Dalili gani zinakujulisha kuwa umri umesogea?

Dalili gani zinakujulisha kuwa umri umesogea?

Sikumoja nimeenda kwenye sherehe wakati wa msosi nasikia mshereheshaji anasema "karibuni wazee wetu tukapate chakula" mara, "Mzee pale ongoza njia" nikadhani kuna mzee nyuma yangu, nageuka nyuma hakuna mtu! Dah! Nilinyanyuka kama mfanyabiashara kaitwa ofisi za TRA [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ila uzee raha sana! No stress!
 
Hata kwenye ofisi za umma wazee mnapewa kipaumbele.
 
Kuna mama niliongea nae, aliniambia ukikutana na traffic ukawaona ni vijana wadogo au daktari hospitali ukamuona ni kama mjukuu wako. Hapo hakuna ubishi wa chumvi uliyoila duniani.
Sky, umeongea vizuri sana, mimi huwa nakumbana na hiyo, ni kweli madaktari na polisi ninaokutana nao sasa hivi wengi ni watoto wadogo, naona kumbe mimi na wewe tumemeza chumvi ya kutosha
 
Unaelewa maana ya dalili?
Dalili hazina time limit acha kukomaza kichwa kwa mambo madogo,kuna mtu anaweza kuona dalili za kuzeeka akiwa kwenye 40s na mwingine akiwa 50s au hata 60s hatufanani.
 
Mie kuna siku mwendokasi inaanza nikapanda kuona likoje. Nimeingia nimekosa siti kuna mtu mzima akanipisha akaniambia kaa mzee. Nilijitathmini njia nzima na ndio ilikuwa mwisho wa kupanda mwendokasi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa kwani wee sio mzee?
 
Nimeanza utaratibu wa kuangalia taarifa za habari kila jioni, nikikuta mda wa habari watu wanaangukia mambo mengine nawauliza hivi ninyi hamtaki kujua ya duniani!!

Hizi ni dalili nzuri za uhenga!
Afu sijui kwanini wababa wote wanapenda hivyo lol, mie hua nakerekwa had baas.
 
Nilienda kucheza Moira jumamos/jumapili mazoezi nashangaa watu wanamuita mzee nipasie huku,mshua kwangu,dingo niwekee halafu nikiwaangalia nawaona ni wakubwa

Nimeshtuka nishaanza kuwa muhenga pro max
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi nashangaa maisha yangu yote sikuwahi kupenda Maua wala bustani Kwanza nilikuwa Naona wanapoteza muda. SASA hivi hata Mie siamini ninalima tena kwenye containers mboga ikifa au ikiliwa na mdudu natamani kulia. Du uzee shikamoo.
Hii tabia ni ya mama kabisa, hataki vitu vyake kuguswa, yupo radhi atoe kingine ila sio chake. Lol
 
Kunasiku nikapekua stoo nikakuta kaseti mabele nikajua kweli umri ushasonga
 
Itabidi nijirekebishe yaani vijana wangu huwa wanacheka wakiona naksirika eti wamechukua charger yaani kuwaziria ni kawaida siulizi kitu mara mbili. Ila nachekwaje? Itabidi nibadilike Jambo dogo nitalikuuzaa.
Hii tabia ni ya mama kabisa, hataki vitu vyake kuguswa, yupo radhi atoe kingine ila sio chake. Lol
 
Mie kuna siku mwendokasi inaanza nikapanda kuona likoje. Nimeingia nimekosa siti kuna mtu mzima akanipisha akaniambia kaa mzee. Nilijitathmini njia nzima na ndio ilikuwa mwisho wa kupanda mwendokasi
nimecheka aisee
 
Itabidi nijirekebishe yaani vijana wangu huwa wanacheka wakiona naksirika eti wamechukua charger yaani kuwaziria ni kawaida siulizi kitu mara mbili. Ila nachekwaje? Itabidi nibadilike Jambo dogo nitalikuuzaa.
Uzee umewadia hapo mama, hakna namna.
 
Back
Top Bottom