Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Tuendeleee.....

Ile text ya jamaa ilinitoa mchezoni kidizain nikaona jamaa anaenda kuharibu furaha yangu na maisha yangu.
Nilipata wazo la kuchukua namba yake ili nimtafute tuongee kama wanaume.
Nilimchek kesho yake baada ya Ile siku alotuma text.
Nikampigia nikamueleza politely nakumbuka niliwambia maneno haya "wewe tayar ni Dokta means ushatimiza baadhi ya ndoto zako na unachanzo kizuri cha uchumi, ebu naomba kama unampango wa kumtaka Mercy kimapenz achana naye yule ni wangu na tuna ndoto nyingi na malengo mengine ukimchukua yule mimi sidhani hata kama chuo nitamaliza najua nitachanganyikiea then nitadisco"
Jamaa alicheka sana mpka nikajiona kam nimejishusha sana na nimekubali kupoteza mpambano.

Dokta alinijibu akasema, "dogo kama lengo lako ni kusoma basi soma ila kama umekuja chuo kutafuta mke basi safar yako ni ngumu sana.
Nikaona Dokta kadhamilia nikakata cm.
Nikawaza nifanyaje. Kumbuka huo ni mwaka wa3 tuenda kumaliza sem1.

Siku Ile niliwaza mambo mawili.
Moja niliwaza nimpige mimba Mercy ili nijihakikishie ushindi ndani ya dk90 ili mimi na Dokta tusiende mpka penat.

Swala la pili, pale napoishi ninabraza ambaye anafanya kaz tanapa huwa anakuja mara moja Moja sana mara nyingi anakuwa kazini maporini huko kuna makambi yao. Sasa kwa mwez ule jamaa alikuepo ni bro ambaye tunaheshimiana sana mpka sasa na jina lake siwez kuliweka wazi. Huyu mwamba alinisaidia pakubwa.

Niliwaza hukumshirikisha mwamba, of course ni muhuni muhuni na sigara kubwa alikuwa anapeleka sana sana yani nilikuwa niliingia kwake kwanzia seburen mpka chooni ni harufu ya ganja tu.
Nilimshirikisha kuhusu Dokta kisha nikampa wazo kwamba tumtafute yule Dokta Ile yeye brother amwambie tena aachane ma Mercy maana kwa yale maneno yake siku ile nilipompigia yalinitoa relini kabisa.

Huyu brother anagari yake moja Subaru Forester, kwahiyo siku hiyo akanambia inabid tumtafute physically sio kwenye cm tena. Nikaona wazo zuri, nakumbuka ilikuwa weekend Mercy yupo kwake mimi nipo magetoni.
Tulijiandaa tukachukua kigari chetu tukasepa town. Nilimuelekeza brother office ya Dokta na jinsi alivo ili aende kumchek kama kaingia asubuh au anashift ya saa6 mchana. Maana siku Ile tulivoenda na Mercy niligundua kwamba pale kuna shifts, yani asubuh mpka saa6 anatoka mtu anaingia mwingine.

Bahati nzuri brother alimkuta yule Dokta yupo kazini na muda ule ilikuwa kaka saa4 na nusu hivi.
Tuliamua kwenda juice point Moja ipo karibu na hosii tukakaa tukawa tunapata juice huku tunasbr jamaa atoke tumdake.
Tulikaa sana, kufika saa sita kasoro tukamuona katoka. Alikuwa anaongea na cm basi nasisi tukasogea karibu yake.
Alipomaliza kuongea na cm tukamsemesha tukamuomba tuongee naye.
Hakuwa na hiana kasogea tulipo.
Tukasalimiana naye tena pale then bro akamuliza kama Dokta ananikumbuka akasema hana kumbukumbu vizur.
Nikaona so kesi nikamuelekeza akasema kanikumbuka tyr.

Basi bro akaanza kuongea pale. Kikubwa alichomwambia Dokta ni kwamba mimi ni mdogo wake. Na anajua kuwa Nina mpenzi anaitwa Mercy na tunapendana sana. Bro akamuomba kistarab kwamba hakuna haja ya vita kuoneshana nani zaid ila kama Dokta akishindwa kuwa muelewa basi hata sisi vita tunaiweza. Bro aliongea huku anatabasam then ghafla tukamuaga bro akamuomba azingatie between the lines yake maneno aloambiwa. Then tukapanda kigari chetu tukaishia mbali.

Nilimshukuru sana bro na hapo nikajisemea kuwa tyr vita nishashinda na Dokta kashaweka silaha begani.
Kipindi tupo njiani bro aliniomba twende mpka kwa Mercy akamchek maana toka bro aje safar ile hakuwah kuonana na Mercy. Tulipita dukani kununua yoghurt na mkate tukanyooka mpka kwa Mercy. Tulipofika getini nikamchek akatoka, tulikuwa katika gari bado kwahyo alivoiona gari akajua kabisa tutakuwemo ndani.

Alisogea nikafungua akaingia. Wakasalimiana, kapewa yoghurt yake na mkate tukasema sisi hatuingii ndani nikamuahid kurud badae. Mercy alifurahi sana bas tukageuza kurud home.

Kumbuka hiyo michongo yote na misuguana na Dokta Mercy hakuwa anajua. Niliamua kupigana vita kimya kimya.

See you..............

===
Muendelezo soma Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy
Ulianza kufeli Hapa.Vita ya Kugombea Mwanamke huwa ni vita ya HISIA zaidi na SIO Physical
 
Condition yake aliyosimulia lazima tujue ilikuwa ni Artane.

Mara nyingi side effects za dawa nyingi hufanana ila hutofautishwa na side effects chache
Mkuu napenda tuelimishane ili namimi nipate uelewa..

Kwanini unafikiri Ni artane?
Alikuwa na Any condition suggestive kwako kupewa artane kama Parkinson au any stiffness?
Alikuwa na Tremors? Alikuwa Tonic Au ,Clonic?

Probably kwangu mimi ningewaza Atenolol..Kwanini?

Atenolol ni Beta Brocker na Probably Inatibu Pressure na Inareduce kama sio Kuprevent Further Effects and complication ya stroke..
 
Kumchafua Dokta kwa mke wake ndo ningeuwasha moto zaidi.

Mercy fek alimaliza chuo pia.

Nipo kazini Tanga saizi.

Mercy yupo kwao huko kaskazini.

Madogo zake Mercy (Beata na Kiano) wananifaham na mimi nawafaham ila wazaz hapana.

Nipo na mpenzi flani wa kitanga ameajiriwa ni mwalim.

Sijui kama Dokta anahudumia au lah na sijawahi kumuuliza Mercy juu ya hili.
Uko maeneo gani Tanga kiongoz? Kama ni hapa town basi nicheck inbox tukutane forodhani kupunguza machungu ya hawa jinsia nyingine
 
TANGA-KOROGWE
Kuna msemo sikio la kufa halisikii dawa, but kama unataka kuishi maisha ya amani hapa duniani mpaka siku Muumba wako atakapokuita, ACHANA NA MERCY, MSAHAU MERCY, ACHA UKARIBU WA AINA YOYOTE NA MERCY, HESABU HAKUWA FUNGU LAKO. Lakini if you ever, ever marry her atakuwa kaburi lako. You knw why? ameshaujua udhaifu wako, so she knws how to manupulate you and how to control you. Na sisi wanawake tukishajua kuvitumia hivyo vitu kwa mwanaume AMEISHA.
 
Kuna msemo sikio la kufa halisikii dawa, but kama unataka kuishi maisha ya amani hapa duniani mpaka siku Muumba wako atakapokuita, ACHANA NA MERCY, MSAHAU MERCY, ACHA UKARIBU WA AINA YOYOTE NA MERCY, HESABU HAKUWA FUNGU LAKO. Lakini if you ever, ever marry her atakuwa kaburi lako. You knw why? ameshaujua udhaifu wako, so she knws how to manupulate you and how to control you. Na sisi wanawake tukishajua kuvitumia hivyo vitu kwa mwanaume AMEISHA.
Nimekupata nashukuru
 
Kuna msemo sikio la kufa halisikii dawa, but kama unataka kuishi maisha ya amani hapa duniani mpaka siku Muumba wako atakapokuita, ACHANA NA MERCY, MSAHAU MERCY, ACHA UKARIBU WA AINA YOYOTE NA MERCY, HESABU HAKUWA FUNGU LAKO. Lakini if you ever, ever marry her atakuwa kaburi lako. You knw why? ameshaujua udhaifu wako, so she knws how to manupulate you and how to control you. Na sisi wanawake tukishajua kuvitumia hivyo vitu kwa mwanaume AMEISHA.
Pia kusikia kwa kenge mpaka sikio litoke damu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Rafiki yangu Mbwambo alinigundua kwamba naenda kuharibikiwa, kuna siku alinifata akanambia anahitaji kuongea namimi nakumbuka ilikuwa tupo chuo kwahiyo tukapanga baada ya vipindi tutaongea wakat tunarud kitaa maana Mbwambo pia alihamia kitaa.
Dada kazingua ikabidi Bwashee aku save maana ulikuwa unaangamia.
 
Nilichokiona mimi kwenye somo hili bwana Admired bado anampenda Mercy kutoka moyoni kikwazo ni mtoto tu kulingana na maandishi yake na pia nadhani amekutana na wasichana kadha wa kadha lkn wengi hawajafit kwenye vigezo vya jamaa ikiwemo huyo Marry yaani ilotokea emergence lkn hafit kwenye cretaria za msela

Sasa nini kitatokea mbeleni!!!?

Hapa kuna mambo wawili ambayo yataendelea kumtafuna jamaa mpk aje mwanamke wa vigezo vya Mercy na si suala la rahisi kufanikisha japo inawezekana akiwa mvumilivu

Pili jamaa akimuoa Mercy hakika mateso hayatakoma kwake labda Dr afe maana yeye ( dr ) yupo kwa ajili ya kumkomoa jamaa yetu na anajiona mshindi na hana mpango hata na huyo Mercy wa kumuoa hata mke wa pili

Tatu ,kama inawezekana mshauri Mercy aolewe na mtu mwingine kabisa asiyejua background ya nyie wawili ( dr na wewe) hiyo itamleta amani ya kudumu

Nne, kwa kuwa binti alijigeuza mwili wake kuwa chombo cha starehe na hakujali hasara aliyokuletea ikiwemo ya afya yako nadhani ni vzr uendelee kumpelekea moto pasipo kumshtua kama jinsi alivyopretend kuwa hamna kinachoendelea ili hali alijua nini anafanya pasipo kujali utaumia kiasi gani

Kwa wewe usijali dr anamla au hamli ,anawasiliana nae au laa ,anahudumia au vp wewe mpige pu...mbu tu siku akili ikimwijia ajue anatumika kote kote basi atachagua njia sahihi kwake
 
Hapa ndo ulipotibiwa
Screenshot_20240226_130413_Maps.jpg

Screenshot_20240226_130305_Maps.jpg



Unaikumbuka Hii offisi unamkumbuka nani kati ya hao..
images (12).jpeg
 
Nmemuonea huruma sana
Ila dokta Ana ujinga mwingi kaamua kumkomoa dogo
Mercy nako kajinga sana yaani kameingia Mtegoni kwa vipesa vya lunch na lift za chuo
Hafai kabisa usimuoe atakuja kukupiga tukio huko mbeleni
Unajua zile akili za kichuochuo hiyo x-trail akipandishwa alikuwa anaona kama ya kwake vile
 
Mkuu napenda tuelimishane ili namimi nipate uelewa..

Kwanini unafikiri Ni artane?
Alikuwa na Any condition suggestive kwako kupewa artane kama Parkinson au any stiffness?
Alikuwa na Tremors? Alikuwa Tonic Au ,Clonic?

Probably kwangu mimi ningewaza Atenolol..Kwanini?

Atenolol ni Beta Brocker na Probably Inatibu Pressure na Inareduce kama sio Kuprevent Further Effects and complication ya stroke..
Dr achana na Hizo dawa,tunataka mwendekezo wa series baada ya Mercy kujifungua unampa Matunzo mtoto?au ndio anakula ugali wa Babu yake?
 
Back
Top Bottom