Kijana wa kiume mwenye zaidi ya miaka 25 na una geto lako mwenyewe acha kuishi mwenyewe kama Jini, tafuta binti anzeni maisha na mpate watoto dunia ipate vijana wapya.
Ukiangalia sababu kubwa ya vijana kutokuoa ni kudai kuwa wasichana wanataka kuhongwa na hamna pesa.
Ngoja ni wambie kitu vijana wenzangu, sio wasichana wote Tanzania na duaniani wanataka kuhongwa, wapo wasichana na wanawake wengi sana wanatamani kuondoka majumbani kwao na kwenda kuishi na wanaume kwa lengo la kuanzisha maisha yao.
TUNAWAKUMBUSHA tu sio kila mwanaume anaweza kuwa baba wa watoto wako.
Wengine Wana sio ya kuwa baba mzazi tu, sio baba wa watoto wako.
Chaguo lako la mwanaume unayezaa nae ni muhimu sana kwa Maisha yako ya baadae na ya watoto wako.
Mwanaume ambaye Hana sifa za kuwa baba wa watoto wako anaonekana mapema tu "red flags", ukiamua kuwa naena kuzaa nae usije kusumbua Jamii baadae kusema wanaume wa hovyo na wala usihangaike kuwaambia watoto baba yenu mbaya, hawatunzi, hawajali na Wala Hana time na nyinyi.
Mabinti kuweni makini na chaguo lako unapoamua kuzaa na mwanaume. Unaweza kuharibu Maisha ya watoto wako kutokana na chaguo lako lisilo na umakini .
Tunarudia tena kuwakumbusha wanawake wengi walio katika matatizo haya, waliingia katika mahusiano na wanaume wa hovyo na viashiria vya dalili mbaya vilikuwepo na waliamua kuingia katika mahusiano walijua kuwa baadae kutakuwa na mabadiliko.
Mwanamke unazaa na mwanaume ambaye ana watoto Saba na wanawake tofauti na hawajali Wala kuwatunza. Na. Wewe unaingia kuwa mama wa 8 hapo.
Topic hii ni ngumu lakini ndio sababu ya wamama wengi kulalamika Sasa hivi kwamba wametelekezwa lakini pia watoto kuwa na baba wasio wajali katika Maisha yao.