Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Kutoa si unatoa tu kwani naondoka nayo, yaani kitumbua nacho ni kitu cha kumnyima mtu kweli, nahuku raha tunapata wote, tena mwanamke ndo anapata raha zaidi ya mwanaume. Halafu PM yako umeifunga dah
Kwahiyo upo kutafuta vitumbua?? Mbona hivo hata binamu zako wanavyo tena vilivyoungua we jisevie kwenu mkuu!
 
🤣🤣🤣Eti Anitha una kumbuka vitu vya kijinga sana
😂😂😂😂😂 Anitha, Anitha wangu.
Nimekumbuka kuna siku tulitoroka tukaenda show ya Matonya, sasa si mzuka ukapanda akajirusha ili wamdake!! Aiseeee watoto wa Moro jau!!! Walimdaka wakamvua cheni, viatu mpk jeans kisha wakamtupia jukwaani na pensi lake la reebok 🤣🤣🤣🤣🤣
 
😂😂😂😂😂 Anitha, Anitha wangu.
Nimekumbuka kuna siku tulitoroka tukaenda show ya Matonya, sasa si mzuka ukapanda akajirusha ili wamdake!! Aiseeee watoto wa Moro jau!!! Walimdaka wakamvua cheni, viatu mpk jeans kisha wakamtupia jukwaani na pensi lake la reebok 🤣🤣🤣🤣🤣
🤣🤣🤣🤣🤣Enzi unasoma Forest?mna roho mbaya sana
 
🤣🤣🤣🤣🤣Enzi unasoma Forest?mna roho mbaya sana
🤣🤣🤣🤣 vibaka wa sabasaba na chamwino sio mchezo mchezo..!!! Moro napamiss sana!!
Halafu ndio kipindi game limeanza kumkataa wakaona nao wamalizie kumpotezea kabisaaa!!

Kuna nyingine hiyo nilitoroka hostel nikaenda club nipo na shosti yangu na bwana ake manager wa kampuni moja ya mtandao wa simu, ndio alitusponsor basi nimevaa high heels zangu najiachia mwenyewe kwa stage huku nimekunywa reds zangu nimewaka…!!
Mara nikamkanyaga mdada walikuwa wanacheza na mpenzi wake pembeni yangu..!!!
Yule dada akapanic akanisukuma weeee na zile heels nusu ning’oe meno 🤣🤣🤣🤣

Nikadondoka kile kisketi kikapanda juu chini kote kunaonekana, niliinuka kwa hasira nikavua konkonko nikamfata yule dada nimtwange navyo hapo reds ndio zinaongea, nimemkaribia nikashangaa jamaa yake kanidaka na bonge la mtama 🤣🤣🤣🤣
Nikaanza kutukana akaja rafiki yangu naye akanunua ugomvi. Lakini nikawa namshangaa mbona haonyeshi cheche!! Kumbe kuna kitu alikutana nacho. Akapigwa butwaa

Nikaona ujinga ngoja nikapambane mwenyewe, nikabeba chupa sasa liwalo na liwe kwenda kumchoma nayo yule dada aiseee!! Hapo kwanza ncheke 🤣🤣🤣

Kumbe yule mdada ni dada yangu naye alitoroka home akaja na bwana club. Hasira zilizidi mara mbili nimeshindwa kukamilisha kisasi changu. Akaanza kunipoza na kunigombeza kwann sisomi nahangaika kwenye maclub usiku…! Hapo kiuno kinauma balaa na ule mtama wa yule bwanaake😏😏

Yule bwana ake baadae nilimfanyia figisu moja hiyo mpk wakaachana ila hakujua km ni mimi nilitengeneza ule mchezo mpk leo.
Ila bado kinaniuma mpk kesho.
 
Tuendeleee..........

Kwanza kabisa kuna kitu ni kama ninakihisi, ni kwamba ninahisi Mercy aliwambia kwao kwamba mwanaume mwenye mtoto ni mimi na siyo Dokta.
Nahisi pia kawadanganya kwamba nimekengeuka sitaki kumuoa mtoto wao kwasababu sasahivi hili sekeseke hadi wao wazaz wa Mercy wameingilia kati. Na bila shaka kama Mercy angekuwa kawambia ukweli kwamba yule mtoto sio wangu ni wa Dokta basi wazazi wangedili na Dokta na siyo mimi.

Mercy namuona ni kama anatumiwa na shetani kunivurugia mambo yangu.
Mercy amepanga mipango ya kuhamia Tanga mahali nilipo ili awe karibu na mimi. Nilijaribu sana kumpiga biti nyingi za makatazo juu ya mpango wake kwani ataniharibia mipango yangu na Mage na ukizingatia Mage tayari tupo naye vizuri sana yani mapenzi ni moto sana saivi.

Mage ni mwanamke mzuri na mpka sasa siamini ni kwanini nilimkuta Mage akiwa single Hana mtu najiuliza je alikuwa anawakataa watu au alikuwa hatongozwi maana Mage ni wife material haswa. Ila nachokiamini Mage hakuwa single ila kaamua kuweka utoto pembeni na kuwa na mimi 100%.

Nahisi pia ni mpango wa Mungu Mage kuwa namimi kwasababu amekuja wakati sahihi wakati ambao nilikuwa nahitaji sana mtu wa karibu ambaye ataridhia kuwa namimi no matter what.

Yale matatizo ya moyo niliyoyapataga
nahisi bado kwa kiasi kidogo yapo bado japo kadri siku zinavokwenda yanazidi kupotea na nazido kuimarika.
Kuna muda nahisi hasira kwa vitu vidogo vidogo, pia kuna muda nadhoofika moyo unakuwa unapiga kwa nguvu mpka nikiweka kiganja juu juu tu katika sehem ya moyo nakuwa nafeel moyo unavopiga kwa nguvu Sasa hii hali inanifanyaga nidhoofike na pia nakuwa na shorten breath.

Mage tayari anafaham hali yangu halisi na ananipa kampani ya dhati sana mpka naona kama vile ni special from God.

Kuna siku nipo na Mage nakumbuka ilikuwa siku ya j pili weekend maana Mage anakuwaga na nafasi ya kuja kunitembelea siku za weekend.
Siku hiyo tupo bed tunapiga stors meseji ya Mercy ikaingia "DeMostAdmired mimi nawewe tulipanga mengi makubwa, kilichotokea mimi kukusaliti mpka kuzaa na Dokta ni kama ajali tu na sikufanya kwa kukusudia naomba unielewe. Dokta nimeshampiga marufuku hanitafuti tena na Hana kabisa mazoea na mimi. Nisamehe kila siku nakuomba msamaha siyo kwamba sitongozwi natongozwa ila nahitaji kuolewa nawewe niambie nini nifanye ili urudishe moyo wako kwangu mimi nipo tayari".

Hii mesej hata Mage ilimpa mashaka japo tayari ameshamzoea Mercy na vimbwanga vyake lakini siku hii Mage alisimama akanambia " baby huyu mwanamke sasa naona anavuka mipaka, mimi sipo tayari kuona unatumiwa mamesej ya kubembelezwa namna hii na wewe ni binadamu kuna kipindi kitafika utaanza kuregea na kuanza kumpenda huyu Mercy"

Mage alinambia either tubadirishane laini yeye atumie yangu namimi nitumie yake au lah basi nivunje hii yangu nisajili nyengine ili Mercy asinipate tena.
Niliona option ambayo kidogo ni nzuri ni hii Option ya pili japo niliwahi kubadirisha laini lakini alipata namba yangu kupitia watu tulomaliza nao chuo ndo walimpa namba yangu na wembe ukawa ni uleule.

Nilimuahidi kwamba atulie mimi ni mwanamume ninaakiki timamu nafahamu Mercy siyo mtu mzuri kwahiyo asiwe na wasiwasi kabisa.
Alikubali japo kwa shingo upande

Siku hii Mage aliwaka sana mpka nikaona kama vile Mercy anaenda kuniharibia mipango yangu na Mage kwasababu mage tayari ameridhia tuanze taratibu za kutambulishana ili tuanze kuishi pamoja kama mume na mke na hapo baadae tufunge ndoa. Hii kitu bado naona ni mapema kwasababu ndo kwanza hata mwaka hatujamaliza.


See you........
 
Back
Top Bottom