Uchaguzi 2020 Dakika 45 na Bernard Membe ITV: Baadhi ya mambo aliyoongea

Uchaguzi 2020 Dakika 45 na Bernard Membe ITV: Baadhi ya mambo aliyoongea

2020 wakileta mdahalo basi utakua mwaka wa kihistoria
 
Hahaha! Membe bana. Hivi atafika hadi mwisho wa uchaguzi kweli?

Sasa hivi yupo ITV.



===

Ikiwa kampeni zinaendelea kupamba moto, vituo mbalimbali vya utangazaji vimeanza kuwahoji baadhi ya Wagombea wa nafasi ya Urais wa Vyama mbalimbali.

Wiki iliyopita mnamo September 3, ITV ilimhoji Ndugu Tundu Lissu mgombea wa chama cha Chadema. Wiki hii kituo cha ITV kimemkaribisha Ndugu Benard Membe ambaye ni mgombea kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo. Akihojiwa na Mwandishi wa habari Bi. Farhia Middle katika kipindi kinachoitwa Dakika 45 alieleza mambo yafuatayo:

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe amesema wakati anaondoka CCM na kukaa kama raia wa kawaida mpaka alipojiunga na chama hicho anajisikia kuwa na raha sana kulinganisha na kule alikokuwa.

Amesema ndani ya ACT-Wazalendo kuna vijana wenye akili hajapata kuona na wanajadili, kukosoa na kukosoana chini ya uongozi wa Maalim Seif na baadae wanatoka wakiwa kama timu.

Membe anasema akijilinganisha na wagombea wengine anajiona kuwa ni mtu anayefaa zaidi kutokana na uzoefu mkubwa alionao katika uongozi wa ndani ya nchi na nje ya nchi na ingekuwa dhambi kubwa sana kama asingegombea nafasi ya Urais.

Aidha, ameongeza kuwa fedha za kununua ndege na kujenga reli hazijatoka kwa Watanzania bali kwenye mabenki ya nje na uwekezaji huu hauleti faida ya haraka kwa ajili ya kulipa hayo madeni. Hakuna Serikali duniani inayomiliki ndege bali ni biashara za watu na Serikali huweza tu kuchukua hisa.

Kuhusu Ilani yao
Tutaawachia wafanyabiashara wote waliobambikiziwa kesi, ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani. Uchumi hauwezi kujengwa na serikali uchumi unajengwa na watu.

Katika dk ya 47:00 ya hiyo video Membe amefanya Monologue namna hii.

Membe: Tarehe 28 wakatupigie kura sisi akina Membe, Mmoja akasema mtatangazwa, Jibu, Tutatangazwa. Hamtaibiwa, Jibu, Sikiliza mimi mwenyewe nilikuwa kwenye hizo shughuli kwa hiyo hakuna wizi mwaka huu.

Membe amedai kuwa hakutakuwa na international observers kutakuwa na observers wa ndani tu.

🤣🤣🤣

Kule kwao walimtimulia mbali kwa kukosa adabu.

Huku nako wamemchinjia baharini.

Namuona atavyopiga magoti na kuomba msamaha ili arejeshwe tena kundini.

Jasusi mbobezi huyo aliyeuingia mkenge wa Twitter na kudhani yeye ndo yeye.

Seriously, hivi kweli kuna watu wanaamini kuwa jamaa ni ‘jasusi’ mbobezi? Like, seriously???
 
Mitandao inadanganya sana ,

Kama lisu wanavyomjaza upepo sasa,

Hataamini kura atazopata.

Wakati Upinzani wakihamasisha watu wao wasijiandikishe CCM ilikuwa ikihamasisha wapiga kura wake kufanya hivyo.

Sasa ngoja tusubiri kilio hapo 28th.
 
Mitandao inadanganya sana ,

Kama lisu wanavyomjaza upepo sasa,

Hataamini kura atazopata.

Wakati Upinzani wakihamasisha watu wao wasijiandikishe CCM ilikuwa ikihamasisha wapiga kura wake kufanya hivyo.

Sasa ngoja tusubiri kilio hapo 28th.
2025 twende na Shangazi 🤣🤣
 
Back
Top Bottom