Dada zetu hivi unajisikiaje wenzako wanavyoolewa wewe upo tu umebung'aa?

Swali la kikatili hili. Kitendo cha kuuliza hivi unawaumiza watu na kuwatweza.
 
Hawa wanabaki kuzalishwa na vibaka tu, mwishowe wanakuwa kama Kajala na mwanawe kuchangia dushe huku wakibong'olea camera na kucheka.
 
I hope hii post ipo kwenye jukwaa la chit chat.

Kinyume na hapo, mtoa mada umeyumba sana mkuu.

Kungeweza kua na namna nzuri ya kuuliza hili swali (kama kungekua na umuhimu wa kuliuliza at all)

The point is, wao hawana control ya 100% kuhusu ndoa. Wanasubiri sisi tu propose.

Tusipofanya hivyo, hakuna ndoa kwao. Kwa maneno mengine, hakuna kikubwa sana wanaweza kufanya kubadili status zao.

Wanatakiwa kukaa na kusubiri.

Hata hivyo, naamini utakua na same courage ya kuuliza hili swali kwa mabinti zako wakigonga 35 halafu ngoma ni bila bila.

Au hata dada zako.
 
Sisi wanaume tunataka dem tunayemhitaji tumpate.(hapa haijalishi huyo dem ana status gani labda awe na magonjwa ya kuambukiza)
Lakini tunataka madem zetu wakihitajiwa wasikubali- wakatae teana wawajibu hata kwa kiburi na dharau hao wanaowahitaji.


Halafu sasa sisi wenyewe tunaendelea kutafuta madem wengine pamoja na kuwa tunao wengine.
....Utajiuliza sasa hawa tunaowatafuta wawe wa aina gani?
Wanaokubali au wanaokataa??
 
binafsi nina 29 na sijaolewa na Hilo halinifanyi nijione takataka Kisha nikubali kuolewa na takataka yoyote Kama mtoa mada kisa tu na Mimi nionekane na jamii nimeolewa,,, ukisema tunachagua Sana unamaanisha hatuna haki ya kuchagua wale tunaoona wanatufaa ktk maisha na haki hiyo Ni kwa wanaume tu sisi tuzoezoe tu Bora liende.... kauli Kama hizi ndizo zinafanya wanawake wengi kuvumilia ndoa za manyanyaso,, vipigo na dharau kisa anaogopa akiachika watu Kama wewe mtoa mada mtamnanga kwa kejeli mtaani bila kufahamu undani wake,, sitoacha kumuomba Mungu anijaaliye mume atakaye kua na kheri na Mimi sababu ndoa Ni ibada na stara kwa wote mwanamke na mwanaume lakini sitokua tayari kujitwika gunia la mavi maana ake mwanaume asiye na busara,, huruma Wala heshima kwa wanawake kwa kuogopea masimango ya wanajamii. hata hao unaowaona wameolewa waliwachagua Waume zao Kati ya wengi waliowafuata wakawaona watawafaa hawakukubali tu Bora liende,,in your next life nakuombea uzaliwe mwanamke,,.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…