KERO Daladala za Buza zinakatisha ruti kila siku, zinatushusha njiani; LATRA chukueni hatua

KERO Daladala za Buza zinakatisha ruti kila siku, zinatushusha njiani; LATRA chukueni hatua

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Bani Israel

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
2,284
Reaction score
4,595
Habari wakuu natumai mko poa kabisa ndugu zangu wahishimiwa wanabodi na kadhalika.

Mimi ni yule yule wa siku zote mkazi sugu wa buza kanisani always nimekuwa nikileta kero za usafiri huku kwetu japo hazitatuliwagi ila sitoacha kutoa kero kwa niaba ya wengi natumai one day zitawafikia wahusika ambao wao wapo maofisini wala hawawazi kabisa kuhusu yanayotukumba wananchi.

Kero yangu ya leo nailelekeza moja kwa moja kwa LATRA mamlaka hii ndio inahusika na kuunda ruti na utoaji vibali vya ruti husika kero hii kuhusu buza naipeleka kwao.

kwanza kabisa latra ndio watoa vibali vya ruti na kuwaagiza wahuska wapite njia hii na kituo ni hiki na hiki na inapotokea mambo yanaenda kinyume basi abiria ndio tunaoteseka.

Kero hizi (3)ndio kuu:.
1 : Daladala kubadili safari nyakati za jioni.
2 : Daladala kufupisha safari
3 : Daladala kutomaiza safari kwenye kituo husika.

1: Daladala za kutoka Gerezani kariakoo kuja buza nyakati za jioni huwa sio za buza tena huwa (70%) huelekeza uelekeo wao Tandika sudani na yombo kilalaka (USHAHIDI UPO)

Daladala za Gerezani mbagala kupitia buza kuishia tandika sudani kama kituo kikuu baladala ya kufika mbagala

1(a) Daladala za kutoka makumbusho Kubadili safari kuelekea Tandika sudani badala ya buza.

2: Daldala kufupisha safari.

Daladala za kutoka makumbusho Kwenda buza kuishia Tandika mango (DEVIS CORNER) Hazifiki buza.

DALADALA ZISIZOFIKA BUZA KABISA NA KUISHIA TANDIKA SUDANI

Daladala kutoka mwenge via sinza hazifiki kabisa buza wana kituo chao Tandika sudani

Daladala za Muhimbili hazufiki kabisa buza wana kituo kabisa cha kumaliza safari Tandika sudani

Daladala za kwenda mbagala via buza hawa nao hawajawahi fika buza kabisaaa

Daladal za stesheni kwenda buza hazifiki kabisa buza.

3 kero ya 3 ni daladala zinazofika buza kuishia sheli ya OLIMPIC kwa mama kibonge hii ndio kero mpya kwa sasa buza haieleweki daladala zinaishia wapi kama kituo kikuu kila mmoja anajiamulia pa kumalizia safari unapanda gari inaitisha buza kanisani ila ikifika sheli ya olimpic kwa mama kibonge wanasema mwisho wa safari hii imekuwa inatutesa sana abiria.

Awali ilikuwa wakiamua kuishia sehemu basi hutafutia abiria usafiri mbadala ila tangu kutokee mkanganyiko wa kituo kipya imekuwa adhabu kwetu wanachi kushushwa shushwa ovyo sehemu zisizo rasmi.

HITIMISHO KWA LATRA tuwanawaomba watoke maofisini waje huku barabarani wakati wa jionii wajue kuwa wanazindua ruti mpya gari hazifiki vituo rasmi na wao wapo maofisini hawafuatilii wamezindua ruti mpya kama 5 za kuja buza gari zinaenda kilakala sa sudani Why??

Tunaiomba RATRA chini ya kiongozi wao Mh habibu suluo na mamlaka za jiji kutatua kero zetu kwanini daladala ziandikwe zinakuja kwetu na hazifiki unakaa kituoni daladala 15 za buza zinapita ila za kwenda buza huwani 3 hadi 4 nazo ni huwa zimejaamno Tukumbuke latra wanatoa vibali kwa idadi maalum sasa daladala zikifupisha safari na kutokuja buza inapelekea abiria kukosa usafiri.

Moderator naomba msaada wenu mtusaidie kupaza sauti kuchukua point kwenye post hii ikiwezekana zipostiwe kwenye page zenu hii kero ni ya kweli na inatutesa sana wananchi.

Pia soma ~ LATRA: Tumeanza kufunga ving'amuzi vya VTS kufuatilia Daladala zinazokatisha ruti na kuzidisha nauli
 
Mkiwa mnatoka buza kuja mjini, kituo mnapandia wapi?
inategemea na wapi wewe ulipo kuna daladala zinafika buza kanisani kuna daladala zinaishia kwa lulenge na kuna daladala zinaishia kwa mama kibonge, ingawa daladala zinatakiwa zifike hadi kanisani ila wameachiwa wajiamulie kumbuka asubuhi na mchana daldal zinakuja buza vizuri ila ikifika jioni zinaenda maeneo mengine kama sudani na kilakala na nyingine kuishia tandika devis cona.

hivyo basi idadi ya daladal zinazokuja asubuhi ni nyingi ila ikifika jioni idadi ya daladal zinazokuja buza huwa ni ndogo kupelekea kuteseka kwa usafiri.
 
Kuna kipindi g/mboto pale traffic walikuwa wanatoa mikeka kwa magari ambayo hayafiki pugu station/mnadani. Hata huko akiwepo trafiki tu, daladala zitafika mwisho.
 
Kuna kipindi g/mboto pale traffic walikuwa wanatoa mikeka kwa magari ambayo hayafiki pugu station/mnadani. Hata huko akiwepo trafiki tu, daladala zitafika mwisho.
trafiki wapo na hiyo ni kama sio kazi yao utawaona kukiwa na foleni tu usku mchana wanakupogi ila hawafanyi lolote
 
Tandika sudani ndio inahitajika iyo kamata kamata sababu daladala haziji huku zinaenda na kuishia kule
 
Nadhani itungwe sheria kali inayokataza daladala kukatiza ruti ikibainika namba za/chesisi ya gari na dereva wake wafungiwe mwaka mmoja
 
Nadhani itungwe sheria kali inayokataza daladala kukatiza ruti ikibainika namba za/chesisi ya gari na dereva wake wafungiwe mwaka mmoja
kiukweli inakera bora kukatiza wanabadili kabisa
 
Nadhani itungwe sheria kali inayokataza daladala kukatiza ruti ikibainika namba za/chesisi ya gari na dereva wake wafungiwe mwaka mmoja
Mana hilo ni tatizo sugu mijini na wahusika wamelala. Inteligensia ya serikaki katika jutatua kero ni zero. Wanasubiri kuzuia maandanano ya Gen Z
 
Back
Top Bottom