nameless girl
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 4,195
- 2,678
Usiwakatishe wadada tamaa mkuu...Dada hio probability ni 0.000000000001
Kila kitu Mungu anakipanga kwa muda wake na makusudi yake. Hakuna ulazima wa kulazimisha kitu kwa sababu Champagnee amesema. Maisha ya ndoa ni zaidi ya umri, uzuri, pesa na vitu vingi sana ambao vijana wasio na fikra hawavitazami. Sasa kwa kuwa leo nina 23 years basi mtu wa hovyo amekuja kunitamkia ndoa nimgande. Hata nikiolewa umri hausimami. Nitazeeka. Nitachoka na kuchokwa. Hata mtu wa miaka 30 ambaye hajaolewa anaweza kuwa anavutia kuliko mie niliyeolewa na 23. Mume akaniacha mie na kumchukua yule wa 30. Mume wangu kama alinipenda kwa kuwa nilikuwa na umri mdogo basi ataniacha na kwenda kwa watoto. Maisha haya kikubwa ni kujua nini unataka katika maisha na kukubali kuwa karibu na Mungu wako. Otherwise you will be doomed.