... uko sahihi to some extent japo pol-ccm wamekuwa very specific gaidi ni mmoja tu, Mbowe, ambaye alikuwa anatafutwa muda mrefu na siku, by coincidence, muda mfupi kabla ya kongamano la katiba mpya akatiwa nguvuni na vyombo mahiri vya usalama baada ya kupata taarifa nzito na nyeti za siri wakishirikiana na vyombo vingine vya kikanda na kimataifa!
... Let's give them benefit of doubt; je, kwa kuwa gaidi hatari sana kwa usalama wa nchi yuko "pahala salama" mikutano ya katiba mpya inaweza kuendelea? Maandiko yanasema, "mdomo wa kweli utathibitishwa milele; bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu." Ndipo tulipofikia kama nchi!