Daladala za Mbezi kupitia Manzese, Fire hadi Mnazi Mmoja zimeanza kazi rasmi

Daladala za Mbezi kupitia Manzese, Fire hadi Mnazi Mmoja zimeanza kazi rasmi

Wanaondesha usafiri katika jiji la Dar Ni vilaza kupitiliza. Wanarudisha mabasi bila kua na vituo.
Foleni zisizo za muhimu zinarudi Tena.
Hivi hapo jiji wanaona shida gani kuajiri watu wenye akili?
Wabunge wapo, wakuu wa wilaya wapo, mkuu wa mkoa yupo lkn wanashindwa kukaa na kuja na kitu chenye kuleta unafuu kwa maisha yetu.
Baada ya kukosa ubunifu wanawaandama dada utamu.
 
Wanaondesha usafiri katika jiji la Dar Ni vilaza kupitiliza. Wanarudisha mabasi bila kua na vituo.
Foleni zisizo za muhimu zinarudi Tena.
Hivi hapo jiji wanaona shida gani kuajiri watu wenye akili?
Wabunge wapo, wakuu wa wilaya wapo, mkuu wa mkoa yupo lkn wanashindwa kukaa na kuja na kitu chenye kuleta unafuu kwa maisha yetu.
Baada ya kukosa ubunifu wanawaandama dada utamu.
Hivi kulikuwa na ulazima wa kujenga vituo vya mwendokasi ambavyo vinakubali magari ya aina fulani tu?
 
Kundi dogo la watu wachache sana linaiangamiza nchi. Mimi sijui huwa wanachoweza ni kitu gani, probably flying to other countries na kufanya matamasha.

Huyu aliyeshika usikani was good kwa kukata utepe tu, haya mengine mnamuonea tu "they" can't do no shit!!
 

Lilikuwa ni suala la muda tu na hatimaye unaweza kusema tumerudi nyuma au tumerudi kwenye maisha yetu ya kawaida au tuliyozoea.

Daladala za kutokea Mbezi mpaka Mnazi Mmoja kupitia Manzese, Magomeni, Fire hadi mnazi mmoja zimeanza kazi rasmi leo.

Hadi muda huu bado zipo chache sana, ila kwa sisi wazee kuliko kuendelea kukaa kusubiri mwendokasi masaa mawili ni nafuu.

Na ukiona una ubavu na unaweza kupanda basi unasogea hapo mnazi ukiwa umeshiba.

Tatizo tinaloenda kupambana nalo ni foleni kutokana na barabara kubana.

PIA SOMA
- Baada ya Serikali kushindwa ni muda sasa wa kurejesha Daladala za kusafirisha abiria Kariakoo-Kimara-Mbezi
Bado kwa mtu mwenye akili atatumia mwendokasi. Maana hiyo daladala kwa muda itakayokaa foleni na kupiga debe, utatumia masaa hadi mawili. Ni bora usubiri tu mwendokasi.
 
Miaka mitatu ya rais mwana mama tumepata yafuatayo.1mwendokasi imekufa rasmi.

2.Shirika la ndege liko taabani.

3.Sgr imesimama.pesa hamna

4.vivuko vya kigamboni vimekufa na

5.kuongezeka Kwa watumishi wazembe,Wala rushwa,wasiozingatia miiko ya kazi na wawekezaji matapeli.
Acha kufichaficha, sema mwana mama Muislam
 
Jiwe aliwahi kutamka kuwa mtamkumbuka kwa mazuri yake. Karma ndiyo imeanza kujibu nini!?

Wazee wa Pwani wameshika mpini. Wao na familia zao wanajitengenezea fursa wao wenyewe na jamaa zao wa karibu. Kibaya zaidi itakuwa ngumu kumpata mrithi wa kiti cha utukufu nje ya wigo wao.

Uzalendo kwao maana yake kuwa chawa kwa kumaanisha kwa upande wao. Aione kwenye jalada Lucas Mwashambwa.
Mkuu, kuna jamaa mmoja si wa bara hili jeusi ni wa huko mbali huko.

Huyo jamaa baada ya stori mbili tatu akaniambia "... nyie waafrika mpo hapa duniani na matatizo ni sehemu ya maisha yenu, haitakiwi kumaliza shida miongoni mwenu na serikali zenu hazipaswi kumaliza shida zenu".

Aliendelea... " Serikali ikimaliza shida zenu bado mtaisumbua na kulalamika..."

Kwenye hili la daladala tayari wanatengeneza tatizo ili baadaye waje walitatue kwa njia ya kujibinafsishia miradi hiyo.
 
Bomu lingine ni hii njia nane ya Kimara, Stop Over hadi Kibaha

Ile barabara ya kati ilisemwa ya mwendokasi ila cha ajabu haina vituo

Mpaka leo haina matumizi yoyote mwendokasi za Mbezi na Kibaha zinatumia vituo vilevile vya daladala

Kuishi Tanzania ni laana
 
Back
Top Bottom