Fatmie kwanza niseme pole sana kwa hali unayopitia. Nimechelewa kuuona uzi wako ila naamini sijachelewa sana.
Pili, kuna nyuzi kadhaa humu jukwani kuhusu mambo ya visa na kazi katika nchi ulizozitaja ambazo tulibadilishana mawazo kwa undani sana. Jaribu kuzitafuta na kuzipitia utapata mwanga wa wapi pa kuanzia.
Nje kazi zipo nyingi tu halali na za chini ya meza changamoto ni kupata visa ya kufika huko. Na kama huna kazi hivi sasa basi the odds against you are even greater, ingekua rahisi kidogo kupata visa wakati ule bado una kazi ila hiyo isikukatishe tamaa.
Kwa uzoefu wangu, USA, visa za shule ni rahisi kidogo kuliko visiting visa, ila utaingia gharama za kuomba chuo, kukubaliwa ndo uje. Visiting visa ni nafuu ila zinahitaji uwe na mwenyeji US na uwe na ties TZ zakuonyesha utarudi yani kazi, nyumba, familia, assets nk.
Uzuri ni kwamba ukiomba visa ya kufanya masters kuna vyuo havikuitishi ada upfront, watakutumia I-20 ambayo utatutumia kuombea visa then watataka uwalipe ada yao ukiwa umeshafika. Ukifika utajiongeza nini cha kufanya.
Aidha ningeshauri angalia zaidi Canada kuliko USA, Canada ni rahisi kupata vibali ukifika nchini mwao kuliko US miaka ya hivi sasa.
Mwisho, nitumie DM nikuchangie chochote kitu.
Best regards,
Bufa