Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Tuendeleee.......

Hapa nikaona kabisa Mercy hakuwa na mapenz na Dokta ila shida ni tamaa za pesa na Dokta alikuwa hana mpango wa kumuoa Mercy ila alihitaji kunikomoa tu. Nilihisi vile baadae baada ya siku moja Dokta kunitumia ujumbe "dogo wanaume tushafanya yetu ole wake hiyo mimba mkaitoe".

Hii text alinitumia siku moja kabla ya Mercy kufanya jaribio la kuitoa ile mimba. Hii text sikumuonesha Mercy niliona kama ntamchanganya tu na Haina maana.

DOKTA ALIMTIA MERCY MIMBA KWA MAKUSUDI NA ALIMLAGHAI KWA PESA ZAKE, HII KITU MERCY MWENYEWE NDO ALINAMBIA.

Niliwaza kama Mercy alikuwa hampendi Dokta ni kwanini alikubali kufanya nae tena kavu siku zake za hatari. Sikupata majibu sahihi nikaamua kuipotezea tu japo niliishia kuamini kuwa pesa ndo ilimshawishi Mercy mpka kubeba mimba.

Swala la Mercy kwenda namimi kwao akanitambulishe sikulikubali niliona Mercy hajafikiria kwa kutuliza akili na pia binafsi sikuwa tayar kuoa mwanamke mwenye mtoto.

SIKU YA KUAGANA NA MERCY ILIKUWA NI MAJONZI SANA.

Nilimsindikiza stand akapanda bus kuelekea kwao. Mimi naye nilibaki kwanza pale town kuna mambo yangu nilikuwa nayafatilia.

Nilikaa kama mwezi hivi ukizingatia hata kodi yangu bado ilikuwa inasoma. Kipindi kile nipo bado pale town niliamua nimtafute Merry, Merry alikuwa tayar kashaondoka kwenda Field alienda mkoa wa dodoma. Nilipomaliza mishe zangu nikapak vitu vyangu nikaondoka nyumbani namimi.

Mawasiliano na Mercy yaliendelea ila upande wangu nilianza kuona Haina tena haja ya kumtafuta mara kwa mara ila yeye alikuwa ananitafuta sana ananisihi nimuoe hata kama bado sijajipanga yeye kwao pesa so shida sana. Aliahidi ataomba pesa ya mtaji tuanze kuzichanga mdogo mdogo ila mimi nikaona kabisa Mercy nikimuoa na tayari kazaa na Dokta nitakua nimejitia kitanzi na kujibuturia kistuli mwenyewe.

Matokeo ya semester ya mwsho yalitoka na mimi na Mercy sote tulifaulu vizur hakukuwa na mtu mwenye kimeo.
Japo nilikuwa bado naumia kumkosa Mercy lawama zangu zote nilizielekezea kwa Dokta na niliahidi kutokuja kumsamehe yule jamaa.

Ilikuwa mwez wa1 mwaka jana Mercy alijifungua mtoto wa kiume na anamuita Johnson, still Mercy ananisisitizia nimuoe lakini bado sioni kama kumuoa Mercy nitakuwa nimefanya jambo la msingi.

Mimi naye hali yangu ya kiafya ilichange ghafla nakumbuka ilikuwa mwez wa 12, 2022 hata graduation sikufanya, nilipatwa na kama kistroke flan yani upande wa kushoto haukuwa sawa. Nilishindwa kutembea, nilipoteza uwezo wa kuongea kwa takriban wiki Moja yani mdomo ulikuwa mzito sana ila nilikuwa natumia maandishi nilipokuwa nahitaji kuongea na mtu.

Nilipelekwa hospital nashukuru Mungu pamoja na madaktari walifanikisha kunipa huduma nikarudi katika hali yangu ya kawaida.
Nilitumia madawa tofaut tofaut ila kuna hiyo moja siwez isahau. Najua kuna wataalam wa afya humu wanaijua vizuri inaitwa "Aten" sijajua kama ndo jina linaishia hapo au linakirefu chake. Hii dawa bhna nakumbuka siku hiyo nilikuwa bado siwez kuongea mtaalam akaagiza ikachukuliwe hii dawa, ni tu vidonge tudogo sana kiumbo, niliambiwa nimeze kamoja tu kwa siku ila mziki wake hii dawa sio wa kitoto.

Hii dawa ukiitumia inakufanya upate ham ya kuongea, inakufanya ujihisi raha yani sinywi na sijawahi kutumia pombe lakini nature ya hii dawa inataka ifanane na tabia ya pombe. Nilikuwa naambiwa nimeze kimoja kwa siku lakini nilikuwa nataman nipige hata tutatu kwasababu yani vilikuwa vinanichangamsha kwanzia kichwani mpka sehem zingine za mwili.

Nilipona kabisa na mpka sasa niko poa.
Mercy naye anaendelea vizuri na mtoto wake na kila siku ananitafuta (hata asubuhi hii kashanitumia text) tunaongea na kuchat saana. Kila siku ananikumbusha kuhusu swala la ndoa na anasisitiza sana nimuoe kwani ananipenda lakini mimi bado sipo tayar kwasababu Mercy tayar anamtoto na sio mtoto tu ila mtoto ni wa Dokta mtu mwenye ROHO mbaya.

NIKIONA KUNA HAJA YA KULETA MREJESHO JUU YA MIMI NA MERCY BASI NITARUDI KUWAPA MREJESHO JUU YA NINI KINAENDELEA LAKINI MIMI BADO SIONI KAMA NINAWEZA KUMUOA MERCY.

Naomba kufunga Uzi wangu kwa kuwashukuru nyote na nawatakia kila lakheri katika safari yenu hapa duniani hasa katika ulimwengu wa mapenzi.

AHSANTENI 🫶🫶🫶.
Bro cha kufanya ungekata mawasiliano nae , trust me hii kuchat chat kila cku ipo siku utakubali ombi lake la kutaka kumuoa.. mtu tabia ya mtu unaipima kwa makosa yake.. ipo siku ukimuoa na atarudia kosa lile lile , wanawake viumbe vingine kabisa .. usiwaamini.. anaweza kuja anakulilia lilia ukamhurumia akishakupata au ukimsamehe , lazma akutende tena maana hawa viumbe hawajali na hua wanasahau mapema. so its better kukata mawasiliano nae , tambua hata siku moja mtu haachi asili yake MSALITI NI MSALITI TUU HATA AKIJIHURUMISHA KIASI GANI KAMWE USIKUBALI KUMRUDISHA. jiulize kwan umezaliwa nae , na usingeenda chuo kimoja ungemjua kwani ?

kinachosababisha na kinacholeta shida hua ni mazoea , sawa kuna muda utamiss moments mlivyokua pamoja , but let her go , na kata mawasiliano nae .. ipo siku atakuteka kiakili na utakubali kua nae trna na ilihari ana mtoto tayari.. So ushauri wangu kata mawasiliano nae
 
Tukupe angalizo tu:
  • Mercy hakupendi, wala usijifariji alifanya vile kwa tamaa ya pesa
  • Angekuwa anakupenda kamwe asingekusaliti, tena kwa dharau zote zile
  • Kuoa single mother ni sawa na kununua kiwanja chenye mgogoro, kamwe usithubutu
  • Mercy ni wa daktari, tayari kuna kiumbe kisichokuwa na hatia kinawaunganisha
  • Anaendelea kukutumia ili umpe faraja tu, kama wewe ungekuwa kwenye hali kama yake asingekupa nafasi
Mwisho; mkiachana halafu mkarudiana mapenzi hayawezi kuwa kama mwanzo na mara nyingi huishia kuachana tu tena.

Lightning never strikes the same place twice.

You can love again, you can do so much better without Mercy. Move on.

Thanks for an educative thread, and all the best in your endeavours.
 
Ndo maana nimemwambia watakuja kuoana. Hii stori ina Part II ni suala la muda tu.
 
Tukupe angalizo tu:
  • Mercy hakupendi, wala usijifariji alifanya vile kwa tamaa ya pesa
  • Angekuwa anakupenda kamwe asingekusaliti, tena kwa dharau zote zile
  • Kuoa single mother ni sawa na kununua kiwanja chenye mgogoro, kamwe usithubutu
  • Mercy ni wa daktari, tayari kuna kiumbe kisichokuwa na hatia kinawaunganisha
  • Anaendelea kukutumia ili umpe faraja tu, kama wewe ungekuwa kwenye hali kama yake asingekupa nafasi
Mwisho; mkiachana halafu mkarudiana mapenzi hayawezi kuwa kama mwanzo na mara nyingi huishia kuachana tu tena.

Lightning never strikes the same place twice.

You can love again, you can do so much better without Mercy. Move on.

Thanks for an educative thread, and all the best in your endeavours.
Msimkatishe tamaa huyu chalii wetu. Kwani hamtaki kupata Part II ya hii stori?
 
Pole kwa maswaiba yote yaliyokupata,nina uhakika umepata relief baada ya kusimulia(umetua mzigo hii ni nzuri sana kwa afya yako).
Ushauri wangu tu unahitaji kusonga mbele wewe bado ni kijana mdogo acha kujitwisha misalaba,naona ingekuwa bora ukafuta namba ya huyo mama.Chukua namba za watu muhimu badili namba,anza maisha upya.Sioni cha muhimu cha kuwafanya muendelee kuwasiliana.
Una mambo mengi ya kufanya kuliko kuendelea kugota upande mmoja wa mapenzi.
 
Hahahaha[emoji23] kweli mapenzi ni upofu, brother don't try again kufall in love hivyo, utakuja kujinyonga ndani ya ndoa pale utakapogundua unachapiwa.
Hata simshangai kwa sababu hizi.

Kuna kipindi nilipiga chini demu wangu kwa sababu ya usaliti wa aina hii, nikaja kudate na demu flani kichwa panzi, Muhuni na hajatulia mara 6 ya demu nilie muacha.

Itoshe kusema ikiwa bado hamjatambulishana, hamuishi pamoja nyie ni marafiki tu. Kila mtu ana cheza na chance zake za kuoa/Kuolewa
 
Dokta hawezi kumwacha dogo akaoshi kwa amani,vinginevyo anafuta kifo cha lazima.Ni ujinga kufa kwa sababu ya mapenzi
ajiulize tuu , kwani saiz Dokta hamtafuti huyo mercy? na unazani hawaongei vizuri ? na unazani matumizi ya mtoto hamtumii? akijijibu haya maswali naamini atakata mawasiliano nae. huyo mercy anakutaka tena sababu kazalishwa na mtu ambae anafamilia yake na hawezi kumuoa.
 
sipo tayar kwasababu Mercy tayar anamtoto na sio mtoto tu ila mtoto ni wa Dokta mtu mwenye ROHO mbaya.
😂😂😂 Jamaa yangu Mimi nilishajua Mwisho wa story ulikuaje yaan story yako ilikua very open Ila hongera kwa kusimulia, hii ina wakuta wengi tu wengine wanapita hapa mda huu wanagongewa watu wao wanaowapenda
 
Back
Top Bottom