Daktari anasoma miaka 5-7 na mhandisi anasoma miaka kati ya 3-4 lakini ona tofauti ya mishahara kati yao hapa chini

Wameboreshewa mkuu 950,000 c.o.
Kama ukimlipa clinical officer laki sita clinical assistant utamlipa shingapi?!
 
We jamaa unaropoka.
Hivi unajua kama madaktari hususan wa upasuaji wanacheza na maisha ya mtu.?!
We kumzalisha mtu kwa upasuaji au kumfanyia mtu upasuaji wa moyo sio kitu rahisi.
Embu kaka tumia akili hakuna mwenye kaz ngumu kama daktari ukimtoa mwanajeshi
Kawaida Mhandisi anatumia akili kubwa kwenye kazi kuliko Daktari.

Daktari anakuuliza dalili za tatizo na kujua ugonjwa lakini Mhandisi anatumia akili nyingi kuvumbua tatizo
 
Angalia muda wanaokaa darasani na kumbuka hizo ni gloss salary take home hapo ni 800,000 yaani hiyo ndio ya kuitafuta kwa miaka 5 university?
Chukua mfano ambapo mwajiri ni mmoja na wote wameajiriwa fresh from the college. Mfano wako si sahihi.
 
Kuna tofauti Kati ya mwalimu na muhadhiri, mkufunzi? Nadhani tofauti itakuja kuwepo mbeleni siku tukianza kupanga wanaotakiwa kusomea ualimu Ni wale tu waliofaulu kwa viwango vilivyotukuka. Kwa Sasa Ni Kama ualimu Ni kichaka Cha.......japo sio wote.
 
Hoja yangu uliielewa lakini? Wengi sio specialist ni hao MD na CO,Kama CO anafanya kazi kubwa hivyo na anazidiwa na Technician was civil huoni kuna haja ya kuwaangalia upya?
Hao ma specialist ndugu ni sawa na kulinganisha senior engineer au wakuu wa vitengo vya uhandisi
Nakupa mfano mkuu wa kitengo cha maabara ya ujenzi anasikika posho za site kuliko mtu yoyote wa civil maana anadeal na quality control ya structures na civil works kila hatua ya mradi hapo sijazungumzia makampuni wanayowapa kazi lazima waache pesa
Kwa ma engineers sio rahisi kununua vitu vya thamani kwa vile wanafuatiliwa maana industry yao inahusisha 60% ya mapato ya serikali ko huwa wanatumia watu wa pembeni ila ni matajili usipime kama watu wa TRA
 
Kaka daktari ana shughuli nzitoo.
Kupasua moyo wa mtu si kitu rahisi kakaaa.
We acha masihara ndio maana wengine mpk wanaua sio km wanapenda
Na unapomfanyia mtu upasuaji unaenda kwa mahesabu kuna mishipa ukiigusa umeua na ni midogo ajabu.
We acha masihara doctor ana shughuli nzito aisee
Wewe unafaham kitu kuhusu Uhandisi?
Unafahama chochote kuhusu Structural Analysis?
 
Malalamiko ambayo huwa nayaona ni reasonable ni yale ya walimu tu. Acha roho ya wivu na ubinafsi mkuu.
 
Chukua mfano ambapo mwajiri ni mmoja na wote wameajiriwa fresh from the college. Mfano wako si sahihi.
Viwango nilivyotaja ni vya first employment,technician II na engineer II na kwa madaktari ni hivyo hivyo
 
Hivi unajua kama Engineer hususani wa majengo anacheza na maisha ya watu?? Vipi hilo jengo unalofanyia kazi lingekuwa chini ya kiwango mpaka sasa ungekuwa umesalimika??

Acheni kujiona wa special sana nyie Kila taaluma ina faida zake kwa nafasi yake na sote tunaishi kwa kutegemeana kila mmoja.
 
Kuleta dharau kwa Engineer ni kujitoa ufaham wa makusudi. Engineer ni mtu wa Applied Science,vitu vingi ni mkono wa Mhandisi. Hapa hatuzungumzii Mhandisi wa Ujenzi au Umeme au Mitambo bali kila unachogusa,ujue Mhandisi yupo. Vifaa vyote vya Hospital basi jua kuna Mhandisi wa Chemical,Umeme,Computer,Material,Mechanical nk. Hizo apparatus,kama hakuna Mhandisi,daktari atang'aa sharubu tu.
Tuchukue mfano wa Sindano.
Kuna Material Engineer kahusika kutengeneza ile plastic ya Sindano na ile needle,kuna Chemical Engineer na Assurance Eng,bila umeme mashine ya kuzalisha mabomba ya sindano isingefanya kazi,lakini mashine inakua na Mechanical Engineer nk. Kwa Scenario hizo,huwez kumdharau Eng hata kidogo. Na hapa Engineer anaezungumziwa ni Wa "Speciality "Yoyote!
 
Unazijua kazi ngumu na nzito wewe?
 
Umeshawahi kufikiria kuwa huyo engineer akiumwa au akiumia nani anamtibu mkuu?

Daktari anahakikisha kwanza afya ya engineer huyo.
 
Sawa mkuu kwa mm namtoa MD nataka c.o ndio ashughulikiwe maana MD wanakula bata nao vile vile.
Ila nimekuelewa mkuu.
MD akishapata mishahara ya hospital mbili akiikutanisha kaka kasha win hapo wa kuangaliwa C.o maana wanamtumikisha 24 hours mshahara mbuzi.
Kwa mimi navyoona mkuu labda kama nimetereza nielimishe. Maana ukutanishe million 1.5 ya Mnazi mmoja na ya Hindumandal million 3 tayar mkuu huoni kuwin tayar hapo?!
Kama fikra zangu duni mkuu nipambanulie zaidi
 
Nataka nichangie kidogo.
Unafaham malipo ya Resident Eng kwenye mradi au Project Manager?
Hivi unafaham mradi mkubwa kama wa Daraja la Mkapa, Project Manager anaweza kulipwa hadi Million 40 kwa Mwezi? Na hiyo sifa ni ya Consulting Engineer.
 
Wameboreshewa mkuu 950,000 c.o.
Kama ukimlipa clinical officer laki sita clinical assistant utamlipa shingapi?!
Nnachokiongea nna uhakika nacho mkuu,sijakurupuka.

Clinical Officer II anaanza na TGHS B ambayo ni 680,000/=
Clinical Assistant II anaanza na TGHS A ambayo inacheza kwenye 450,000/=
Assistant Medical Officer (AMO) ipo kwenye TGHS C ndiyo hyo 980,000/=
 
Siku hizi ni mara chache MD anakuwa na vijiwe vingi kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya MD’s mtaani.! Ila MMed ndo haswa wanakuwa na vijiwe hususani kwenye hizo hospitali kubwa.
 
Nnachokiongea nna uhakika nacho mkuu,sijakurupa.

Clinical Officer II anaanza na TGHS B ambayo ni 680,000/=
Clinical Assistant II anaanza na TGHS A ambayo inacheza kwenye 450,000/=
Assistant Medical Officer (AMO) ipo kwenye TGHS C ndiyo hyo 980,000/=
Mkuu kwa kumbukumbu zangu TGHS A ni 432000/=
 
Asee umeenda mbaali.
Tumia akili ya kawaida kusimamisha jengo lisimame ni pahala padogo sana mtu hukosea.
Ila sio kupasua kichwa cha mtu au kurudishia mfupa kama ulivyo mwanzo Asee kaka.
We mtu analetwa hospital ama dispensary yule ktk critical condition ukimchelewesha kaenda na maji.
Hususan sisi ma c.o wa zaman tumeteseka sana nashukuru.Mungu nimekua c.o within 1 year basi.
Engineer akijenga jengo chin ya kiwango ni ujinga wake na anafaa alaumiwe kwasababu cement zenye ubora zipo na nondo zenye ubora zipo.
Ila sio kucheza na mishipa midunchu mkuu.
We mtu anakuletea ndugu yake mwenye abnormal ECG.
mapigo ya moyo yameshuuka anakulalamikia umshughulikie yarudi sawa ndugu sio kazi rahisi kam kuchanganya zege
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…