Daktari anasoma miaka 5-7 na mhandisi anasoma miaka kati ya 3-4 lakini ona tofauti ya mishahara kati yao hapa chini

Daktari anasoma miaka 5-7 na mhandisi anasoma miaka kati ya 3-4 lakini ona tofauti ya mishahara kati yao hapa chini

Udaktari tiba ni fani nyeti na ngumu sana lakini cha kushangaza daktari anapata salary ya tsh.1,500,000 gloss huku mhandisi wa civil pale Tanroads(case study) anapata 2,000,000
Clinical officer/tabibu =950,000 huku Civil Technician=1,118,000 per month
Kwa staili hii case za rushwa zitaisha huko hospitali na vituo vya afya? Tafadhali serikali wapeni madaktari uzito unaostahili kwenye malipo,wanatumia kusoma na wanaumia kazini.
Hata kwenye stahiki za posho na benefits zingine daktari hamfikii mhandisi lakini pia mhandisi hasa wa civil wako kwenye industry ambayo possibility ya yeye kupata pesa ni kubwa kuliko watu wa afya hadi semina zije.
Chonde chonde serikali mnapopanga viwango mliangalie hili na ule mpango wa kuwianisha malipo ya wafanyakazi walio na elimu moja limeishia wapi?
Mkuu umechanganya hapo,Tanroads ni Kama shirika la umma ama taasisi mishahara ipo tofauti na halmashauri ama serikali kuu,ulichofanya wewe umelinganisha daktari wa halmashauri na mwandisi wa taasisi.
Sasa nakupa home work linganisha daktari wa TFDA,NHIF,TANAPA na BOT na mwandisi anayefanyia huko.

Tena linganisha daktari wa halmashauri na hospitali au wilaya na mwandisi wa halmashauri au wilaya.
 
kama hakutoshi njoo tulinde geti la kanjibahi hapa Upanga mwisho wa mwezi napokea Tsh 120,000/ na tukufundishe kunywa maji ya kandoro unayosemaga yanaumiza matumbo na tunalala kwenye mabox wakati huo kanjibahi anatengeneza watoto
 
tatizo dr anaajiliwa na wizara na sio taasisi kama ilivyo kwa mhandisi wa TANROAD, laiti kungekuwa na shirika au taasisi inayojiendesha yenyewe upande wa afya wangekula ndefu sana. mishahara mikubwa katika mashirika makampuni na taasisi za serikali lakini serikali kuu nothing. mfano nenda shirika la Elimu Kibaha pale ml wa degree anaanza na 1M lakini wa wizara 700k even madaktari pale ni juu. yote ni kwa sababu hizi taasisi zinatoa salary inayopamgwa na board
 
kama hakutoshi njoo tulinde geti la kanjibahi hapa Upanga mwisho wa mwezi napokea Tsh 120,000/ na tukufundishe kunywa maji ya kandoro unayosemaga yanaumiza matumbo na tunalala kwenye mabox wakati huo kanjibahi anatengeneza watoto
Wote tukiwa maskini tutatokaje mkuu
 
Hoja yako ulipoianza nimeipenda, ni kweli kumlipa Civil Engineer zaidi ya Daktari wa binadamu haiingii akilini. Labda aliyepanga ngazi za mishahara alikuwa Civil Engineer. Majukumu na uwajibikaji wao ni mbalimbàli lakini risk pia ni kubwa kwa Dokta kuliko Injinia. Hili ni tatizo lililoanzishwa na ukurupukaji na sasa waneshindwa kulitafutia dawa hata walipounda tume ya mishahara ambayo nayo imeshindwa kurekebisha tatizo zaidi ya kelele za "Tumefikia hatua nzuri".
Hata hivyo udhaifu huo hauwezi kuhalalisha uonezi wanaofanyiwa walimu. Ifike mahali tujue chanzo cha maarifa yote ni Mwalimu. Hata hiyo miaka 5 ya Daktari hawi peke yake, anakuwa na Mwalimu kwa muda huo wote. Daktari ni mwanafunzi kwa miaka 5-7 kama ulivyosema, lakini Mwalimu ni mwanafunzi muda wote wa maisha yake. Kazi yake ni kutotoa Madaktari, Mainjinia, Wachumi, na kuabort mbumbumbu ambao wengine wanageuka kupanga mshahara wake wakitokea kwenye siasa ambako ni Kokoro la waliomo na wasiokuwamo.
Mwalimu ni Kila kitu ingawaje anaonekana si kitu.
Acha kutetea tetea pasipo logic, huwezi kumlinganisha mtu anaeokoa maisha ya watu na Mwalimu anaefundisha kutoka kwenye kitabu Kazi Ya Mwalimu ni nyepesi mno Na isingekuwa nyepesi watu hawangekuwa wanaenda kurundikana huko, wewe huoni wavivu wooote wa darasani hukimbilia ualimu? Mtu anaenda kupasua kichwa cha mtu amtoe uvimbe Halafu amshone than unamlinganisha Mwalimu kweli? Acha kulinganisha udaktari na ualimu Kwanzaa inatakiwa Mwalimu apate asilimia 20 ya mshahara wa daktari
 
Mkuu umechanganya hapo,Tanroads ni Kama shirika la umma ama taasisi mishahara ipo tofauti na halmashauri ama serikali kuu,ulichofanya wewe umelinganisha daktari wa halmashauri na mwandisi wa taasisi.
Sasa nakupa home work linganisha daktari wa TFDA,NHIF,TANAPA na BOT na mwandisi anayefanyia huko.

Tena linganisha daktari wa halmashauri na hospitali au wilaya na mwandisi wa halmashauri au wilaya.
Achana na hao wa taasisi nazungumzia watu wa serikali kuu,Tanroads hapo ni case study tu lakini wahandisi wanaolipwa kidogo ni wa halmashauri lakini wa serikali kuu ukiacha hao wa Tanroads na Tarura wako vizuri sana kuliko madaktari
 
Mshahara wa daktari na mhandisi unatakiwa kuwa Mara tano ya mshahara wa walimu, kwani hamjui kuwa huko nyuma waliokuwa wanaenda ualimu ni wale waliofeli? Leo mnajifanya kusahau eeh mnataka walipwe Kama mhandisi acha kujitoa ufaham fani ya ualimu ni nyepesi mno Na haina risk yoyote, kila magonjwa yakijitokeza mnawapeleka madkari huko huko Leo mnataka walipwe Kama walimu khaaaa
 
Tarura ni kama Rea....... Ambapo kwa kada ya afya nazungumzia TACAIDS nenda kaulize mshahara wa clinical officer,Kisha njoo tena
Achana na hao wa taasisi nazungumzia watu wa serikali kuu,Tanroads hapo ni case study tu lakini wahandisi wanaolipwa kidogo ni wa halmashauri lakini wa serikali kuu ukiacha hao wa Tanroads na Tarura wako vizuri sana kuliko madaktari
 
Tarura ni kama Rea....... Ambapo kwa kada ya afya nazungumzia TACAIDS nenda kaulize mshahara wa clinical officer,Kisha njoo tena
Sasa hao wa mataasisi ni wachache kuliko majority wenye pesa kiduchu ambao ndio hoja yangu
 
Kawaida Mhandisi anatumia akili kubwa kwenye kazi kuliko Daktari.

Daktari anakuuliza dalili za tatizo na kujua ugonjwa lakini Mhandisi anatumia akili nyingi kuvumbua tatizo
Hii imekaa kwa kukariri kidogo.
Sidhani kama unazijua vizuri kazi za hao wataalamu.

Engineer wa bongo anafanya uvumbuzi?
Daktari MD anatumia akili sana kukuandikia vipimo sahihi baada ya kukusikiliza na kukuona kwa macho.

Ujue dalili za magonjwa mengi zinafanana sana kiasi kwamba dokta hasipotumia akili kubwa anaweza asikuandike vipimo sahihi na mwisho unakosa tiba sahihi ya tatizo lako na kusababisha ukumbwe na mauti au ulemavu.

Ukimzungumzia daktri unazungumzia kati ya kifo na kuishi(maisha).

Nawaheshimu wote wanatumia akili kubwa sana hongera zao. I wish I could be one of them. I mean either a doctor or an engineer.
 
Udaktari tiba ni fani nyeti na ngumu sana lakini cha kushangaza daktari anapata salary ya Tsh.1,500,000 gloss hukuhandisi wa Civil pale TANROADS(case study) anapata 2,000,000
Clinical officer/tabibu =950,000 huku Civil Technician=1,118,000 per month

Kwa staili hii case za rushwa zitaisha huko hospitali na vituo vya afya?

Tafadhali serikali wapeni madaktari uzito unaostahili kwenye malipo,wanatumia kusoma na wanaumia kazini.

Hata kwenye stahiki za posho na benefits zingine daktari hamfikii mhandisi lakini pia mhandisi hasa wa civil wako kwenye industry ambayo possibility ya yeye kupata pesa ni kubwa kuliko watu wa afya hadi semina zije.

Chonde chonde serikali mnapopanga viwango mliangalie hili na ule mpango wa kuwianisha malipo ya wafanyakazi walio na elimu moja limeishia wapi?
Sasa unataka alipwe laki 2,mbona mbunge msukuma anapata zaidi ya milioni 8 kwa mwezi ulalamiki?acha wivu alafu sio taasisis zote mhandisi analipwa hivyo
 
Walimu kwa sasa wanalipwa vizuri kuliko awali,na ukiangalia ugumu na risks za kazi ualimu sio mgumu wala sio risk Kama daktari
Hapa ndo umeharibu kila kitu... kulipwa vizuri ndo kiwango gani!!

Risks zipi unazomaanisha?

Kila kazi ina umuhimu wake ila ualimu ni proffession inayoweza ibadili jamii kifikra na kuleta mageuzi katika nyanja zote ama kuleta taifa lisilokuwa na uelekeo.

Kwa wenye fikra fupi na kutegemea matokeo ya papo kwa papo hawawezi tambua hili.

Kwa zama hizi ambazo kila kitu lazima ugharamike maswala ya wito hayapo tena.

Waalimu kwa nyanja zote wapewe heshima na motisha kwa kazi hii..
 
Mlinganisho wako sio sahihi kwa upande mmoja.

Umeongelea TANROADS ambayo ni Taasisi, zungumzia mshahara wa daktari katika Taasisi kama vile MUHIMBILI ndio utapata usawa.

Je,unafahamu mshahara wa Civil katika ngazi ya serikali ya mtaa ni kiasi gani na MD nae ni kiasi gani?!

Halafu kwenye Case ya CO umepotosha kidogo kwa kumzidishia kiasi fulani, yeye anapata 680,000 kwa mwezi na sio 980,000/.

Nawasilisha..!
Mimi nimetaja co anapata 950,000 sijataja ulichoandika wewe sasa kama anapata 680,000 AMO anapata ngapi? Nesi je
 
Back
Top Bottom