Daktari anasoma miaka 5-7 na mhandisi anasoma miaka kati ya 3-4 lakini ona tofauti ya mishahara kati yao hapa chini

Kama unataka daktari aongezewe mshahara basi uwapiganie waongezewe mshahara ila usi jaribu kutaka ku down grade Engineers maana hata wao kazi yao ngumu sana usichukulie poa asee.. engineers na daktari kazi zao wote ni life or death .. Engineer wasipokua na solutions sahihi kwenye project zao they can get people killed . Usichukulie poa
 
Ha ha haa, yaani imekuwa kama ile tuliyonayo Watanzania wengi kufurahia aliye na maslahi makubwa anaposhushwa ama tuwe nae sawa au hata tumzidi, ndio sababu ya watu kuanza kupimanisha kazi kwamba hii ni ngumu na nyingine si ngumu; mwisho wa siku ni ubinafsi, kila mwenye fani atatetea fani yake ionekane ngumu na bora kumzidi mwenzake. Ukipambania maslahi ya kazi yako, pambana bila kuomba maslahi ya mwenzako yashuke au kuiona fani ya mwanzako ni ya chini, kwa kitendo tu cha kufundishwa darasani na vyuoni, maana yake ni ya muhimu na ina ugumu wake. Kazi rahisi au nyepesi ni ile isiyohitaji utaalamu wowote
 
Bila kujali ni daktar, ni mhandisi au ni mwalimu... anacholipwa mfanyakazi wa Tanzania kina sifa ya kuitwa mshahara?...kina mwezesha kuishi?...
 
Wala sisemi serikali iwapunguzie mie nataka serikali ione tu jinsi ambavyo haifanyi fair
 
Bila kujali ni daktar, ni mhandisi au ni mwalimu... anacholipwa mfanyakazi wa Tanzania kina sifa ya kuitwa mshahara?...kina mwezesha kuishi?...
Wengine zinawatosha ila kada ya afya na ualimu haziwatoshi
 
Tunasafari ndefu sana, kijana unasoma unawaza kuajiriwa nadhani utapata tabu sana.
 
Dogo inaonyesha bado upo shule..
Hzo stethoscope na thermometer zinatengenezwa na nani?.
Hizo amplicox zinazalishwa kwa fermentation, najua hayo huyajui unafikiri who run those fermenters?.
Halafu unasema upo kituo cha afya then et unalipwa 950k, serikali gani hiyo inalipa maco kiasi hicho?.
 
Miaka inavyokwenda na ugunduzi wa kisayansi madaktari watakosa kazi soon. Roboti linakutibu unasepa.

Tuitie roboti lijenge lami.
Kwenye utabibu... Bado aisee kwa sababu dalili za magonjwa zinachanganya... Mda mwingine zinafanana.... Magonjwa mengine yanapatikana kwa baadhi ya maeneo duniani..... Ugonjwa mwingine hubadili dalili kadri muda unavo zidi kwenda..... Itakuwa ngumu kutengeneza software itakayoweza kujua fika ni aina gani ya uginjwa au magonjwa yanayomsubua mtu fulani.....
 

Hapo kwenye red nimegundua sasa wewe ni half cooked idiot

Na nyie ndio aina ya madaktari tulionao huku..Akija mgonjwa mwenye shule akiwachimbisha mnapaniki kuwa mnafundishwa kazi kumbe hakuna mjualo halafu mpo hapa kudai muongezewe pesa...Kuleni laki sita hiyo
 
Hufaham kitu kuhusu taaluma ya udaktari.

Kwa hiyo operation za moyo, mgongo, kichwa n.k huwa anakuja kuzifanya engineer
Mkuu utamlaumu jamaa bure; mwili wa binadamu ni kitu ambacho haibadiliki badiliki. Inayo mfumo na principle inayofahamika kwamba ukitaka kufanya upasuaji wa moyo unatkiwa kuanza na hiki na hiki; ukitaka kufanya upasuaji wa kichwa unatakiwa uanze na hiki na hiki tofauti na hapo utakua siyo mtaalam.

Sasa turudi kwenye fani ya uhandisi wao wanashughulika na vitu ambavyo havina sheria maalum au principle timizi. Leo daktari atamwambia tunapata shida na madhara yatokanayo na kuchoma watu sindano tunapochukua vipimo hivyo tunaitaji vifaa ambavyo tutatumia kuchukua vipimo vya damu bila kuchoma mtu.sindano hapo ndo akili inaanza kutumika kuipata vipimo.

Kuna jengo lipo Pale kariakoo chini first floor imearibika ila floor za juu ni nzima hivyo afanye maarifa ili ya chini irekebishwe bila zingine kuleta madhara ujue hapo haina sheria maalum.
Kwenye tiba tunajiushisha na dalili.; hivyo miongoni mwa dalili hizi kuna kitu kati ya hizi mgonjwa atakua nazo.

Kuna matumizi makubwa sana ya akili kwa wahandisi zaidi ya koda zote; na wataalam walishaipigia kura mara nyingi sana.
 
Mimi siyo Mhandisi lakini hawa watu ndo najua wanatumia akili na stress juu; ebu fikiria hizi ndege zinazoua watu kila mara hapa karibuni wahandisi wako katika haki gani? avumbue kifaa, aiendeshe, airekebishe, afanye utfiti kwa kuiboresha zaidi, aangalie gharama yake na ubora wake, agundue nzuri zaidi ya hiyo ya kwanza, awasiliane na kada zote kujua challange wanazozipata wanapotumia hizo mitambo na azifanyie kazi kwa haraka. Machine hizo za madaktari zimearibika azirekebishe kwa haraka na muda muafaka.
 
Hao ni Maeng wa Mbelee.. Eng wa bongo michosho tu!
 
Ininia huyo huyo anamaliza na yeye anarud mtahan hana kaz
 
Utajir ni nyota tu ya mtu. Unaweza ukasoma huo uinjinia na bado ukawa na maisha ya kawaida tu
 
Hata bajaji hawezi Iunda akipewa...[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
bado ni mawazo yao ila wanaojua kazi wengine wengine wamefanya wanawapa heshima zao;
 
Kipi kinafanya, Taasisi kuwa na Mishahara Mikubwa?
Kunatofauti Kati ya
Mamlaka na Taasisi?
naposema taasisi namaanisha authority,agency,company,corporation na zinazofanana nazo hizi salary scale huamuliwa na board yake hususani ile wakati wa kuanza kazi kwa mfano afisa biashara wa TRA at first anaweza anza na 1.5M wakati wewe wa jiji ukaanza na 900K
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…