TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
Lilikuwa ni suala la muda tu na hatimaye unaweza kusema tumerudi nyuma au tumerudi kwenye maisha yetu ya kawaida au tuliyozoea.
Daladala za kutokea Mbezi mpaka Mnazi Mmoja kupitia Manzese, Magomeni, Fire hadi mnazi mmoja zimeanza kazi rasmi leo.
Hadi muda huu bado zipo chache sana, ila kwa sisi wazee kuliko kuendelea kukaa kusubiri mwendokasi masaa mawili hii ni nafuu.
Na ukiona una ubavu na unaweza kupanda basi unasogea hapo mnazi mmoja ukiwa umeshiba.
Tatizo tunaloenda kupambana nalo ni foleni kutokana na barabara kubana.
PIA SOMA
- Baada ya Serikali kushindwa ni muda sasa wa kurejesha Daladala za kusafirisha abiria Kariakoo-Kimara-Mbezi