Dai la katiba mpya linaweza kuwa ni ugaidi kwa maana hii

Dai la katiba mpya linaweza kuwa ni ugaidi kwa maana hii

Rais amesema suala hili lisubiri kwanza wakati akiirudisha nchi yetu katika hali iliyo bora kuliko hapo awali kinachoshangaza uharaka wa suala katiba mpya sielewi chadema kwa nini wanalilazimisha kupita maelezo, Kwa vyovyoye hawa ni watu ambao ni waroho wa madaraka na lango lao kuingilia ikulu ili kujineemesha ni kudai katiba kwa nguvu, TANZANIA NI NCHI YA KIMAJADILIANO ZAIDI KULIKO MABAVU YAO, nadhani hekima ni wangeomba majadiliano kuhusu lini serekali inaona ni wakati muafaka wa kulijadili jambo hili.
Kama Tanzania ni nchi ya majadiliano mbona ccm wanatumia mabavu ?
 
Endapo wameomba kuonana na mamlaka husika wavute subra ratiba ya itapangwa wakati utakapofika kwa sasa rais wetu ana shughuli nyingi sana za kurudisha nchi kwenye mstari wake
Lini nchi ilitoka kwenye mstari ?
 
Endapo wameomba kuonana na mamlaka husika wavute subra ratiba ya itapangwa wakati utakapofika kwa sasa rais wetu ana shughuli nyingi sana za kurudisha nchi kwenye mstari wake
Imetoka kwenye mstari upi na anairudisha kwenye mstari upi ?
 
Sidhani kama kudai katiba ni sababu..mbona waliodai katiba ni wengi na hawajapewa kesi ya ugaidi?..mbowe atakua na mambo yake mengine tu nahisi
Kutoka moyoni mwako, na kwa imani ya dini yako (ingawa, Nina shaka kama we' ni muumini wa Dini yoyote imtambuaye Mwenyezi Mungu)unaweza UKAAPA kuwa, unaamini mashtaka aliyotuhumiwa ni kweli?
 
Vyama vya upinzan gan vinavyodai katiba zaid ya mbowe??aanzie na katiba ya chama chake kwanza,why miaka 17 yupo hapo hapo na hatak kuondoka??
Big show hakuwahi kuwa mvivu namna yako hiyo. Kama wote wakitulia bila kuidai itakujaje hiyo katiba mpya ?!. Kila jambo lazima wawepo wasukuma hoja na ndiyo hao Cdm . So usikereke

Katiba za vyama kuwa mbovu , ni kwa sababu katiba mama ya nchi imetoa mwanya huo. Katiba ya Ccm ni mbovu sana kama ilivyo hiyo ya Cdm .
 
Endapo wameomba kuonana na mamlaka husika wavute subra ratiba ya itapangwa wakati utakapofika kwa sasa rais wetu ana shughuli nyingi sana za kurudisha nchi kwenye mstari wake
Kwani ilikua imeenda wapi mpaka kuirudisha kwenye mstari wakati yeye alikua ni sehemu ya serikali iliyokuwepo. Hapa ndio nashindwaga kuzielewa sera za CCM kila Raisi anakuja na mambo yake hakuna consistency mipango yao kwa style hii maendeleo yatachelewa sana maana chama hichohicho lakini hakuna muunganiko kwenye mipango yao kila anayekuja atabomo na kuanza upya nchi haijegwi hivyo. Kiufupi chama tawala kinaogopa kufanya mchakato wa katiba mpya kwa sababu wanaogopa kupotezaa nguvu
 
Endapo wameomba kuonana na mamlaka husika wavute subra ratiba ya itapangwa wakati utakapofika kwa sasa rais wetu ana shughuli nyingi sana za kurudisha nchi kwenye mstari wake
Yaani wewe ni juha sana. Yaani unatoka hadharani kusema nchi ilitoka nje ya mstari nahutaki katiba mpya??
Sasa huoni kuwa walioitoa nchi nje ya mstari walijua hawafanywi chochote kwasababu wanalindwa na katiba iliyopo
 
Lissu unamuona yupo sawa? I,q ni zile zile creaming capabilities ni moja,nguvu ya kuona wanajua kila kitu ni moja, nguvui ya kutokubali kushindwa ni moja hali ya kutoambilika ni moja terrible terrible terrible utu uzima dawa kuishi kwingi kujifunza mengi
 
Usifanye mchezo na katiba mpya, inawezekana huu ndo wembe anaotaka kuutumia mdude..
 
Nimewaza mengi. Nikagundua kwamba kudai katiba mpya italeta hofu ya kupokwa madaraka miongoni mwa viongozi walioko madarakani , hofu hupelekea presha (hypertension) na visukari (diabetes) kupanda, na hatimaye kifo. Hivo basi kudai katiba mpya kunako fanywa na wanaharakati na vyama pinzani ni ugaidi wa kutaka kuua viongozi wa serikali.
Umeconnect the dots vizuri.Unajua ukisha zoea kupanda V8 basi kurudi kwa VITS ni hatari mno
 
Rais amesema suala hili lisubiri kwanza wakati akiirudisha nchi yetu katika hali iliyo bora kuliko hapo awali kinachoshangaza uharaka wa suala katiba mpya sielewi chadema kwa nini wanalilazimisha kupita maelezo, Kwa vyovyoye hawa ni watu ambao ni waroho wa madaraka na lango lao kuingilia ikulu ili kujineemesha ni kudai katiba kwa nguvu, TANZANIA NI NCHI YA KIMAJADILIANO ZAIDI KULIKO MABAVU YAO, nadhani hekima ni wangeomba majadiliano kuhusu lini serekali inaona ni wakati muafaka wa kulijadili jambo hili.

Unayemtetea alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba 2014. Akaongoza wengine kukataa rasimu ya wanananchi (iliyoonekana kuwapunguzia mamlaka viongozi waliopo madarakani na kuwanyima ulaji) na wakaja na Rasimu Pendekezwa ambayo JPM alikuwa akasema sio kipaumbele na SSH anasema apewe muda. Tanzania sio nchi ya majadiliano, kama ingekuwa hivo kwa jambo hili la Katiba tulijadiliana na tume ya Warioba na kisha Bunge la Katiba - kwani umesikia hata wakisema mwaka fulani tufanye majadiliano? Ni majadiliano ya namna gani huchukua miaka karibu 7 sasa bila zao??

Haujui hata “mabavu” yana maana gani. Unaona Chadema imetumia nguvu? Wameita watu kuzungumza tena bila kificho. Wanaotumia mabavu ni wanaozuia majadiliano kwa kutumia polisi. Matakwa ya CCM ni kubaki na Katiba hii. Usiitaje serikali katika jambo hili la Katiba. Sema ni CCM haitaki majadiliano ya jambo hili.

Kama watu wanaowaza kama wewe ni wengi nchi hii, tutegemee kukwama siku zote. Kiwango cha kuwaza kwa chini namna hii ndio kikwazo kwa taifa hili! Mtu asiyeweza kufanya analysis bali anayeangalia mambo kwa nje hana tofauti na yule anayeambiwa “timiza wajibu wako upige” kura halafu baada ya hapo huna wajibu wowote mwingine katika nchi zaidi ya kulipa kodi!!
 
Endapo wameomba kuonana na mamlaka husika wavute subra ratiba ya itapangwa wakati utakapofika kwa sasa rais wetu ana shughuli nyingi sana za kurudisha nchi kwenye mstari wake

Bro, una akili kidogo sana mpaka nimeogopa. Kumbe unakubali kuna mambo hayako kwenye mstari lakini unadhani muda ndio hitaji la marekebisho. Unajua muda huo ni kiasi gani?? Au wewe ni muumini wa “time will tell”?? SSH hakutaja hata muda anaohitaji, ndio maana pressure hii iko! Sioni kama unajua hata hilo!!

CCM ingekuwa na nia njema ya kurekebisha nchi hii ingeweza kufanya hilo sasa hivi. CCM siku zote inahitaji wavumilivu na walio tayari kusubiri kama wewe. Ndio maana huduma za kijamii hakuna miaka nenda rudi na kila mara wanakuja na Kilimo Kwanza, Big Results Now, Uchumi wa Viwanda, Hapa Kazi Tu nk lakini bado unaona matatizo. Inahitaji watu wanaoamini katika kubadilisha watu na sio mifumo (processes) kama wewe ili mtu akifukuzwa kazi au akijiuzulu muonge mambo yamebadilika hata kama anayekuja atapita mulemule.

Waambieni watu ukweli kuwa Kongamano la Katiba linaibua fikra tofauti na zenu na kuwaerevusha wale mnaotaka siku zote wawe chini!! Kuwa hamtaki watu wawaze tofauti na Mwenyekiti!! Kuwa ninyi tu ndio mko sahihi!!
 
... uko sahihi to some extent japo pol-ccm wamekuwa very specific gaidi ni mmoja tu, Mbowe, ambaye alikuwa anatafutwa muda mrefu na siku, by coincidence, muda mfupi kabla ya kongamano la katiba mpya akatiwa nguvuni na vyombo mahiri vya usalama baada ya kupata taarifa nzito na nyeti za siri wakishirikiana na vyombo vingine vya kikanda na kimataifa!

... Let's give them benefit of doubt; je, kwa kuwa gaidi hatari sana kwa usalama wa nchi yuko "pahala salama" mikutano ya katiba mpya inaweza kuendelea? Maandiko yanasema, "mdomo wa kweli utathibitishwa milele; bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu." Ndipo tulipofikia kama nchi!
Constructive point.
 
Reformations zipi ?
Labda Mheshimiwa Rais awamu ya nne aulizwe!! Nakumbuka ndani ya tume miongoni mwao walikuwemo mawaziri wakuu wastaafu wawili, jaji mkuu mstaafu,majaji,Wahadhiri wa vyuo vikuu na wengine wengi wabobefu wa mambo ya siasa,sheria na utawala.wote hawa walikuwa wajinga kutumwa kwenye jambo lisilo na faida!! Vipi kuhusu gharama ya kazi hiyo nani awajibishwe!!
 
Hawa wenzetu naona wanachelewesha katiba kwa malengo makuu mawili.
1. Hawataki tena wengine wajadili hoja za kitaifa kwa sababu ccm hawana majibu tena juu ya hoja hizo.

2. Wanataka waitumie kama ajenda yao kwenye uchaguzi ujao ili wajipatie kura tena.
 
Rais amesema suala hili lisubiri kwanza wakati akiirudisha nchi yetu katika hali iliyo bora kuliko hapo awali kinachoshangaza uharaka wa suala katiba mpya sielewi chadema kwa nini wanalilazimisha kupita maelezo, Kwa vyovyoye hawa ni watu ambao ni waroho wa madaraka na lango lao kuingilia ikulu ili kujineemesha ni kudai katiba kwa nguvu, TANZANIA NI NCHI YA KIMAJADILIANO ZAIDI KULIKO MABAVU YAO, nadhani hekima ni wangeomba majadiliano kuhusu lini serekali inaona ni wakati muafaka wa kulijadili jambo hili.
Mabavu yapi unamaanisha? Mbona wameomba sana majadiliano kwa maandishi! Kufanya kongamano ndio mabavu? Utajengaje hoja kama hukutani na watu mkajadiliana kwenye kongamano?
 
CCM wanamwogopa sana Mbowe.
Wamesha hangaika sana kumharibia miradi na biashara, kuleta mamluki, kumnunua, kumtisha, kumzushia tuhuma.
Kuna wakati hata bunge la Ndugai liliamua kuwa kijiwe cha vigodoro.
RPC Kakwale - KILI nae alitumwa na kutumia nguvu kubwa kumuibia kura za ubunge.
Wataendelea kumshindwa SHUJAA
Sidhani kama kudai katiba ni sababu..mbona waliodai katiba ni wengi na hawajapewa kesi ya ugaidi?..mbowe atakua na mambo yake mengine tu nahisi
 
Rais amesema suala hili lisubiri kwanza wakati akiirudisha nchi yetu katika hali iliyo bora kuliko hapo awali
Chama gani kilisababisha hali kuwa mbaya hapo awali na je hyuy wa sasa anayesema anataka kurekebisha hali anatoka chama gani?
 
Mabavu yapi unamaanisha? Mbona wameomba sana majadiliano kwa maandishi! Kufanya kongamano ndio mabavu? Utajengaje hoja kama hukutani na watu mkajadiliana kwenye kongamano?
URAIS NI TEAM WORK NA SIYO ISSUE YA PERSONAL ISSUE UMWANDIKIAPO BARUA HAIWEZI KUJIBIWA KESHO YAKE THE WAY YOU THOUGHT KUNA MAMBO MENGI YANAPITA NDANI YAKE KABLA YA KUONANA NANYI NDIO MAANA NASEMA YEYE AMESHATUAMBIA TUVUTE SUBIRA BASI YATUPASA TUVUTE SUBIRAAU MLITAKA MKANYWE CHAI BILA KUWEPO NA AJENDA MAALUMU?
 
Back
Top Bottom