Dalili gani zinakujulisha kuwa umri umesogea?

Nilienda kucheza Moira jumamos/jumapili mazoezi nashangaa watu wanamuita mzee nipasie huku,mshua kwangu,dingo niwekee halafu nikiwaangalia nawaona ni wakubwa

Nimeshtuka nishaanza kuwa muhenga pro max
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Eti mzee nipasie huku

Mshua kwangu!
 
Kuna mama niliongea nae, aliniambia ukikutana na traffic ukawaona ni vijana wadogo au daktari hospitali ukamuona ni kama mjukuu wako. Hapo hakuna ubishi wa chumvi uliyoila duniani.
Na vipi kuhusu kichwa kujaa mvi na kuanza kupoteza kumbu kumbu?!
 
Hizi ni dalili za umri kwisha, sio kusogea.
 
Mie kuna siku mwendokasi inaanza nikapanda kuona likoje. Nimeingia nimekosa siti kuna mtu mzima akanipisha akaniambia kaa mzee. Nilijitathmini njia nzima na ndio ilikuwa mwisho wa kupanda mwendokasi
Daah nimecheka sana,
Naona mzee ulisononeka mnoo, ukaanza kukumbuka ujana wako ulivyoutumia leo hii unapishwa siti na kuitwa Mzee!
Kweli dunia njia.
 
Nilienda kucheza Moira jumamos/jumapili mazoezi nashangaa watu wanamuita mzee nipasie huku,mshua kwangu,dingo niwekee halafu nikiwaangalia nawaona ni wakubwa

Nimeshtuka nishaanza kuwa muhenga pro max
Mbavu zangu jamaniiii [emoji23][emoji23][emoji23]
Mshua nipasie hukuuuuu
 
Kuanza kuchanganya thamani za hela, mfano 5000 unatamka mia tano, elfu kumi unaiita elfu moja, mia tano yenyewe unaiita hamsini, na elfu moja unaiita mia. Ndugu yangu jua umr unapunga mkono😅😅😅
 
Macho kubadilika!
yanakuwa kama mekundu mekundu yaani shida tupu!
 
Kuna moja umenigusa, bustani nashangaa hata hobby hii imetokea wapi!
 
Kuna mama niliongea nae, aliniambia ukikutana na traffic ukawaona ni vijana wadogo au daktari hospitali ukamuona ni kama mjukuu wako. Hapo hakuna ubishi wa chumvi uliyoila duniani.
Kuna siku moja nilienda shule moja ya chekechea aliyokuwa anafundisha rafiki wa kike wa mdogo wangu. Baada tu ya kufika na kukaa kama dakika tano wale watoto wakawa wananong'onezana "wewe Frank baba yako amekuja" hahahahaaaa nilicheka sana nikajisemea kimoyomoyo kumbe sasa ninalazimika kuwa na familia ya watoto kadhaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…