Anaitwa Saidi Abdallah Mikidadi Potea, miaka 33, mkazi wa Kijichi, Temeke mkoani Dar es Salaam.
Saidi amejikuta akipambana kwa kila njia kuunusuru uhai wake kufuatia gonjwa la ajabu la uvimbe shingoni huku daktari akimwambia bila Shilingi Milioni 40 za Kitanzania, hatoboi miezi mitatu ijayo.
Saidi kwa sasa ni kama amemwachia Mola wake. Maana anasema anahesabu siku kukifikia kifo chake kwa sababu daktari alisema kwa vile uvimbe wake unakua kila kukicha, ikifika Machi mwaka huu (2026) kama hatafanyiwa upasuaji, utapasuka na yeye kupoteza maisha!
Anasema: "Naumia sana moyoni. Kwa sababu familia imepambana sana hadi kufikia hatua ya kukata tamaa. Wapi sijapelekwa mimi? Hospitali, kwa waganga, makanisani, kwa mashehe. Lakini wapi!
Anaendelea kusema: "Mwisho kabisa Muhimbili wameniandikia kwenda Hospitali ya Apollo iliyopo nchini India. Lakini gharama ni Shilingi Milioni 40."
Saidi anasema kwa sababu familia yake ambao ni nduguze watatu (baba na mama walishakufa), hivyo, anapiga magoti kuwaomba Watanzania wenzake watakaoguswa na tatizo lake kumchangia ili aweze kwenda kufanyiwa upasuaji huo nchini India.
MKASA KAMILI, TATIZO LILIPOANZA
Akisimulia kwa masikitiko makubwa na katika hali ya kukata tamaa kuhusu chanzo cha uvimbe huo wa ajabu, mdogo wa Saidi aitwaye Jundani Mikidadi Potea, alianza kwa kusema:
"Kusema ule ukweli kaka yangu Saidi anapitia mateso makubwa sana. Kaka anapitia mtihani mzito. Lakini pamoja na yote haya hatuachi kumwomba Mungu atusaidie, aturehemu na huu ugonjwa wa kaka yangu."
Jondani anasema: "Ilikuwa mwezi wa saba mwaka jana (2025). Uvimbe huo ulianza kwenye shingo ya kaka upande wa kulia.
"Baadaye tukagundua uvimbe unakua kila kukicha. Yaani unazidi kuvimba na kumsababishia maumivu makali kwa nyakati fulani. Hatua ya awali kabisa tulimpeleka Hospitali ya Amana, vipimo vikaonesha hana tatizo. Tukaambiwa twende Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kitengo cha Magonjwa ya Ngozi.
"Kule walimchukua kinyama na kukipima Mahabara Kuu ya Taifa, majibu yakawa hawaoni tatizo. Na wala siyo kansa. Wakashauri twende Hospitali ya Robininsia Memorial (Tegeta-Namanga) ambako pia vipimo vilishindwa kubaini tatizo.
"Wakasema wanaweza kumfanyia upasuaji lakini mdomo utapinda na atapata tabu wakati wa kuongea. Hilo nalo likawa ni tatizo jingine. Yaani mdomo kupinda na kuongea kwa shida. Huo ulikuwa mwezi wa kumi mwaka jana (2025)."
KWA WAGANGA WA KIENYEJI
Jundani akaendelea kusimulia kwamba, wakati juhudi za kutafuta uponyaji zikiendelea, baadhi ya watu walimwambia lazima kuna 'mkono wa mtu' kwenye ugonjwa wa kaka yake, hivyo walimshauri aende kwa waganga wa kienyeji kuwaona 'wabaya wa mgonjwa' ni akina nani!
"Tulikwenda kwa waganga wa kienyeji mbalimbali. Mfano; tulikwenda Horohoro, Tanga (njia ya kwenda nchini Kenya). Tukaenda Dumila (Morogoro). Tukaenda Kilwa (Pwani). Tukaenda Somanga (Pwani) ambako alikaa kwa wiki mbili akiogeshwa madawa mbalimbali.
"Kote huko tuliambiwa kaka yangu alitupiwa kitu kibaya na watu wabaya. Waganga wote kwa nyakati zao tulizokwenda walimpa dawa za asili za kutumia lakini uvimbe umeendelea na unaendelea kukua." (kama unavyoonekana pichani).
WACHUNGAJI, MASHEHE
"Ushauri haukuishia kwenda kwa waganga tu. Wengine wakatushauri twende kwa wachungaji au mashehe. Waliyotushauri hivi, kila mmoja aliamini imani yake. Tuliambiwa akiombewa na wachungaji atapona. Hata kama ana mapepo yatakimbia. Kwa mashehe tuliambiwa atasomewa kisomo, kama ana kitu kibaya mwilini kitaondoka. Kwa hiyo atapona.
"Tulianza kwenda kwa shehe mmoja pale Ubungo. Akasomewa kisomo. Lakini wapi! Ndiyo kwanza uvimbe uliendelea kuvimba.
"Tukaenda Msasani kwenye kanisa moja la EAGT (Evangelical Assemblies of God Tanzania) lipo Msasani (Dar). Akaombewa. Lakini hakulipuka mapepo wala nini. Uvimbe umeendelea kukua."
DAKTARI TOKA INDIA AWASILI DAR, AONANA NA SAIDI
Jundani anaendelea kusema kuwa, siku moja alipigiwa simu na Dokta wao wa Muhimbili ambako pia walikwenda baada ya kutoka Amana (hospitali) na kabla ya kwenda Robininsia (hospitali).
"Akasema kuna daktari anaitwa Prased Namani amekuja Dar kutoka Hospitali ya Apollo, iliyopo mji wa Hyderabad nchini India, wamemweleza kuhusu tatizo la kaka, akataka tumpeleke akamwone. Kama akimwona anaweza kupelekwa India kwa upasuaji, itabidi Muhimbili wamwandikie rufaa ya kwenda. Kama hataweza, itakuwa basi.
"Basi, tulikwenda Muhimbili. Tulikutana na Dokta Prased. Alimchunguza kwa undani kaka Saidi. Mwishowe akasema aandikiwe barua ya kwenda India. Kule atafanyiwa upasuaji na daktari mpasuaji wa vichwa na shingo (head & neck surgeon). Anaitwa Arsheed Hakeem.
"Mshtuko mkubwa ulikuja baada ya Dokta Prased kusema kuwa, endapo upasuaji huo hautafanyika hadi kufika miezi mitatu ijayo, yaani hadi mwezi wa tatu (mwaka huu 2026), basi uvimbe utapasuka na mgonjwa atapoteza maisha. Hii inatuuma sana sisi familia na mhusika mwenyewe.
"Hivyo, haraka sana ikabidi Muhimbili watuandilie taratibu za kwenda India ikiwa ni pamoja na gharama za matibabu na nauli ya mgonjwa peke yake kwenda India. Ni shilingi milioni 40. Hapo ni bila msindikizaji. Lakini wakasema kwa sababu mgonjwa anatembea na kuongea mwenyewe, anaweza kupelekwa na mtu akishamkabidhi kule Hospitali ya Apollo, anarudi Tanzania.
"Sisi kwa kuzaliwa tuko watoto wanne. Wa kike wawili. Baba na mama walishafariki dunia. Katika hao wawili, mmoja alifiwa na mume mwaka jana mwishoni. Alipata ajali ya gari. Wote hao nawahudumia mimi. Kaka Saidi ndiye mkubwa lakini kwa hali yake amekuwa tegemezi. Mtu ambaye awali alikuwa na shughuli zake za ufundi wa kompyuta na tulimtegemea yeye. Sasa hawezi tena.
"Kwa hiyo sisi tunachowaomba Watanzania wenzetu watuchangie chochote kile ambacho mtu atajaliwa na Mungu."
SAIDI NA HISTORIA YA VIMBE MWILINI!
Pamoja na simulizi hiyo ya Saidi ambayo inasikitisha, pia mgonjwa huyo ana historia ya kupata uvimbe mwilini.
Jundani anasema Saidi akiwa na miaka 7 alipata uvimbe wa ajabu kwenye mguu wake wa kushoto (angalia picha).
Anasema walimpeleka Hospitali ya Tumbi mwaka 2002 ambako alifanyiwa upasuaji lakini mguu haukuwahi kukaa sawasawa. Umepinda na umevimba upande mmoja.
"Mwaka 2009 alifanyiwa tena upasuaji Hosptali ya Taifa Muhimbili. Lakini hakuna kilichoendelea. Mbaya zaidi huu mguu kila ulipokuwa unafanyiwa upasuaji, ndipo uvimbe ulizidi hadi familia ikaamua kuuacha kama ulivyo ukiwa umepoteza mwonekano halisi.
"Mbali na uvimbe wa mguuni ambao ulimuanza akiwa na miaka saba, pia ana uvimbe juu ya kiganja cha mkono wa kulia ambao ulimuanza mwaka 2014. Alienda Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila mwezi wa 3 mwaka jana (2025). Lakini madaktari wakamwambia asipasuliwe bali akubaliane na hali yake hiyo.
"Lakini sasa, vimbe zote hizo zimekuwa zikimwachia uchungu mkubwa kaka yangu akiwa kama binadamu anayetamani kuwa kama wengine. Kwa sasa anashinda amefunga kitambaa kuzunguka shingo ili kupunguza macho ya watu wanaomwangalia kwa kumshangaa.
"Huwa ikafika wakati unamwona anavyoumia hata usoni. Kwa kweli najikuta na mimi nikiumia kama yeye. Na familia nzima inaumia kwa pamoja. Mtu ukiishi kwa kuhesabu siku inaleta unyonge mkubwa na kuhisi kama dunia imekukataa. Lakini mimi naamini dunia haijamkataa kaka yangu. Bado dunia ina watu wenye moyo wa kutoa. Bado dunia ina watu wanaomjua Mungu wa kweli," alimaliza kusema mdogo wa Saidi Mikidadi, Jundani Mikidadi.
* KUWASAIDIA WAGONJWA NI IBADA KWA MUJIBU WA VITABU VITAKATIFU.*
Kwa Mtanzania atakeyeguswa kuchangia chochote namba za kutumia ni;
Simu: 0710434416 Jundani Mikidadi Abdallah.
NMB: 20310131829 Jundani Mikidadi Abdallah.