Les goo...........
Maneno ya Mercy yalinifanya nione kama vile ananinyanyasa yani ananiona mnyonge sana.
Nikajikaza nikawa mpole nikamwambia ajitahidi kuwa na subira asiamini juu ya anayoyadhania juu yangu.
Nilijishusha kwa makusud, na hii kitu ilinipa maana Mercy alipoa tukarudi kuwa sawa.
Zilikuwa zimebaki siku chache twende UE, basi tukajipiga brush final touches ili tukafanye vizur katika UE.
Course works zilikuwa nzuri tu kwahiyo tulikuwa na uhakika UE tunaenda kubonda vizur.
Kesho yake nilimchek Mercy fek nikamuomba tukutane sehem flan sikutaka iwe rum kwangu wala kwake. Nilikuwa nimepanga kwenda kumpa somo aache kushindana na Mercy kwani Mercy hajui chochote kuhusu mission yetu ndomana anavoona tunawasiliana anahisi kunamchezo mbaya unaendeleaj kati yetu.
Tulikutana sehem flan kulikuwa na juice point hukohuko mtaani kwetu.
Nilimueleza kinagaubaga na akanielewa akaniahid kupunguza mashambulizi kwa Mercy lakini alisisitiza sana kwamba anahitaj penz langu.
Nilimsihi sanaaache hayo mawazo na niliona endapo kama nitampiga mashine basi kuna uwezekano akaja kuanza kumvimbia Mercy kwa dhana ya kwamba anashea naye penzi. Nikaona nitajaribu mission kwahiyo nilijikaza sana, alizid kunikumbusha kuhusu hili swala la kumnyandua lakini nikawa nampa ahadi zisizoisha na mwisho wa siku ili kumtuliza nikamwambia wakati wa likizo fupi baada ya kumaliza UE Mercy ataondoka kwao kwahiyo tutabaki na uhuru zaidi.
Huu mchoro nilompa ulimuingia na akatulia kabisa.
Nirudi kwa Dokta na Mercy fek, mpka siku ile naongea na Mercy fek pale juice point alinambia kwamba mission inaendelea vizur lakini Dokta kaomba anitoe out.
Basi kwasbb tulikuwa tunakaribia UE nikamwambia amsubirishe mpka UE iishe then tutatafuta uongo mwingine huko mbele. Tukapiga stor zingine kidogo then tukaachana. Lakini wakati nasepa Mercy fek akapitisha mkono wake kwenye mjegeje wangu madai yake et ni bahat mbaya na niliona alifanya makusud ila sikushangaa sana kwasbb namfaham ni mtu wa aina gani. Tuliachana pale kila mtu akala 50 zake.
Nilirud geto na nikamchek Mercy katika cm ili niende tukajisomee hii ilikuwa ishafika weekend ambayo j 3 yake ndo UE inaanza.
Nilienda kwa Mercy akapika tukale then tukaaza discussion.
Ambacho nilikuwa nafurah pia ni kwamba mimi na Mercy wakati wa kujisomea au discussion tulikuwa tunajikuta kama dada na kaka yani kulikuwa na userious wa uhakika na ilitusaidia sana kwenye masomo kiukweli.
Hatukuwa tunatumia mda mwingi sana kudiscuss kitu kimoja kwasbb tulikuwa tunafocus sana kwenye jambo ambalo tulikuwa tunalidiscuss.
Wakati tunasoma iliingia text katika cm yangu na cm yangu alikuwa nayo Mercy kwasabb alikuwa anaitumia kusoma maswali kwenye past papers ambazo nilizipiga picha kwa cm yangu.
Mesej ilikuwa ni ya Mercy fek ilisomeka "we fala hilo rungu lako limekaa utamu sana, Mercy anafaid"
Ndugu zangu Wana JF hii text ilikuwa chanzo cha mambo yote kuharibika kwani Mercy aligeuka mbogo na akasisitiza niondoke kwake na nisimpigie wala kumtext.
Nilijaribu kujitetea lakini Mercy hakunipa hiyo nafasi nikaamua nijikusanye nisepe.
Njiani nilimpigia cm yule malaya nikamuomba tuonane, safar hii nilienda kwake nikiwa ninahasira sana. Nilipofika nikamkuta kama alivozaliwa na najua alifanya makusud baada ya kujua nilikuwa namfata kwake.
Nilipomkuta vile nikamsihi avae nguo kwani sikwenda kwa ajili ya ule upuuzi. Alianza kunisogelea huku ananiangalia aliponikaribia nikarudi nyuma akanyoosha mikono yake anivute nikaipunch kwa nguvu.
Kitendo cha mimi kumpunch kikamtisha kidogo akarud nyuma nayeye. Akauliza kwani kuna shida gani, nikamjibu hiyo mesej uloituma Mercy kaiona na hapa nimekuja kwako nikiwa nahasira sana nawew kwani Mercy kunifukuza kwa hasira sana na sidhani kama nitaweza kumrudisha awe katika hali nzur na ukizingatia j3 UE. Nilimlaumu sana na yeye alijuta akajitetea kwamba hakutegemea kama Mercy angeweza kuiona mesej akaniomba msamaha akavaa nguo zake chap kwasbb aliona kabisa kwamba kaniudhi sana na nipo out of mood to the maximum.
Basi nikarud home nikiwa katika dimbwi la mawazo nikaona kama vile sina bahat katika ulimwengu wa mapenz kwasababu ugomvi na Mercy ilikuwa almost kila week. Na hii yote ilianza baada ya Mercy kukutana na yule Dokta mshenz kule hospital.
Kwasabb asingekuwa Dokta nisingekuwa close na Mercy fek.
Kesho yake ilikuwa jpil nilienda church na ukizingatia j3 ilikuwa ni UE basi nilienda pia kumuomba Mungu atutangulie katika mtihani. Baada ya kutoka church nikampitia kwa Mercy sikumkuta nikajua kabisa atakuwa bafo hajatoka church. (Mimi na Mercy tulikuwa tunaabudu madhehebu tofauti mimi fpct Mercy kkt)
Basi nikaka nje kulikuwa na tumiti twa michungwa nikakaa pia kulikuwa na vibench vimesimikiwa palepale chini ya miti.
Baada ya dakika 15 hivi nikamuona Mercy kaingia getini. Alikuwa kavaa gauni la rangi ya brown na viatu vyeusi nichwani alikuwa kasuka na ki handbag chake kilikuwa cha rangi ya pink.
Wazee Mercy alijua kupendeza siku hii.
Alipofika nilipokuwa nimekaa akanisalimia kisha akaingia ndani namimi nikamuwahi kabla hajafunga mlango.
Nilipoingia ndani akaniuliza nimefata nini nikamjibu apunguze hasira kwani yote anayodhania ni uongo hakuna la kweli hata moja.
Kabla sijaanza kumuelezea cm yake iliita kuitoa ilikuwa ni namba ngeni.
See you.............
===
Muendelezo soma
Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy