Hoja yako ulipoianza nimeipenda, ni kweli kumlipa Civil Engineer zaidi ya Daktari wa binadamu haiingii akilini. Labda aliyepanga ngazi za mishahara alikuwa Civil Engineer. Majukumu na uwajibikaji wao ni mbalimbàli lakini risk pia ni kubwa kwa Dokta kuliko Injinia. Hili ni tatizo lililoanzishwa na ukurupukaji na sasa waneshindwa kulitafutia dawa hata walipounda tume ya mishahara ambayo nayo imeshindwa kurekebisha tatizo zaidi ya kelele za "Tumefikia hatua nzuri".
Hata hivyo udhaifu huo hauwezi kuhalalisha uonezi wanaofanyiwa walimu. Ifike mahali tujue chanzo cha maarifa yote ni Mwalimu. Hata hiyo miaka 5 ya Daktari hawi peke yake, anakuwa na Mwalimu kwa muda huo wote. Daktari ni mwanafunzi kwa miaka 5-7 kama ulivyosema, lakini Mwalimu ni mwanafunzi muda wote wa maisha yake. Kazi yake ni kutotoa Madaktari, Mainjinia, Wachumi, na kuabort mbumbumbu ambao wengine wanageuka kupanga mshahara wake wakitokea kwenye siasa ambako ni Kokoro la waliomo na wasiokuwamo.
Mwalimu ni Kila kitu ingawaje anaonekana si kitu.