Dada yenu nawaomba sana ndugu zangu Msaada wenu kupata kazi Nje ya Nchi

Nchi hizo ulizo zisema utaishia kuota tu

Jitahidi kutafuta kazi hapa bongo ili ufanikishe hayo malengo yako ya kwenda nje

Otherwise labda utaenda kuwauzia papa wazungu tu na watakuchakaza kweli kweli

Au nasema uongo ndugu zangu

Huu ndiyo ushauri wa Mtanzania halisi sasa!! Kubezana na kukatishana tamaa kisa yeye ana ugali na juisi mezani 😂😂😂😂
 
Nimepitia comments karibia zote humu aisee Jamii Forum iko na watu wenye utu sana me naamini atapata kazi tena ya maana sana VIONGOZI WETU mbali mbali wenye mamlaka wataguswa na kumpa kazi kubwa tu ata serikalini na atakuja kutoa ushuhuda hapa.Ngoja wake atasaidiaka hapa wanasaidiwa sana watu wenye shida za kila namna.
Mtoa mada awe anaingia online japo kila siku tumtumie Pesa ya bundle ata Elfu 20 kwa Mwezi ili awe anakuja kutoa feedback hapa Jukwaani hilo ni wazo langu.
Akiiii wewe Dada @Marhah Barikiwa sana unamoyo wa dhahabu sana yaan Barikiwa sana umetoa mawazo mazuri sana kwa Mwanamke mwenzetu, yaan tukipata Wanawake Kama ww kwenye Jamii yetu basi tutanyanyuka sana kwa kusaidiana na kunyanyuana kwa vidogo vyetu tulivyo jaaliwa na kuchagua kubebana by leaving no one behind, Mimi namchangia pia (Laki 1 tsh) naomba ingia PM Dada mtoa mada nipatie no yako ya TigoPesa nikuchangie sasahivi, Wala sitaki kukuona Wala kukujua naomba TigoPesa yako tu.
 
Umetoa maelelezo mazuri sana na Ubarikiwe nadhani akifatilia hayo itakua Ni sehemu kubwa ya msaada kwake
 
kulingana na mtazamo wako ajira za nje zinakutaka uwepo nchi husika tayari hivyo ndo naona nchi kadhaa zinafanya direct hiring from your home ni nadra maana ajira nyingine unatakiwa kujoin immediately kwahiyo inafaa uwepo nchi hiyo
after all usikate tamaa na maisha mungu atakusaidia
 
Nilikuwa na dada yangu toka utotoni ndoto yake ilikuwa kuolewa na mzungu, tunavozungumza sasa hivi yuko kwa mzaramu uko chanika. Nachojaribu kusema flow with the wave husijichoshe akili na nafsi yako kwa vitu visivo vya lazima maisha ni popote na nchi yako inakuitaji bado.

KUKUBALI HALI NI KUFUNGUA MILANGO MINGINE.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Mkubwa,ungetusaidia kidogo kujua vyuo ambavyo haviitaji kulipa ada kwanza kama unataka kusoma Masters.
 
Barikiwa saana Mkuu Barikiwa mnoo🙏 nashukuru sana kwa muongozo wako na mawazo yako ya busara na yakinifu🙏

Anza ukikwama sehemu tujulishane tutatafuta ufumbuzi. Kila la kheri
Mkubwa,ungetusaidia kidogo kujua vyuo ambavyo haviitaji kulipa ada kwanza kama unataka kusoma Masters.

Kipo Canada. Last time mtu alienda bila kulipa ada upfront sijui kama wamebadilisha sasa. Check nao.

Kwa US, state universities nyingi hawaitishi ada upfront mf. Michigan State Uni, etc. Double-check.

Good luck.
 
Punguza Jazba twende nae taratibu, Huyu mdogo wetu anaonekana bado Mtoto wa mama
 
na watoto wa Marehem Kaka yangu ambao walikufa siku moja kwa ajali na Kaka yangu hao watoto wako 3 Yatima, wananitegea kuanzia kula yao, kusoma kwao

Watoto watatu waliokufa siku moja na baba yao kwa ajali kwa sasa ni yatima na wanakutegemea kwa kula yao, soma yao, lala yao, kila kitu...

Please!

Come clean now!

I mean, Fatuma please!
 
Canada kazi za kumwaga na Australis kazi kibao hasa kwa mafundi mchundo
 
watu wanaosemaga wanatamani waende ulaya wakafanye kazi huku atume hela nyumbami na kusave hela huwa nahisi hawajawahi kwenda huko. nilienda nchi flani kodi ndogo kabisa ya chini ya nyumba ya kimaskini ni tsh laki 5 kwa wiki, maji ya chupa nusu lita tsh elfu 20, juice ya embe ile ndogo kabisa kama ile sisi tunanunua mia 6 huko inauzwa dola 6 kama elf 18 hivi. hayo ndio maisha huko. nilishindwa aisee. sasa hapo ulipwe sh ngapi uishi, utume nyumbani, kisha usave ili baadae uwe na maisha bongo. anyway all the best
 
Naomb izo FURSA za geita
 
Ahsante sana🙏
Nahitaji kazi ata ndani ya Nchi ila nimeshaomba sana bila mafanikio na hali inazidi kua mbaya siku hadi siku
Pole sana dada yangu, nchi za kiarabu ndio zingekufaa zaidi, na kutimiza malengo yako, na sio nchi za ulaya na amerika utaishia kubeba mabox, huko hapafai ni risk kwako piaa, sijui mnapendea nini huko,, na isitoshe nchi za kikafiri hizo na wewe ni binti wa kiislamu na huko uendapo hakuna ndugu ambae atakustiri kwake, utaishia kutangatanga mwisho wa siku utajutia,,, Allah atafanya wepesi ukhuti.


Ushauri wangu, peleka maombi kampuni yoyote hapa kwetu, especially kampuni ya azam, dangote, GSM or vituo vya mafuta,, na usichague kazi ukhuty. Kazi yoyote wewe fanya tu ilimradi iwe na masilahi na ya halali vilevile,, kwa uwezo wa Allaah utapata kazi.

Ushauri wangu,,kama ulaya huna ndugu wa kukupokea na kukuhifazi achananako, fanya hapahapa kalibu na ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…