Uchaguzi 2020 Dakika 45 na Bernard Membe ITV: Baadhi ya mambo aliyoongea

Uchaguzi 2020 Dakika 45 na Bernard Membe ITV: Baadhi ya mambo aliyoongea

Kwa nini Membe anapinga serikali kuchukua financial loans kununua ndege?

Je, kweli tulikopa ili kununua ndege?
Anasema kwa sababu ndege hairejeshi pesa papo kwa papo kama mafuta ambayo leo kesho unaanza kuuza na kupata faida.
 
Anasema kwa sababu ndege hairejeshi pesa papo kwa papo kama mafuta ambayo leo kesho unaanza kuuza na kupata faida.
Mafuta ukiuza leo kesho unaanza kupata faida? Kivipi?

Biashara yoyote kunakuwa na mtaji unaweka na kuanza kupata faida ni baada ya muda, mfano hiyo ya mafuta: kuanzisha hiyo biashara let say inahitaj uwe na bil 1, so ukiuza leo kesho hiyo billion 1 inarudi?
 
Hahaha! Membe bana. Hivi atafika hadi mwisho wa uchaguzi kweli?

Sasa hivi yupo ITV....

===

Ikiwa kampeni zinaendelea kupamba moto, vituo mbalimbali vya utangazaji vimeanza kuwahoji baadhi ya Wagombea wa nafasi ya Urais wa Vyama mbalimbali.

Wiki iliyopita mnamo September 3, ITV ilimhoji Ndugu Tundu Lissu mgombea wa chama cha Chadema. Wiki hii kituo cha ITV kimemkaribisha Ndugu Benard Membe ambaye ni mgombea kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo. Akihojiwa na Mwandishi wa habari Bi. Farhia Middle katika kipindi kinachoitwa Dakika 45 alieleza mambo yafuatayo:

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe amesema wakati anaondoka CCM na kukaa kama raia wa kawaida mpaka alipojiunga na chama hicho anajisikia kuwa na raha sana kulinganisha na kule alikokuwa.

Amesema ndani ya ACT-Wazalendo kuna vijana wenye akili hajapata kuona na wanajadili, kukosoa na kukosoana chini ya uongozi wa Maalim Seif na baadae wanatoka wakiwa kama timu.

Membe anasema akijilinganisha na wagombea wengine anajiona kuwa ni mtu anayefaa zaidi kutokana na uzoefu mkubwa alionao katika uongozi wa ndani ya nchi na nje ya nchi na ingekuwa dhambi kubwa sana kama asingegombea nafasi ya Urais.

Aidha, ameongeza kuwa fedha za kununua ndege na kujenga reli hazijatoka kwa Watanzania bali kwenye mabenki ya nje na uwekezaji huu hauleti faida ya haraka kwa ajili ya kulipa hayo madeni. Hakuna Serikali duniani inayomiliki ndege bali ni biashara za watu na Serikali huweza tu kuchukua hisa.

Kuhusu Ilani yao
Tutaawachia wafanyabiashara wote waliobambikiziwa kesi, ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani. Uchumi hauwezi kujengwa na serikali uchumi unajengwa na watu

Katika dk ya 47:00 ya hiyo video Membe amefanya Monologue namna hii

Membe: Tarehe 28 wakatupigie kura sisi akina Membe, Mmoja akasema mtatangazwa, Jibu, Tutatangazwa. Hamtaibiwa, Jibu, Sikiliza mimi mwenyewe nilikuwa kwenye hizo shughuli kwa hiyo hakuna wizi mwaka huu

Membe amedai kuwa hakutakuwa na international observers kutakuwa na observers wa ndani tu

Very good, ITV....

Mnafanya vizuri sana kupata nafasi ya kuzungumza na wagombea hususani wa Urais....

Hopefully, wiki zijazo tutamuona Ndg John Pombe Magufuli wa CCM naye akijieleza na kujibu maswali peke yake hapo studio.....

Natumaini pia Bwana Magufuli hataingia studio na daftari la notes alizoandikiwa na Chakubanga Polepole 😀 😀😀 haa haa haa....
 
Mafuta ukiuza leo kesho unaanza kupata faida? Kivipi?

Biashara yoyote kunakuwa na mtaji unaweka na kuanza kupata faida ni baada ya muda, mfano hiyo ya mafuta: kuanzisha hiyo biashara let say inahitaj uwe na bil 1, so ukiuza leo kesho hiyo billion 1 inarudi?
Unaniuliza mimi au unamuuliza membe ?

Mimi nimemnukuu membe alivyojibu tu siwezi kutetea hoja aliyojenga yeye bali naweza kuinukuu tu.
 
Very good, ITV....

Mnafanya vizuri sana kupata nafasi ya kuzungumza na wagombea hususani wa Urais....

Hopefully, wiki zijazo tutamuona Ndg John Pombe Magufuli wa CCM naye akijieleza na kujibu maswali peke yake hapo studio.....

Natumaini pia Bwana Magufuli hataingia studio na daftari la notes alizoandikiwa na Chakubanga Polepole 😀 😀😀 haa haa haa....
Tatizo wanawadhiti sana wahojiwa,Jana membe kila akianza kufunguka vizuri anakatizwa,anapigwa swali jingine naona kama wanakuwa waoga sana kumpatia mgombea Uhuru wa kutosha kutoa ufafanuzi.Kingine je hawafanyi editing? maana hiki kopindi sio live
 
Anasema kwa sababu ndege hairejeshi pesa papo kwa papo kama mafuta ambayo leo kesho unaanza kuuza na kupata faida.
Ana hoja ya msingi.Hii mikopo ya kibiashara ina marejesho makubwa na ndio maanda tunashindwa kuongeza mishahahara
 
Mgombe Urais kupitia ACT amesema hakuna nchi duniani inayomiliki ndege ashangazwa Tanzania kuendelea kununua Ndege
 
Attachments

  • VID-20200908-WA0022.mp4
    2.4 MB
Jasus mbobezi hahahaaaaaaaaaaaaa nyie mliomdanganya mtaenda motoni walahi.
Wabongo nuksi walimwambia tangulia tuko nyuma yako! na yeye akaamini kuwa kuna watu elfu moja watamfuata baada ya kuhamia ACT cha kushanganza hakuna hata mtu mmoja aliyemfuata. Anatia huruma sana huyu mbobezi kabaki peke yake. Kwa sasa siyo 'asset' tena bali ni 'liability' ndani ya ACT na muda si mrefu Zitto atambadilikia maana anaingiza hasara tu.
 
Tatizo wanawadhiti sana wahojiwa,Jana membe kila akianza kufunguka vizuri anakatizwa,anapigwa swali jingine naona kama wanakuwa waoga sana kumpatia mgombea Uhuru wa kutosha kutoa ufafanuzi.Kingine je hawafanyi editing? maana hiki kopindi sio live

..hata mimi hilo nimeliona, kwamba Membe alikuwa anakatishwa akianza kushika kasi.

..hiki kipindi kinazidi kutuonyesha jinsi Magufuli alivyo dhaifu kulinganisha na wagombea wenzake.

..naamini wakihojiwa na wengine, Magufuli atafunikwa na Tundu Lissu, Bernard Membe, na Prof.Ibrahim Lipumba.

..watu wa ccm huwa wanabebwa na watumishi wa serikali, lakini wakiwa wenyewe ni weupe na hawana hoja.
 
Mbinu yao walioitumia CCM na TISS mwaka 2015 kumpandikiza Lowassa upinzani, sasa kwa Membe imebuma watu wameshtuka .
Kwahiyo kuna watu hiyo 2015 walikuwa wanaamini kabisa kuwa Lowassa yupo serious anautaka urais?
 
Mgombea wa CCM Mpya asipojisahihisha ataangukia nafasi ya tano nyuma ya Bernard Membe na Prof. Ibrahim Haruna Lipumba.

Na msimamo wa ligi kuelekea Ikulu kwa kuwepo ktk gumzo la kisiasa mwisho wa mwezi huu wa tisa (september) utasomeka hivi (hapo chini) na hivyo mwezi wa Oktoba yote utakuwa mwezi wa kuteseka sana kwa mgombea wa CCM Mpya na wafiaChama wahafidhina wa CCM Mpya:
  1. Tundu Antipas Lissu
  2. Maalim Seif Sharrif Hamad
  3. Bernard Carmillus Membe
  4. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
  5. John Pombe Joseph Magufuli
Hayo matokeo hupatikana bila tume huru na hata ccm wakiiba kura? maana miaka yote tunaambiwa ushindi wa ccm ni wa kuiba kura.
 
Angekuwa mume wangu ningemshauri aache tu hyo shughuli, sion kitu hapo
 
Katika watu wanaotia huruma ni Mh B membe.why because hawezi kuwa Rais wa nchi hii labda huko mtwara why kwa sababu huko mbele tuendako Lissu atakuwa more popular and strong and why because ACT haiwezi kuwa strong kuliko chadema and so Membe hata akihamia chadema hawezi mzidi Tundu na akirudi CCM hawezi kukubarika mpaka apewe bendera ya chama so amekufa kifo cha mende
 
Back
Top Bottom