PICHA NZIMA YA YANAYOENDELEA YANAANZIA KATIKA HII EPISODE.
Tuendeleee.......
Mwezi wa 10 katika harakati zangu, ilikuwa nampeleka mtoto wa dada skul. Mtoto wa dada yangu wa tatu kuzaliwa, huyu mtoto ni wa kike alikuwa anaishi na mama mkubwa hapo Kilimanjaro moshi. Huyu dogo now yupo form town means mwaka jana alikuwa form one na alihama kutoka hiyo skul ya moshi akaletwa huku Tanga katika skul flan.
Mimi ndo nilipewa jukumu la kumpokea na kumpeleka skul kurepot. Nilipofika skul kama kawaida nikafata taratibu zote na dogo akapokelewa.
Sasa katika harakati za kumripotisha dogo pale skul nikaonana na madam ni second mistress pale skul.
Ni mwanamke mbichi tu japo kanizid kama miaka miwili (inanifanya nisite kumuoa). Huyu binti niliona kama nimemuelewa hivi lakini sikuwahi na uhakika kama ni kweli au ni macho ya kifisi tu kama ya brother INSIDER MAN kwa akina Asmah, Lucy, Marry na Vicky.
Nilifanikiwa kumuomba namba na alinipa bila ajizi, nikaanza kuwa namtafuta nayeye anarespond. Mwanzo nilikuwa namtafuta kumuuliza maendeleo ya anko wangu dogo anaitwa Gisela.
Nikawa nauliza maendeleo ya Gisela anasema dogo yupo poa na anaonekana kuwa smart na mtu makini (of course yupo poa kichwani). Hii skul ni ya private ada imechangamka kimtindo.
Mawasiliano na huyu madam (nimuite Mage, fake name), tulizidi kuzoeana na mpka ikafikia hatua nikaanza kutupa nyavu. Kifupi nilipambana sana mwisho wa siku madam akajaa na nikaanza rasmi kudate naye.
Huyu Madam Mage yupo smart sana nafikiri ndiyo maana hata kapewa u second mistress akiwa na umri mdogo tu ingali wakubwa kumzidi wapo pale skul.
Huyu Madam Mage tumpe maua yake kabla hata sijaanza kuelezea ni mambo gani special ameyafanya na anaendelea kuyafanya hasa katika hili sekeseke langu na Mercy kwasababu Mercy bado haelewi namimi kuna muda nashindwa kufanya uamuzi sahihi japo Madam Mage shemej yenu na wifi yenu wa faida anaplay part yake vilivyo kabisa.
Nimewawekea picha ya mesej za Mercy alinilazimisha niende kumuona kwao huku akidai kuna mipango madhubuti kama familia wameiweka ili kuhakikisha tunaoana mimi na Mercy na tunaishi maisha bora.
Kwahyo saivi hii vita siyo yangu dhidi Mercy tu bali ni yangu na familia ya Mercy kiujumla.
Mercy amekuwa haelewi japo nimemwambia tayari kwamba nipo na mchumba wangu na tuna mipango ya kuoana. Baada ya kukwambia hiki kitu ndo ni kama nimechochea moto kwasababu anaomba nimpe namba ya huyo mchumba wangu Mage amuombe kistarabu kama mwanamke mwenzake aniache mimi ili nimuoe yeye Mercy akidai kwamba yeye ndo wa kwanza kuingia katika uchumba namimi ila kwa bahati mbaya mambo yakavurugika (siku hii nilicheka sana).
Kuna wakati nawambia Mercy ni kama kachanganyikiwa kwasababu kafikia hatua mbaya eti mimi nitoe namba ya Madam Mage (mchumba wangu) nimpe yeye ili avuruge mahusiano yangu. Hii kwa akili ya kawaida tu ni kitu ambayo ni ngumu na haiwezekani mimi nimpe Mercy namba ya Madam Mage ni hakuna.
Upande wangu mchumba wangu Mage nishamueleza kuhusu Mercy na anaelewa na nimuelewa kwahiyo huwa hata Mercy akituma sms, alipiga cm Mage huwa hamind kwasababu anajua kinachoendelea. Ila cha zaid tu huwa ananisihi nifanye maamuzi sahihi kwani maisha yanahitaj utulivu sana na sio kila kitu kinahitaji uzingatie hisia bali uhalisia.
Mpka saivi mzani umezidi sana kwa Madam Mage kwani nimenotice vitu flan vya msingi sana ambavyo mage anavyo ila Mercy anazingu.
Mfano: Mage anahali flani ya kujishusha sana akikosea au tukigombana huwa anajishusha kitu ambacho Mercy pia anacho ila anazidiwa na mage (Magnitude).
Kuna siku nilikuwa kazini kuna kazi flani ni ya kutumia nguvu ila akili zaidi. Siku hiyo Mage alikuwa kaniomba nimuwekee tsh 50k alikuwa anaongezea anunua cm mpya maana cm yake iliibiwa siku hiyo alikuwa anaenda kununua Samsung note 10 plus gb256 ni hizi used from abroad.
Bajet yake ilikuwa kama 550k hiyo ni Bei ya used sijajua brand new Bei yake ni ngap. Kwahyo aliniomba nimuongezee kama 50k tu nyengine anayo. Nikasema sawa, sas muda huo mimi nilikuwa bize kuifanya ile kazi hafu na Mage katoka ckul anaenda mjini ili kuifata ile cm kwahyo akawa anaharaka sana nimuwekee katika cm yake mpesa. Muda huo namimi nakimbizana na muda niimalize kazi niwasilishe.
Mage alipiga sim na kutuma texts mimi sikuwa na time na cm na nilikuwa dizaini kma nimesahau kama nilitakiwa kumuwekea pesa Mage.
Mage alikasirika akatuma text "DeMostAdmired mbona kama unafanya mambo ya kitoto acha upuuzi". Ile text nilikuja kuiona baadae na nilipoiona nilikasirika sana. Kwasabb nilikuwa nina hasira sikutaka kumjibu chochote kwasababu najua ningemjibu vbaya sana nikamkwaza.
Niliamua kuanza transaction ya kumuwekea ile 50k lakini kabla sijaingia kwenye menu ya mpesa niliona text inaingia ya Mage inasema "am very sorry my love DeMostAdmired najua nimekukwaza ila nisamehe zilikuwa hasira na usiwaze pesa nishaikamilisha na cm nishanunua".
Haya maneno ya Mage yalinifanya nipate furaha isiyo kifani na ndo aina ya wanawake naowapenda yani kakosea, kajua kosa lake na akajiongeza kuomba msamaha kabla sijacomplain. Namimi nilijiongeza nikamtumia 80k badala ya 50k, akanitumia mesej " honey nilikuwa nishakamilisha na cm tayar ninayo hata hivo nakushukuru na nakuomba unisamehe sana kwa yale maneno". Nikamjibu usiwaze I understand and love you so much.
Sasa Mercy kitu hiki hana. Mercy alikuwa nikimuudhi kama nipo kwake alikuwa ananifukuza Sasa hii ni ishara ya dharau, na vijitabia vingine vingi vingi vya ajabu alikuwa navyo japo nayeye anamazuri yake mengi ndomana hata nilimpenda sana.
See you........a