Dada yenu nawaomba sana ndugu zangu Msaada wenu kupata kazi Nje ya Nchi

Fatmie kwanza niseme pole sana kwa hali unayopitia. Nimechelewa kuuona uzi wako ila naamini sijachelewa sana.

Pili, kuna nyuzi kadhaa humu jukwani kuhusu mambo ya visa na kazi katika nchi ulizozitaja ambazo tulibadilishana mawazo kwa undani sana. Jaribu kuzitafuta na kuzipitia utapata mwanga wa wapi pa kuanzia.

Nje kazi zipo nyingi tu halali na za chini ya meza changamoto ni kupata visa ya kufika huko. Na kama huna kazi hivi sasa basi the odds against you are even greater, ingekua rahisi kidogo kupata visa wakati ule bado una kazi ila hiyo isikukatishe tamaa.

Kwa uzoefu wangu, USA, visa za shule ni rahisi kidogo kuliko visiting visa, ila utaingia gharama za kuomba chuo, kukubaliwa ndo uje. Visiting visa ni nafuu ila zinahitaji uwe na mwenyeji US na uwe na ties TZ zakuonyesha utarudi yani kazi, nyumba, familia, assets nk.

Uzuri ni kwamba ukiomba visa ya kufanya masters kuna vyuo havikuitishi ada upfront, watakutumia I-20 ambayo utatutumia kuombea visa then watataka uwalipe ada yao ukiwa umeshafika. Ukifika utajiongeza nini cha kufanya.

Aidha ningeshauri angalia zaidi Canada kuliko USA, Canada ni rahisi kupata vibali ukifika nchini mwao kuliko US miaka ya hivi sasa.

Mwisho, nitumie DM nikuchangie chochote kitu.

Best regards,
Bufa
 
Shukran sana kwa kujali kwako Ubarikiwe sana jaman🙏 nashukuru kwa maelezo yako yakinifu yaliyonipa mwangaza halisi juu ya Visa nitapitia websites mbali mbali kuweza kupata hizo nafasi za kusoma kwaajili ya Masters iwe kama njia ya kutimiza lengo langu. Nikipata tu chance ya kwenda huko najua within a short period of time nitakua nimekamilisha malengo yangu kutokana na bidii yangu kwenye kazi.
Nakushukuru sana umenipa nguvu kifikra na mwangaza wanguvu juu ya kutokukata tamaa kwenye haya mapambano. Ubarikiwe sana saana saana 🙏nimeshaku DM tayari.
 

Utagharamia application fees mara nyingi ni $100.

Kutuma documents zako, kama wanataka original then itabidi utumie DHL au FEDEX.

Visa yenyewe sijui sasa ni shingapi.

Bank statement usiwaze zinachakachuliwa tu.

Na nauli. Ukifika kiwanja hamna kinachoshindikana, watu wanafika leo na asubuhi wanaamkia box hata njia bado hawaijui.

Kila la kheri.
 
Ngoja kwanza, kwanini huna mume?
 
Huyu dada yuko committed sana wakuu..., wakuu wa humu wameona na hawataliacha lipite bure.
Barikiwa
 
Kuhusu asia , fanya tafiti hizi nchi mbili hapa ujue ukweli: Qatar /Doha , UAE /abu Dhabi, Dubai
 
Nakuinga mkono kwa wazo la kutafuta fursa nje ya nchi siyo jambo baya kabisa..

Natamani vijana wengi tupate hizi fursa hii itasaidi familia zetu/vizazi na hata nchi yetu kiuchumi.
 
Barikiwa saana Mkuu Barikiwa mnoo🙏 nashukuru sana kwa muongozo wako na mawazo yako ya busara na yakinifu🙏
 
Nakuinga mkono kwa wazo la kutafuta fursa nje ya nchi siyo jambo baya kabisa..

Natamani vijana wengi tupate hizi fursa hii itasaidi familia zetu/vizazi na hata nchi yetu kiuchumi.
Shukran sana Mkuu naamini wenye nazo watakuja kutupa hizo fursa na sote kwa pamoja tuweze kunyanyuana na kushikama mkono
 
Huyu dada yuko committed sana wakuu..., wakuu wa humu wameona na hawataliacha lipite bure.
Barikiwa
ALLAAHUMA AMIIIIINA Mkuu🙏
Nashukuru sana kwa comment yenye faraja, nami naamini hivyo kua hawataniacha
 
Ndugu zangu wanaJF najua humu ndani kuna Ma-Managers mbali mbali kwenye Taasis za Umma na Binafsi, humu ndani kuna Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa yote, kuna Wabunge humu, kuna Ma -HR's mbali mbali, kuna Ma-C.E.O. mbali mbali, kuna Waheshimiwa Mawaziri mbali mbali, kuna Madaktari wakubwa, kuna Wakuu mbali mbali, Ma-Officers mbalimbali na kuna Wafanyabiashara Wakubwa mbalimbali wanaomiliki Biashara zao na Makampuni yao mbali mbali.

Yaan JF ndio kila kitu, nawaomba Wanawanake Wenzetu tumshike mkono huyu Dada jaman, mimi niliplay part yangu nikamsaidia sio kwa kujitangaza lkn kwa namna moja au nyingine msaada wangu ulimsogeza kwa kiasi flani na naamini mpk sasa hana kitu, Unajua kwa Mwanamke kupatwa na changamoto kama hivi na kuweza kua open kuhitaji msaada wa kazi sio jambo jepesi yaan ni amajitoa na ni SHUJAA ndio maana nilipoona tu hii post niliguswa kama Mwanamke na kumsaidia bila kumhoji kwa chochote kile.

Niko na wazo kama Mwanamke mwenzetu ili aendelee kuwatunza mayatima na Mama yake na aweze kujisimamia huku tunasubiri Watakaoguswa kumsaidia na kumpa kazi ili asiingie kwenye Depression tumchangieni ata Milioni Mbili za KiTanzania (TSH) afanye biashara yoyote ile itakayoweza kumsaidia na yeye kujisimamia aweze kujikwamua kimaisha aweze kulipa hizo bills huku akiendelea na hustle za kupambana na kazi taratibu otherwise Depression itamuhusu.

Tumuokoe Mwanamke mwenzetu jaman asidhalilike, maana akikata tamaa atapotea na kuingia sehemu mbaya

Simjui hanijui lakin kuona Mwanamke anapitia magumu hivi sio jambo dogo, wenye connections basi jitokezeni mfateni PM mshikeni mkono msaidieni.

Niliwasiliana nae kipindi nilichomtumia kiasi kadhaa cha pesa akasema kwa Qualification zake ata Congo DRC, Ethiopia,Somalia, South Africa yuko tayari kwenda endapo nafasi ya kazi itapatikana (Kiuzoefu wa kazi yuko vizuri) Mimi binafsi ningekua kwenye nafasi ya kumsaidia kumpa kazi ningempatia kazi lakin siko kwenye position hiyo.

Sasa tukisema tumpe hizo laki laki zitaisha kwenye kula na bills lakin tukichanga ikafika angalau Milioni mbili au Tatu atafanya kitu na tutakua tumemstiri Mwanamke mwenzetu.

Kuna mtu anajiita PCK namuona huko Instagram anaonekana anasaidia watu ila connection nae sina ningekua na connection nae ningemtafuta tuone kama angeweza kumsaidia huyu Dada.

Mimi sina kikubwa nimejaaliwa cha kawaida tu, nawaomba tujitokeze watu 30 tumchangie Laki Laki itapatikana Milioni 3 kisha ziweze kumsaidia aweze kujisimamia, mimi naanza kukuchangia leo tena Laki mbili ya KiTanzania Cash Taslim naomba ukiipata nijulishe PM au hapa kwenye post

Kutoa ni MOYO sio Utajiri.

Sifanyi kwa kujitangaza ila nafanya iwe kama motisha kwa wengine, kwa wasiopenda kuonekana wametoa basi watoe wamchangie kwasiri na kumwambia kua asiwatangaze.

Naanza namimi nakutumia Laki Mbili sasahivi, ukiwa na bundle utakuja kutoa mrejesho, nakutakia kila la heri Mwanamke mwenzangu niamini WanaJamii Forum wana roho nzuri sana wana Utu sana utasaidika mpaka ushangae niamini wanakuja kukusaidia na kukufuta machozi.

Ndani ya dakika mbili utapokea Laki mbili ya KiTanzania sasahivi
Bado watu 28......tumchangie jaman.
 
Nchi hizo ulizo zisema utaishia kuota tu

Jitahidi kutafuta kazi hapa bongo ili ufanikishe hayo malengo yako ya kwenda nje

Otherwise labda utaenda kuwauzia papa wazungu tu na watakuchakaza kweli kweli

Au nasema uongo ndugu zangu
Umesema ukweli ila umetumia lugha kali.... Loooh
 
Nashukuru sana kwa mawazo yako mazuri yenye faraja, naomba nisaidie nipate kazi ata apa ndani ya Nchi maana nimeshafanya Applications saana bila mafanikio, Ahsante
Mtafute Ummy Mwalimu, omba kuonana nae. Mwambie nimekuagiza kwake.
 
Mungu akufanyie wepesi ufanikishe kila jema na familia yako yote hakuna kurudi nyuma.
 
CV yako iko vizuri darling naamini utasaidika pole Sana Mwanamke mwenzangu naweza kukusaidia kwa kiasi nilichonacho ili usogeze siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…