Niliyoyaona mpaka mda huu:
Mosi, wengi wetu tunamuona mercy mbaya, huenda kweli alifanya vibaya lkn je alianza kuwa mbaya bilasababu?
Baada ya kukutana na text za ajabu ajabu toka kwa mwamba alianza kuumia na Mara nyingi alilalamika siku akichoka akija kuanza yeye asishtuke au kushangaa, kwahiyo mercy kwakifupi alilipiza baada ya mwamba kumwaga ugali yeye akamwaga mboga, kwahiyo Mercy asilaumiwe sana.
Pili, dokta alifanya aliyofanya baada kupigwa mkwala na mwamba pamoja na mzee wa miganja, kwahiyo ilikuwa iwe jua iwe mvua na kwa gharama yoyote amle mercy ili arudishe heshima yake na amefanikiwa katika hilo, ndio maana kila alipokuwa magetoni alikuwa anakutext kukwambia kuwa sasa namtafuna dem wako, na alikuwa anamleta chuo makusudi ili kuhakikisha unaumia vilivyo, hapa wachambuzi wa fasihi tunasema mhusika ameitendea haki nafasi ya uhusika wake, tumpe tu maua yake hata kama anawakera, na hapa kuna somo kubwa usiende kumpiga mkwara mwanaume mwenzako ila muombe kwa unyenyekevu akuachie kipenz chako, wanaume huwa waelewa sana.
Tatu, kwako mwandishi na mhusika mkuu wa uzi huu, ulifanya makosa kadhaa baada ya kuona viashiria ambavyo sio vizuri kwa penzi lako lkn ulivifumbia macho na mwisho wa siku ulipata ulichokipanda, hapa tunajifunza katu tusidharau dalili ndogo ndogo kwani mwisho wa siku huwa ni majuto.
Nne ,Usifanye jambo kwa hasira eti kwakuwa unataka kumkomoa mtu kwani mwisho wa siku hasira hasara, hapa mhusika mkuu ni mercy alidhani anamfundisha adabu mpenzi wake kumbe anajikaanga na mafuta yake mwenyewe.
Mwisho, mwanaume haijalishi unampenda vipi mwanamke hakikisha mda wote unabakia kuwa mwanaume kwa maamuzi na vitendo.
Ni hayo tu!