu katika imani umetoa maoni Bora sana ..watu wasichokijua uislamu aujakataza kusoma elimu dunia uyo kijana no matter atafanya nini bila kukaachini na mama yake wakawekana sawa amna kitu atakachokifanya kwenye dunia hii kitakachokuwa na baraka as long as mama yake ana lalamika kitu pekee ambacho muislamu atakiwi kumsikiliza mama yake ata kama akisema ni kumuasi allah pekee ..
Kasoma kamaliza chuo kaatafutiwa ajira kaona hauendani na imani yake kaamua kuacha mamake anataka akubali ajira hiyo huyo kijana hanakosa kwa mamake,imeandikwa hivi mtiini allah na mtumewe,na muwafanyie ihisani wazazi 2 lakini wakikutaka kumuasi allah usiwakubalue lakini uishi nao kwa wema
 
Kuna best yangu aliacha kupasua mende mtihani wa taifa form 6 biology, kisa alikuwa radicalized huko msikitini kwao, tulikuwa tunasoma wote baadae akahamia huko mazima, nilikuwa namwona na container lake anakuja kuchukua msosi au kama kuna mwalimu class anatokea, alikuwa amepauka ngozi sijui kwanini. It was so sad, na akazungusha yai matokeo ya from 6, wakati alikuja na division 1 ya point 8 sijui.
Shule za uboyizini ndio zao.

Kwanza wanalazimisha wapewe wajenge msikiti.

Sasa huko msikitini ndio kunageuka kuwa chimbo hawaende class ni ku radicalizing each other hadi kufikia stage za KiTaliban.

Jamaa wanajitenga hawataki urafiki Wala shirikiana na dini tofauti.

Madogo wasioenda swala Tano wanachapwa mikanda.

Wanafundishana Karatema Kung Fu huko.

Wemgi hupata matokeo mabaya labda wale wanaojiweza kimasomo.
 
Hapana hata dini inataka tufanye kazi baada ya kumaliza swala ,na hata kama unataka kumtumikia mungu angefanya kazi yake ya udaktari na muda wa ziada angeenda kufanya hiyo ibada nyingine, kwani pia kuhudumia watu kwa taaluma yake pia ni ibada bora kwa mungu, hata mtume wetu ametuambia tukatafute elimu hata uchina , sasa jitu lina elimu linaacha taaluma hata mungu hapendi
Ndio madhara ya kusomesha mtoto ukitegemea akiajiriwa upate sehemu ya mshahara wake, mimi nilidhani mvuta banghe mwizi mlevi mzizi kumbe kachagua njia nzuri sana ya mitume na manabii, ifahamike kusoma sio lazima uajiriwe huyo mama asimkatie tamaa amuulize kazi anayoiweza amuwezeshe t
 
Ndio madhara ya kusomesha mtoto ukitegemea akiajiriwa upate sehemu ya mshahara wake, mimi nilidhani mvuta banghe mwizi mlevi mzizi kumbe kachagua njia nzuri sana ya mitume na manabii, ifahamike kusoma sio lazima uajiriwe huyo mama asimkatie tamaa amuulize kazi anayoiweza amuwezeshe tu
Atawezeshwa misikitini huko si kachagua hayo Maisha?Kwa ushauri wangu huyo kama familia wamteme tu sio muda watamsikia Guntanamo huko
 
Dada yangu 49 years now ameajiriwa kwenye Hospitali Binafsi kubwa sana hapa Dar, ana kijana wake wa kiume ambae ndio alitegemea aje hata aonyeshe njia maana watoto wake wengine ni tia maji wote wanamsumbua huyu ndio alijua atakuja kumfuta machozi, Cha kwaza kijana wakati yupo form six tu walifukuzwa shule yeye na wenzake 4 sababu ya kuanzisha makundi ya kidini yenye misimamo isiyoeleweka na kufanya vurugu, ikabidi Dada amtafutie shule nyingine private kwa gharama kubwa kumnusuru.

Dogo akamaliza Advance akaaply Chuo cha udaktari Tanga huko, hali ilivyokuwa ngmu maana Baba yake hakuwa na msaada wowote Dada akakopa sh milioni 5 pale kazini kwake kwa ajili ya kumsomesha tena hiyo milioni 5 iliisha, ikabidi awe anapambana kuongezea hela sehemu nyingine, Dogo akapiga kitabu akamaliza kwa tabu sana.

Mwaka 2020 Dada kwa sababu ni Mkongwe pale kwenye Hospitali anayofanya kazi akafanya juu chini kumuombea nafasi na moja kwa moja Dogo akapata nafasi ya kuajiriwa kama Daktari

Balaa likaanza Dogo baada ya kuajiriwa tu akawa anakuja kazini Amevaa Nusukanzu, Kobazi na Kibarakashia huku Anafuga Ndevu kama Osama, hadi akawa anatisha waajiri wake ikabidi Sister aitwe haraka sana akaambiwa kuwa Huyu kama ni mwanao basi kaa nae umkanye mara moja kuwa Yale hayakuwa mavazi sahihi kwa mfanyakazi akashauriwa kuwa avae mavazi official ambayo yapo kwenye muongozo kwa mujibu wa kazi.

Sister na sisi wajomba zake ikabidi tumuite Dogo tumkanye kuwa Uongozi wa pale wamemkanya ajirekebishe ile ni Hospitali kubwa na ni lazima afuate miongozo, Dogo akawa mbishi na alipoona anazongwa sana kwa lile swala akaacha kazi kabisa kwa Hasira akaenda mikoani huko akawa anajihusisha na mambo ya kidini.

Kuanzia kipindi hicho Dada yangu ni presha za kupanda tu na kushuka, Juzi kati hapa hadi akazimia maana kijana alikengeuka akawa hamuheshimu na hana maisha ya kueleweka tena na ukiangalia amechoma zaidi ya milioni 7 kumsomesha na hadi leo hii hana kiwanja wala nyumba, amepanga.

=====================
=====================

NINEONA BAADHI YA WATU WAKIMLAUMU SISTER KUWA JUKUMU LA KULEA MTOTO NI LAKE HIVYO HAKUTAKIWA KULALAMIKA KUWA DOGO HAMSAIDII

JAMANI NIWAAMBIE TU MTU MWENYE JUKUMU LA KUSOMESHA NA KULEA KWA ASILIMIA KUBWA NI BABA LABDA AWE AMEFARIKI, NA DOGO BABA YAKE ALISHAKIMBIA MAJUKUMU HIVYO ALITAKIWA AJUE MAMA YAKE AMEENDA KUKOPA KARIBIA MILIONI 8 KUREPLACE JUKUMU LA BABA YAKE HIVYO ALITAKIWA DOGO ANAPOMALIZA SHULE AANGALIE KUWA MAMA YAKE HAKUWA NA HZO PESA NA ALIJITOA MUHANGA KUREPLACE NAFASI YA BABA YAKE ILI ASOME SO DOGO ALIPOMALIZA ILIKUWA NI MUHIM KUSAIDIANA NA MAMA YAKE MNAOSEMA KUWA DADA ASILALAMIKE NGOJENI YAWAKUTE
Waislam mambo leo mshukuru sana kwa kuzaliwa zama hizi ila pasi na shaka yoyote laiti kama mngemuona Mtume Muhammad jinsi ndevu zake na mavazi yake alivyokuwa akivaa basi bila ya shaka mngemkataa kama hivi mnavyomkataa mtoto wenu kwa ajili ya kuwaridhisha makufar. Yaani mnaona aibu ku-practice dini yenu halafu mnajidai kumfuata na kumpenda Mtume Muhammad pbuh.

Mtume hakuwa akinyoa wala kuchonga ndevu zaidi ya kupunguza masharubu tu, juu alikuwa akivaa kofia na kilemba na pia alikuwa akivaa kanzu zisizovuka vifundo vya miguu yake (wenyewe mnaita njiwa).

Mna khofu ya rizq mtafikiri ninyi ndio mnayoiteremsha. Yaani mara elfu kumi kufanya kazi na wazungu ambao huwa hawaingilii mavazi wala mwili wa mtu kuliko kufanya kazi na watu wanaojinadi ni waislam halafu wanawapinga wale wanafuata sunnah za Mtume Muhammad pbuh
 
Mtume Muhammad pbuh alisema kweli kuwa "hakika uislam uliabza ukiwa mgeni na utarejea tena ukiwa mgeni, bishara njema kwa watakaokuwa wageni."

Leo hii ukishikamana na uislam unaonekana chizi ,huna mbele wala nyuma, upo upo tu kwasababu tu hufati yale wanayoyataka mayahudi na manaswara. Kibaya zaidi watu wa mwanzo watakaoanza kukupiga vita ni wazazi,ndugu na familia yako.

Isomeni dini yenu muepukane na ujinga (ujahili)
 
Allah amrehemu huyo kijana na awasamehe nyinyi ndugu zake kutokana na ujinga mliokuwa nao.

Mtume alisema zitafika zama, muumini kushika dini yake itakuwa sawa na kushika makaa ya moto katika mkono wake.

Anas ibn Malik reported: The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said, “A time of patience will come to people in which adhering to one’s religion is like grasping a hot coal.”

Source: Sunan al-Tirmidhī 2260

Grade: Sahih (authentic) according to Al-Albani
 
Yaani kijana kasoma mpaka kafikia kuwa Mganga mfawidhi halafu eti mnamuita mjinga kisa kaamua kushikamana na dini yake kama Mtume alivyoifundisha. Sijui mna akili sawasawa enyi watu?!

Yaani kufuga ndevu,kuvaa kofia na kutokuburuza nguo( isbaal) ndio kuna mfanya mumuone chizi? Mngemuona Mtume na maswahaba zake si mngesema ni wendawazimu tu?!
 
Anakosea Kutomuheshimu Bi Mkubwa dini Haisemi hivyo, akiendelea Kutomushimu Basi Hata Harakati zake za Dini Hazitamfikisha Peponi, Akae Vizur Na Bi Mkubwa amuelekeze Kuwa Yeye Kaamua Kuwa Mwanaharakati Kupambania Dini Yake. Then Aendelee Kupambana Sio Kila Mtu Lazime Ajiriwe Katika Carrier Aliyoisoma.
Yeye anaona Tayari Kaondoa Ujinga Basi Inatosha.
Ogopa sana hao vijana wakifundishwa hayo mambo yao ya Dini za itikadi kalii hata Mama yake anaweza Kumchinjaaaa...!
 
Nani
Acha avune alichokipanda kama kunyoa ndevu hataki wacha hadi m@vuzz asinyoe si anataka kuwa kama Osama?
Nani kakwambia kuwa ukifuga ndevu hutakiwi kunyoa mavuzi?

Kwa taarifa yako Mtume kafundisha wanaume wa kiislam wafuge ndevu na wanyoe masharubu, wanyoe nywele za makwapani, wanyoe mavuzi na wakate kucha pia kuoga baada ya kufanya mapenzi ili kuondoa janaba.

Uislam ni dini ya usafi kiasi kwamba hata ukienda kukojoa unatakiwa utawadhe kwa maji kuondoa mkojo na pia uhakikishe cheche na mikojo hazikurudii kwenye nguo.

Soma uelimike sio kuongea vitu usivyo na elimu navyo
 
Ogopa sana hao vijana wakifundishwa hayo mambo yao ya Dini za itikadi kalii hata Mama yake anaweza Kumchinjaaaa...!
Wapi umeona mtoto wa kiislam kamchinja mama yake
Wakuu hamjuagi tu vile wazazi wanaumia kama hawajui mtoto anafanya nini haijalishi ana umri gani, huwa wanaumia sana.

Wazazi wengi husomesha watoto waje wawasaidie mbele lakini kama hilo mtoto haliwezi(sio lazima) basi walau awe na mwelekeo wa maisha.

Mzazi anakuwa na amani sana kama akiona mwanae analepea kama kishada kimaendeleo, hata kama atapambana kulipa madeni basi atalipa akijua yes walau jembe langu limetusua.
Yaani mtoto wa kiislam akiamua kusoma na kuifata dini yake inakuwa tatizo ila mtoto wa kikiristo akisoma na kuwa mchungaji anaonekana ana akili na mjanja!. Mbona hamuwatukani mapadre na wachungaji
 
Angemfungulia msikiti au madrasa tu.
Mimi mwanangu nikiwa simuelewi namfungulia kanisa awe kama yule mchungaji wa Kenya McKenzie
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom