Dalili gani zinakujulisha kuwa umri umesogea?

Dalili gani zinakujulisha kuwa umri umesogea?

Ukiona kwa hiari yako unapunguza na kuacha "unnecessary movements" unapenda sana kukaa nyumbani kwako, ile hali kuhisi sehemu pekee unayokaa kwa amani ni nyumbani kwako hata kama huna pesa na kuna purukushani za kila aina, kiasi ile hata ukitoka au ukisafiri unapata wasiwasi kwa kuhisi huko nyumbani mambo yataharibika, umekariri idadi ya vijiko hadi plastic cups za kijani na unaijua nyumba kuanzia nyufa hadi idadi ya panya yaani hapo umeshafuzu kabisa kuitwa mhenga.
 
Kuna Jamaa humu humu ndani katika thread ya mpira aliuliza inakuwaje Wachezaji wa zamani walikuwa na miili mikubwa ila wasasa wana miili midogo? Kuna Member akamjibu hapana kwakuwa zamani ulikuwa mtoto(Umri mdogo) kwahiyo wale wachezaji ulikuwa unawaona wakubwa ila kwasasa ushakuwa mkubwa(mwili mkubwa) ndio maana unawaona hawa wa sasa wana miili midogo.

Na kweli zamani nilikuwa namuona Treach(Naughty By Nature) ni Bonge la Baunsa(Mbavu Nene) kwenye video na mimi nikawa napiga Nondo sana Gym niwe kama Treach ila nikiangalia video za Treach kwasasa namuona ana mwili mdogo.
 
Wala usipate taabu! Ukipanda daladala, hususani mchana wakati ndani ya daladala hakuna msongamano, basi anza kutupia macho ya udadisi abiria mmoja baada ya mwingine kujaribu kukisia umri wao huku ukilinganisha na wa kwako!

Najua inauma sana lakini ukweli ni kwamba, ukikuta mara kwa mara unaibuka kidedea au labda unakuwa umepitwa na watu wawili au watatu tu basi fahamu, Joash Onyango ile ni sura yake tu lakini kuna uwezekano mkubwa amezaliwa wakati wewe umeshafanya mtihani wa darasa la nne kama sio LY kabisa!
 
Mie kuna siku mwendokasi inaanza nikapanda kuona likoje. Nimeingia nimekosa siti kuna mtu mzima akanipisha akaniambia kaa mzee. Nilijitathmini njia nzima na ndio ilikuwa mwisho wa kupanda mwendokasi
Hakika you made my day,,so ukachanganyikiwa kabisa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna mama niliongea nae, aliniambia ukikutana na traffic ukawaona ni vijana wadogo au daktari hospitali ukamuona ni kama mjukuu wako. Hapo hakuna ubishi wa chumvi uliyoila duniani.
Jinsi salamu ya salamuya shikamoo inavyoendelea kubadilikq. Shikamoo , shikamoo Dada/kaka, shikamoo Baba /mama , shikamoo Mzee, shikamoo babu/Bibi
 
Kuna mama niliongea nae, aliniambia ukikutana na traffic ukawaona ni vijana wadogo au daktari hospitali ukamuona ni kama mjukuu wako. Hapo hakuna ubishi wa chumvi uliyoila duniani.
Ukiona umeanza tabia za kuwa too selective kwenye vyakula ujue hapo hakuna ubishi wa chumvi uliyoila duniani.

Ukiona kama umemaliza kukojoa na kufunga zipu ya suruali yako, kumbe baada ya muda mchache ukagundua mkojo umerudi tena under gravity na kuloanisha suruali yako ujue wewe tayari ni mhenga.
 
Back
Top Bottom