KERO Daladala za Mwanza zinatabia ya kukatika route, tunaomba mamlaka zifuatilie kero hii

KERO Daladala za Mwanza zinatabia ya kukatika route, tunaomba mamlaka zifuatilie kero hii

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Imekuwa ni tabia ya muda mrefu kwa baadhi ya daladala jijini Mwanza kufupisha route nyakati za usiku, hali inayowaacha abiria kwenye maeneo ambayo siyo vituo vyao vya mwisho.

Kwa mfano, jana nilipanda daladala kutoka Kiloleli, ambapo konda alieleza kuwa gari hilo linaishia Kona ya Bwiru. Hata hivyo, tulipofika Kona ya Bwiru na abiria wote kushushwa, dereva na konda waliendelea na safari kuelekea Buhongwa.

Mamlaka husika zinaombwa kulifuatilia suala hili na kuchukua hatua stahiki ili kulinda abiria dhidi ya usumbufu na changamoto za usafiri, hususan nyakati za usiku.

Haki ya abiria kuhudumiwa kwa mujibu wa route iliyotangazwa izingatiwe.
 
Back
Top Bottom