Daftari la mauzo linapendeza lakini ukweli ni kwamba hakuna faida. Mzigo niliojumua 3.8M na kuuza 8.2M umenipa faida ya laki 1 tu

Daftari la mauzo linapendeza lakini ukweli ni kwamba hakuna faida. Mzigo niliojumua 3.8M na kuuza 8.2M umenipa faida ya laki 1 tu

Biashara hizi ndogo ndogo zenye mtaji wa chini ya 10M kusavaivu ndani miaka mitatu ni ngumu sana mwaka jana nami nilifunga duka baadaya ya kutoona faida kutokana na gharama kubwa ya uendeshaji kwa mfano
1. Tra 250,000
2. Leseni jiji 200,000(phones and accessories)
3. Kodi jengo (150,000*12)=1,800,000
4. Umeme (10,000*12)=180,000
5. Afu kuna hawa jamaa wa fire niliwakataa
6. Posho ya mfanyakazi (100,000*12)=1,200,000
7.ulinzi (10,000*12) =120,000
8. Usafi na mengineyo=100,000
9. Service levy( hapa niligoma kabsa kutoa) wakatisha kufunga biashara wakanipa control number kwa lazima ila sikulipa

Kwa gharama Hizi kutoboa ni ngumu sana aisee bora niendelee kuajiliwa ila biashara ni big no kabsa
Kwan wanao weza wanatumia njia gani
 
Biashara fanya mwenyewe mwanzoni na usipofanya mwenyewe mwanzoni uwezekano wa kukua ni mdogo pia biashara kwenye majijini bakubwa nishida sana kunaitaji kuwa na wazo zuri la biashara sio kuuza vitu vidogovidogo utaona faida.
Ideas are one thing; Implementation is the King; Ukija na Wazo zuri kama barriers of entry sio ngumu siku mbili tu watu watachukua idea yako na kuifanya kwa ubora zaidi...

In short mtaani pagumu na hizi ndoto kwamba kila mtu anaweza kuwa mfanyabiashara ni Ramli wanayotudanganya watunga Sera ili wasitunge Sera za kuhakikisha kuna ajira za watu kupata ujira...
 
Ni hesabu nilizopiga katika duka langu dogo nililoweka binti wa kazi mwaka jana, Nimehitimisha biashara ilikuwa inapiga nondo / kujitekenya / BREAK EVEN.

Siku ya jumapili duka hufungwa hivyo kwa mwaka zinabaki siku 261, kuna siku 8 nje ya jumapili binti hakufika, hivyo duka lilifunguliwa kwa siku 253 .

thamani ya mzigo kwa bei niliyouza 8,245,000
thamani ya mzigo kwa bei niliyojumlia 3,867,000
FAIDA YA MZIGO BILA GHARAMA ZA BIASHARA 4,378,000

GHARAMA ZA BIASHARA KWA MWAKA
Frem (laki 1 na nusu miezi 12) - 1,800,000
mshara 100,000 miez 12 - 1,200,000
chai, usafiri, choo, chakula elf 3 siku 253 - 759,000
tra kodi - 250,000 (haikuwa fair kabisa)
jiji, ulinzi, taka - 18,000
misiba, waombaji - 27,000
umeme - 71,000
leseni - 80,000
JUMLA YA GHARAMA - 4,205,000

FAIDA YA MZIGO - GHARAMA ZA BIASHARA = 173,000
Pole sana ila naona tatizo liko kwako. Ulivyojumua mzigo uka-relax ukisubiri mzigo wote uishe ununue mwingine. Pia uliweka bei kubwa sana kwenye bidhaa zako. Mzigo wa 3.867m kuuza na kupata 8.245m ni faida zaidi ya 100% kitu ambacho kitafanya mzigo ukae kwa muda mrefu dukani. Ungeweka hata 50% ya bei ya mzigo kama faida ili uishe fasta na kununua mwingine. Ukiwa na mzunguko mkubwa ndo utaona faida na sio na kukaa na mzigo mwaka mzima. Na hizo faida ungeziongezea kwenye mtaji. Kimsingi kulingana na maelezo yako ni kuwa udhaifu uko kwako.
 
Biashara yangu ni kwamba napewa mzigo naweka dukani, mzigo wangu pekee ni ule niliouza, kama haujauzika huo unaweza kurudi nilikochukua, mzigo ukiisha unaongezwa
 
Nje ya mada..

Hivi kumbe hutu tudada dada natotuonaga tunauza maduka ya simu full kuringa ringa na kuongea kwa nyodo, kujidai tu slay queen, kumbe tunalipwa laki tu kwa mwezi..?🙄
Mwanamke hakuumbwa afanye kazi ngumu. Tena utakuta hapo kwenye duka la simu kajishikiza tu ionekane anafanya kazi na sio kwamba ana shida sana na hiyo laki moja. Kuna baadhi wanakuwaga na hela nyingi kuliko mabosi wao kwasababu ya kuhongwa. Mambo ya wanawake waachie wenyewe
 
Kusema kweli hakuna mazingira rafiki Kwa Wafanyabiashara wadogo Tanzania.

Imagine huo Utitiri wa Kodi
Fire
TRA
Property tax
Service levy n.k.

Mbaya zaidi wanataka hiyo Kodi wakati mfanyabiashara haujaanza kuzalisha hata shilingi 50 ya Faida

It's unfair 😭
 
Sure, mabinti wapo madukani wanatumia mabando ya elf 3 kila siku, ukichunguza vizuri kuna vidume kama vitatu kila moja kamuungia bando ili wawasiliane video call
 
K

Kufanya biashara mjini shida ndio maana mm ufanya biashara zangu bushi ujenga town ata kodi sitozwi kama utitiri uwo. In short kodi Tanzania zipo town tu.
 
Sure, mabinti wapo madukani wanatumia mabando ya elf 3 kila siku, ukichunguza vizuri kuna vidume kama vitatu kila moja kamuungia bando ili wawasiliane video call
Kuna siku dukani nimepokea msg ya Silent Ocean mzigo umefika natakiwa nilipie kama 1.7m na kwa bahati mbaya kwa target zangu nilidhani utachelewa kwahiyo kwa hiyo siku sikuwa hata na laki kwa sababu ya kununua stock. Wakati ninawaza yule binti akaniuliza vipi mbona kama unawaza.. nikamjibu mzigo umefika na leo sina hela ya kuutoa. Akaniuliza ni Tsh ngapi nikamjibu. Nikashangaa ananiambia nimruhusu aende nyumbani kuniletea hizo pesa. Nilishtuka na kumuuliza mara tatu kama yuko serious. Baada ya muda karudi na hela. Hiyo ndo siku nilielewa kwanini anko wangu aliniambia USISHINDANE NA DADA YAKO. Huyo binti hakudumu sana kazini alikuja kuolewa na kuachishwa kabisa kazi.
 
Nje ya mada..

Hivi kumbe hutu tudada dada natotuonaga tunauza maduka ya simu full kuringa ringa na kuongea kwa nyodo, kujidai tu slay queen, kumbe tunalipwa laki tu kwa mwezi..?🙄

Usishindane na wadada, anaweza akawa na vyanzo kedekede vya pesa...
 
Kufanya biashara mjini shida ndio maana mm ufanya biashara zangu bushi ujenga town ata kodi sitozwi kama utitiri uwo. In short kodi Tanzania zipo town tu.
Kodi zipo Kila mahali Mkuu, hata huko Vijijini Kodi zipo

Hujawahi kutembelewa na Watu wa Halmashauri wakaanza kudai Kodi kwenye hizo biashara zako.

Kama hujatembelewa itakuwa bahati yako, ila binafsi nimetembelewa hadi na watu wa Fire kudai Kodi

Ni utasema ukitokea ajali ya moto wanaweza kuja hata kusaidia kuzima maana hata Vifaa vya Kuzimia hapo Wilayani hawana ila Kodi wanachukua
 
Back
Top Bottom