Pole sana dada yangu, nchi za kiarabu ndio zingekufaa zaidi, na kutimiza malengo yako, na sio nchi za ulaya na amerika utaishia kubeba mabox, huko hapafai ni risk kwako piaa, na isitoshe nchi za kikafiri hizo na wewe ni binti wa kiislamu na huko uendapo hakuna ndugu ambae atakustiri kwake, utaishia kutangatanga mwisho wa siku wajomba wanapita na wewe,,, Allah atafanya wepesi ukhuti.
Kule uarabuni ndio pangekufaa zaidi endapo wasingezuia wadada wa kazi, mshahara wa housegirl laki 5-6 mpaka 9,,,, wakati hapa kwa kisomo chako sizani kama wangekulipa ata laki 3.
Ushauri wangu, peleka maombi kampuni yoyote hapa kwetu, especially kampuni ya azam, dangote, GSM or vituo vya mafuta,, na usichague kazi ukhuty. Kazi yoyote wewe fanya tu ilimradi iwe na masilahi na ya halali vilevile,, kwa uwezo wa Allaah utapata kazi.
Ushauri wangu,,kama ulaya huna ndugu wa kukupokea na kukuhifazi achananako, fanya hapahapa kalibu na ndugu.