Daladala Mwanza, Dar es salaam zaomba kusitisha huduma ya usafiri kuanzia kesho tarehe 09

Daladala Mwanza, Dar es salaam zaomba kusitisha huduma ya usafiri kuanzia kesho tarehe 09

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Saa chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra) kutangaza kuongeza muda wa wiki mbili zaidi wa kupokea maoni kuhusu mapitio ya nauli, Umoja wa Wasafirishaji Abiria Dar es Salaam na Mwanza umeomba kusitisha kutoa huduma.

Kwa mujibu wa wasafirishaji hao, sababu kuomba kusitisha huduma hizo jijini Dar es Salaam na Mwanza zimetokana na kujiendesha kihasara tangu ongezeko gharama za mafuta lililoanza Aprili Mosi, 2026 lililotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).

Kauli ya wadau hao imetolewa leo Jumatano Aprili 8, 2026 na viongozi wa umoja huo jijini Dar es Salaam wakati wakiwasilisha maoni ya taasisi hizo ya namna inavyojiendesha tangu kupanda kwa bei za mafuta katika mkutano wa wadau wa usafirishaji ulioandaliwa na Latra.

Mwenyekiti wa Umoja huo Mkoa wa Dar es Salaam (Uwadar), Jafar Kismat amesema baadhi ya mikoa kama ya Mbeya na Arusha, Kilimanjaro kuna nyakati daladala ziligoma kutoa huduma sambamba na kuongeza nauli kinyemela na hakuna hatua zilizochukuliwa hata hivyo, Uwadar haitaki kufika huko, lakini Latra iwaangilie.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji Abiria Mkoa wa Mwanza, Yusuph Lupilia amelalamikia kitendo cha usafiri wa bajaji kufanya kazi sawa na daladala katika vituo vyote jijini humo.

Lupilia ameitaka Latra kuongeza bei ya nauli ili daladala zijiendeshe akipendekeza kuanzia kilomita sifuri hadi kilomita 10 iwe Sh800 kutoka Sh 600.

Chanzo via Mwananchi
 
😲😲kituo hadi kituo ni tsh 600 dar na Mwanza!eti wanaomba ifike walau 800,KARIBU MBEYA kabla ya mafuta kupanda kituo hadi kituo ilikuwa Tsh 800 ila kwa sasa ni tsh 1000!
MBEYA LATRA HAWAHUSIKI KUPANGA NAULI,WANANCHI WANAUMIA SANA.
 
Serikali ikiwa batili halafu legelege lazima kila kitu kiende mrama
 
nimesoma title tu..

ila bei ya mafuta ikipanda automatically nauli lazima ipande.

kilichotakiwa kufanyika/point ya ku intervien
Sirikali kufanya maridhiano na wafanyabiashara wakubwa wanaoagiza mafuta na kusupply mafuta inji hii.

kama watawapunguzia kodi na tozo au watawapa ruzuku.

ili wao matajiri wa mafuta wasipandishe bei ya mafuta,na bei isipande kwenye vituo vya mafuta na gharama za maisha zisipande ikiwemo nauli.

Wrong approach
ni kuwabana hawa masikini wanyonge wamiliki wa vyombo vya usafiri..hakuna atakayekubali kuendesha daladala kwa hasara.
 
Back
Top Bottom