Dada yenu nawaomba sana ndugu zangu Msaada wenu kupata kazi Nje ya Nchi

Shukran sana Kiongozi niko tayari kwa ajili ya hizo fursa ata kwa kuja huko huko Geita niko tayari Kiongozi..niko flexible enough working in any hardship environment na kuishi popote na Mkoa wowote ule ata kama mazingira yake ni magumu kiasi gani naweza kuvumilia

Kikubwa niweze kuwasimamia hawa Yatima na Mama yangu🙏

Shukran sana🙏
 

Kama una shida kweli ondoa Ulaya na Amerika weka Asia (QATAR na U.A.E-Dubai).

Why Asia? Kazi zipo pia hakuna masharti ya ajabu ya kupata VISA kama Ulaya na Amerika.
Nashukuru sana kwa mawazo yako Kiongozi

Ninashida sana yaan saana mpaka kujitosa kuandika hapa Mtoto wakike sio jambo dogo, kutokana na tafiti ndogo nilizozifanya mitandaoni Asia wanasema Waarabu wanyanyasaji sana na malipo yao ni finyu kupita kiasi, hizo ni tafiti nilizoziona mitandaoni wakisema

Na kwa upande wa Americans opportunities ziko nyingi sana kikubwa ujitume tu na ustick kwenye malengo yako

Na kama ikiwa ngumu kwa America ntaenda ata huko Asia iwe kama starting point kwangu, naweza nikiwa huko nikapata connections za kwenda America na ikawa ni kama sehem ya kutimia kwa Ndoto zangu🙏

Naomba sana MWENYEZI MUNGU amguse mtu anisaidie kwahili na tuandikishiane nikishafika na kuanza kazi Pesa zake zote nimlipe kwa maandishi kabisa ili awe huru na apate amani ya kutodhulumiwa🙏
 
Ahsante sana kwa mawazo yako yaliyonishibisha Ubongo wangu Kiongozi🙏

Niko tayari kama nitampata mtu wa kunisaidia basi niandikishiane nae kwa maandishi na mashahidi na Mwanasheria wake juu ya gharama atakazozitumia, na nitakapofika huko nifanye kazi na kumlipa gharama zake zote

Naamini katika uwezo wangu mkubwa wa kazi na bidii ya kupambana kwa mda mfupi tu kama nitapata hiyo safari ya nje basi gharama zake zote nitamrejeshea

Ahsante sana kwa kunitia moyo najua nitafanikiwa tu na nitarudi hapa kurudisha mrejesho🙏
 
Ndio mana ikaitwa JF sio lazima kila mtu afikirie kama unavyofikiria ww,
 
Dah😭umeongea kwa uchungu sana mm kama mwanamke mwenzako nimeguswa sana. Connection za kazi sina ila ningekua nazo ningekusaidia

Vip umeshapata kazi mpaka sasa????ushapata yoyote aliekusaidia kupata kazi??

Ingia PM yako nikutumie ata Laki 1 niliyojaaliwa nayo kwakua uko Mama pamoja na Mayatima hiyo ni sadaka yangu kwako najua sio pesa kubwa ila kidogo itakusoheza

Uko kwenye maombi yangu, na hapa ni mahali sahihi naamini wenye nafasi za kuweza kukusaidia basi watakushika mkono na kukusaidia, JF kuna watu wenye utu sana na na wenye kujitoa kwa ajili ya watu. Usikate tamaa unaonyesha ww ni mpambanaji sana endelea kupambana usirudi nyuma na utafanikiwa Mungu ni wetu sote. Ingia PM yako Dada, Pole sana utafanikiwa na utanyanyuka tena
 
Fatmie ajira za majuu sio jambo rahisi mkuu na Zaidi kwa kukurupuka. Ningekushauri tafuta plan B kujaribu kujikwamua alau kwa sasa mengine utapanga mbeleni.
Ikiwa unaona Ajira kwenye fani yako imekua ngumu Jaribu kufikiria nje ya Box Mkuu
 
Nashukuru sana kwa mawazo yako mazuri yenye faraja, naomba nisaidie nipate kazi ata apa ndani ya Nchi maana nimeshafanya Applications saana bila mafanikio, Ahsante
Kama ni kutoitwa kwenye interview inategemea na uandishi wako wa barua ya maombi, kwa hiyo CV yako ulipopita tu ipo vizuri.
Kama upo kwenye whatsapp ingia kwenye web ya ajiraleo kisha utakutana na magroup yanayotoa taarifa za ajira kila siku. Social work nafasi huwa zinatangazwa sana.
Yawezekana uandishi wa barua na ulivyoiweandika tu CV yako, kama hadi kwenye interview huwa unaitwa ila huchaguliwi hiyo ni issue nyingine ila kama huitwi tu kwenye interview ntakuonesha sample ya barua na cv
 
Mwaka huu huwezi kwenda nje sababu ya Corona ila kuanzia mwakani na kuendelea lazima utapanda pipa tu.
Endelea kuandaa passport n.k
Corona na usumbufu wa chanjo, vikwazo vya kusafiri, uchumi kuvurugika vyote hivi vimefanya mwaka huu uwe mbaya.
 
Mwaka huu huwezi kwenda nje sababu ya Corona ila kuanzia mwakani na kuendelea lazima utapanda pipa tu.
Endelea kuandaa passport n.k
Corona na usumbufu wa chanjo, vikwazo vya kusafiri, uchumi kuvurugika vyote hivi vimefanya mwaka huu uwe mbaya.
Shukrani sana kwa faraja🙏 nitafuata ushauri wako kuhusiana na Passport Ubarikiwe sana
 
Shukran sana kwa mawazo yako
 
Sijui ata niandike nini kuweza kuonyesha shukran zangu za dhati kwako, najaribu kutafuta maneno mazuri nakosa naona yote hayatoshelezi wema wako kwangu, Shukran sana kwa support yako uliyonipatia, MUNGU akulipe na akutimizie mahitaji yako na kwakila uliombalo akukamilishie nashukuru sana ndugu yangu, ur a true definition of a Lady ( Womens empowering or lifting each other ) hujui tu umenigusa kiasi gani lakin malipo yako utayapata nakushukuru sana Pesa niliipata ontime kabisa ikanisogeza kwenye Bills kama Luku na Maji pamoja na Iftari, Uzidi kuongezewa kwa pale ulipopunguza hakika haujapoteza ila umewekeza na malipo makubwa utayapata🙏
 
Fatmie ajira za majuu sio jambo rahisi mkuu na Zaidi kwa kukurupuka. Ningekushauri tafuta plan B kujaribu kujikwamua alau kwa sasa mengine utapanga mbeleni.
Ikiwa unaona Ajira kwenye fani yako imekua ngumu Jaribu kufikiria nje ya Box Mkuu
Shukran sana kwa mawazo yako
 
Habarini Wapendwa, mpaka sasa sijafanikiwa kupata kazi Nchini mwenye kuweza kuwa sehem ya msaada kwangu naomba anisaidie hali inazidi kua mbaya

Marnah nakushukuru kwa Msaada wako wa Pesa taslimu Shilingi Laki 1 ilinisaidia saana nakosa nisemeje sikujui na haunijui lakin hukutaka kuhoji chochote zaidi ya kunisaidia malipo yako utayapata na uzidi kuongezewa pale ulipopunguza🙏

Bado nahitaji kazi ndugu zangu nawaomba
 
Kama unataka kazi za Dubai, Oman, Qatar pitia hizi page zipo Facebook huwa wanapost mara kwa mara ajira zilizopo huko na kuwasafirisha wafanyakazi baada ya Interview.

1. Everlast - Recruitment Service Kenya
2. Elmvale Agency
3. The Job Centre - Malawi

Hizi zote zipo nchi jirani ila Watanzania wanaoomba pia huwa wanachukuliwa.
 
Shukran sana nazipitia kuanzia sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…