ChekoFagia
Senior Member
- Sep 20, 2025
- 115
- 339
WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba ameagiza kufutwa kazi kwa daktari aliyekuwa akimtibu msichana mwenye umri wa miaka 18 aliyekuwa na tatizo la uzazi kwa kumdhalilisha kijinsia baada ya kumchoma sindano ya usingizi Urambo wilayani Tabora.
Agizo hilo amelitoa akiwa Leganga wilayani Arumeru mkoani Arusha wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua maeneo yaliyoathirika na vurugu zilizotokea Oktoba 29, mwaka huu.
Dk. Mwigulu amesema daktari huyo alipomaliza kumsikiliza mgonjwa huyo alimdanganya mgonjwa kwa kumchoma sindano ya usingizi na alipokuwa katikati ya sindano hiyo ya usingizi alimdhalilisha kijinsia.
“Mgonjwa alikwenda na mume wake, daktari akamsikiliza akamdanganya kwa kumchoma sindano na kumbaka lakini mgonjwa aliamka usingizi ila alibakwa na daktari huyo, haya ni mambo ya hovyo sana,” alisema Dk Mwigulu.
Amesema nesi alishuhudia tukio hilo na madaktari wengine wameshuhudia na wamethibitisha kuwa daktari huyo alimbaka msichana huyo na ameagiza muhusika anyang’anywe leseni. “Huyu akamatwe na asiachiwe,” alisema Dk Mwigulu na amemuelekeza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, amfukuze kazi.