Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Pole na hongera kwa maswahibu.
Ila jua tu kua wanawake tunapenda sana attention kutoka kwa wanaume. Mtu wa kukukeep busy with good mornings, umekula etc.
Sasa huyo mercy saiv anasumbuliwa na upweke na anatafuta attention. Mahali pa kupata attention ni kwako. Akipata tu mwanaume wa kumpa attention utaona amepunguza message au kuacha kabisa. Kaa naye mbali sana.
Nashukuru
 
Kumchafua Dokta kwa mke wake ndo ningeuwasha moto zaidi.

Mercy fek alimaliza chuo pia.

Nipo kazini Tanga saizi.

Mercy yupo kwao huko kaskazini.

Madogo zake Mercy (Beata na Kiano) wananifaham na mimi nawafaham ila wazaz hapana.

Nipo na mpenzi flani wa kitanga ameajiriwa ni mwalim.

Sijui kama Dokta anahudumia au lah na sijawahi kumuuliza Mercy juu ya hili.
Utuletee episode kadhaa za binti wa kitanga
 
Kilicho chako hakipotei, mercy hukupangiwa kuwa na wewe. Ulikuwa unalazimisha tu. Na dokta katumika kama catalyst tu ya kukuonyesha mercy ni mtu wa aina gani. Mercy angekuwa hamtaki dokta,angemla block mapema tu.

Umekaa na mwanamke miaka mitatu hajabeba mimba, ila kaenda kwa mwingine miezi kadhaa tu karudi na mimba.

And Nadhani wewe hukuwa karibu sana na mshua wako au hukupata malezi proper ya upande wa kiumeni.
 
Tukupe angalizo tu:
  • Mercy hakupendi, wala usijifariji alifanya vile kwa tamaa ya pesa
  • Angekuwa anakupenda kamwe asingekusaliti, tena kwa dharau zote zile
  • Kuoa single mother ni sawa na kununua kiwanja chenye mgogoro, kamwe usithubutu
  • Mercy ni wa daktari, tayari kuna kiumbe kisichokuwa na hatia kinawaunganisha
  • Anaendelea kukutumia ili umpe faraja tu, kama wewe ungekuwa kwenye hali kama yake asingekupa nafasi
Mwisho; mkiachana halafu mkarudiana mapenzi hayawezi kuwa kama mwanzo na mara nyingi huishia kuachana tu tena.

Lightning never strikes the same place twice.

You can love again, you can do so much better without Mercy. Move on.

Thanks for an educative thread, and all the best in your endeavours.
Ungebold hapa aone vizuri.
 
Mkuu mimi nina uwezo wa kuzipata ila siwezi kufanya hivyo Kw sababu haipendezi..

Kwanini nasema nina uwezo wa kuzipata
Umetoa information ambazo kiIntelligenjia zinaweza kutumika kujua Kuhusu Wewe..
Kiforensic pia zinaweza kukutrace wewe..
Mwaka uliosoma..
Course uliosoma
Mazingira ya shuleni
Shule umesoma miaka mingapi
Baadhi ya majina

Siitaji kufanya hivyo kwa sababu sina haja na wala siwezi kwa sababu zangu maalumu usisahau hata gari la Daktari kwa miaka ya 2020 mpaka 2021..
Umelitja aina ya Xtrail..

But why nifatilie kama ni fiction au ni non fiction cuz Hata kama ni fiction ipo kunifundisha pia na kuniburidisha na kupunguza mawazo na uchovu wa shughuli za kutafuta ugali..

Uncle shusha vitu bhna achana na hayo.mambo
🤣🤣🤣Sema tu unamjua Dr bwana mambo yasiwe mengi
 
Tuendeleee.......

Hapa nikaona kabisa Mercy hakuwa na mapenz na Dokta ila shida ni tamaa za pesa na Dokta alikuwa hana mpango wa kumuoa Mercy ila alihitaji kunikomoa tu. Nilihisi vile baadae baada ya siku moja Dokta kunitumia ujumbe "dogo wanaume tushafanya yetu ole wake hiyo mimba mkaitoe".

Hii text alinitumia siku moja kabla ya Mercy kufanya jaribio la kuitoa ile mimba. Hii text sikumuonesha Mercy niliona kama ntamchanganya tu na Haina maana.

DOKTA ALIMTIA MERCY MIMBA KWA MAKUSUDI NA ALIMLAGHAI KWA PESA ZAKE, HII KITU MERCY MWENYEWE NDO ALINAMBIA.

Niliwaza kama Mercy alikuwa hampendi Dokta ni kwanini alikubali kufanya nae tena kavu siku zake za hatari. Sikupata majibu sahihi nikaamua kuipotezea tu japo niliishia kuamini kuwa pesa ndo ilimshawishi Mercy mpka kubeba mimba.

Swala la Mercy kwenda namimi kwao akanitambulishe sikulikubali niliona Mercy hajafikiria kwa kutuliza akili na pia binafsi sikuwa tayar kuoa mwanamke mwenye mtoto.

SIKU YA KUAGANA NA MERCY ILIKUWA NI MAJONZI SANA.

Nilimsindikiza stand akapanda bus kuelekea kwao. Mimi naye nilibaki kwanza pale town kuna mambo yangu nilikuwa nayafatilia.

Nilikaa kama mwezi hivi ukizingatia hata kodi yangu bado ilikuwa inasoma. Kipindi kile nipo bado pale town niliamua nimtafute Merry, Merry alikuwa tayar kashaondoka kwenda Field alienda mkoa wa dodoma. Nilipomaliza mishe zangu nikapak vitu vyangu nikaondoka nyumbani namimi.

Mawasiliano na Mercy yaliendelea ila upande wangu nilianza kuona Haina tena haja ya kumtafuta mara kwa mara ila yeye alikuwa ananitafuta sana ananisihi nimuoe hata kama bado sijajipanga yeye kwao pesa so shida sana. Aliahidi ataomba pesa ya mtaji tuanze kuzichanga mdogo mdogo ila mimi nikaona kabisa Mercy nikimuoa na tayari kazaa na Dokta nitakua nimejitia kitanzi na kujibuturia kistuli mwenyewe.

Matokeo ya semester ya mwsho yalitoka na mimi na Mercy sote tulifaulu vizur hakukuwa na mtu mwenye kimeo.
Japo nilikuwa bado naumia kumkosa Mercy lawama zangu zote nilizielekezea kwa Dokta na niliahidi kutokuja kumsamehe yule jamaa.

Ilikuwa mwez wa1 mwaka jana Mercy alijifungua mtoto wa kiume na anamuita Johnson, still Mercy ananisisitizia nimuoe lakini bado sioni kama kumuoa Mercy nitakuwa nimefanya jambo la msingi.

Mimi naye hali yangu ya kiafya ilichange ghafla nakumbuka ilikuwa mwez wa 12, 2022 hata graduation sikufanya, nilipatwa na kama kistroke flan yani upande wa kushoto haukuwa sawa. Nilishindwa kutembea, nilipoteza uwezo wa kuongea kwa takriban wiki Moja yani mdomo ulikuwa mzito sana ila nilikuwa natumia maandishi nilipokuwa nahitaji kuongea na mtu.

Nilipelekwa hospital nashukuru Mungu pamoja na madaktari walifanikisha kunipa huduma nikarudi katika hali yangu ya kawaida.
Nilitumia madawa tofaut tofaut ila kuna hiyo moja siwez isahau. Najua kuna wataalam wa afya humu wanaijua vizuri inaitwa "Aten" sijajua kama ndo jina linaishia hapo au linakirefu chake. Hii dawa bhna nakumbuka siku hiyo nilikuwa bado siwez kuongea mtaalam akaagiza ikachukuliwe hii dawa, ni tu vidonge tudogo sana kiumbo, niliambiwa nimeze kamoja tu kwa siku ila mziki wake hii dawa sio wa kitoto.

Hii dawa ukiitumia inakufanya upate ham ya kuongea, inakufanya ujihisi raha yani sinywi na sijawahi kutumia pombe lakini nature ya hii dawa inataka ifanane na tabia ya pombe. Nilikuwa naambiwa nimeze kimoja kwa siku lakini nilikuwa nataman nipige hata tutatu kwasababu yani vilikuwa vinanichangamsha kwanzia kichwani mpka sehem zingine za mwili.

Nilipona kabisa na mpka sasa niko poa.
Mercy naye anaendelea vizuri na mtoto wake na kila siku ananitafuta (hata asubuhi hii kashanitumia text) tunaongea na kuchat saana. Kila siku ananikumbusha kuhusu swala la ndoa na anasisitiza sana nimuoe kwani ananipenda lakini mimi bado sipo tayar kwasababu Mercy tayar anamtoto na sio mtoto tu ila mtoto ni wa Dokta mtu mwenye ROHO mbaya.

NIKIONA KUNA HAJA YA KULETA MREJESHO JUU YA MIMI NA MERCY BASI NITARUDI KUWAPA MREJESHO JUU YA NINI KINAENDELEA LAKINI MIMI BADO SIONI KAMA NINAWEZA KUMUOA MERCY.

Naomba kufunga Uzi wangu kwa kuwashukuru nyote na nawatakia kila lakheri katika safari yenu hapa duniani hasa katika ulimwengu wa mapenzi.

AHSANTENI 🫶🫶🫶.
Aiseee pole sana ,Nimeumia hapo ulipopata stroke kisa mapenzi,,,Mungu akupe Mtu sahihi,na usichukie madaktari ni watu muhimu sana kwenye jamii achana na huyo Mmoja mshenzy...
 
Back
Top Bottom