Dalili gani zinakujulisha kuwa umri umesogea?

  1. Unapoenda haja ndogo huku ukiamini kua umefungua zipu na kumbe hujaifungua,
  2. Unapoanza kuisahau njia ya kurudi nyumbani,
  3. Unapoanza kuwachanganya watoto wako kwa sura zao na majina yao.
  4. Unapoanza kula vidonge kama chakula chako badala ya chakula,
  5. Unapokua na appointment za Hospitali kila mara,
  6. Unapoanza kulala mapema na kuamka mapema,
  7. Unapoanza kuutambua umuhimu wa majirani zako,
  8. Unapoanza kuwakumbuka rafiki zako wa zamani na kuwathamini zaidi,
  9. Unapoanza kuachiwa Nyumba na watoto ili ukae nao pindi wahusika wanapotoka out,
  10. Unapoanza kuachiwa funguo na majirani.....
Hii namba 10 [emoji23][emoji23][emoji23]
 
1) Kuanza kujali ratiba zako na muda wako.......

2) Kujiepusha na maugomvi na malumbano yasiyo na msingi......

3) Utaanza kuona thamani na maana na umuhimu wa kuoa au kuwa na familia......

4) Kuwa makini na aina ya mavazi na kauli zako.......

5) Afya yako ya mwili na akili inakuwa kipaumbele chako baada ya fedha na mali......

6) Kuanza kuletewa kesi nyingi za kifamilia kwa ajili ya usuluhishi......

7) Kukumbuka mambo ya zamani mara kwa mara........

8) Kuanza kuwa makini na matumizi yako ya fedha na kuwa mkali kwenye matumizi mabovu ya fedha.....

NB;
Hii ni kwa wale wanaojua kuwa wakati ni ukuta.......na kuishi kulingana na nyakati......
 
Ninapoona ndugu au marafiki wananitegemea kwa matatizo yao iwe kiushauri au kivitendo .nahisi kabisa umri umenitupa mkono japo soon naweza kupata mjukuu

Kiukweli nautamani ujana lakini umri unanivuta shati pamoja na kuhangaika na mazoezi na mlo kamili lakini haizuii raia kuniona umri umekimbia

Pia uzee sio laana ni baraka kama pension inasoma
 
Inaonekana ujana una bandwidth ndogo sana na haudumu, katika life span ya mwanadamu
Hakika na ndo maana kule tunajadili magari na engines zake na si kuhusu mitindo ya nguo na nywele
 
Mie kuna siku mwendokasi inaanza nikapanda kuona likoje. Nimeingia nimekosa siti kuna mtu mzima akanipisha akaniambia kaa mzee. Nilijitathmini njia nzima na ndio ilikuwa mwisho wa kupanda mwendokasi
😂😂😂😂
 
[emoji3][emoji16][emoji23][emoji1787][emoji2][emoji1][emoji28][emoji3][emoji16][emoji23][emoji1787][emoji2][emoji1][emoji28][emoji3][emoji16][emoji23][emoji1787][emoji2][emoji1][emoji28]
 
Siku nilipoambiwa na kulazimishwa kuongoza kikao cha ukoo kama mwenyekiti, asee nikajua sasa nishajumuishwa kwenye orodha ya wazee wa ukoo. Tangu Siku hiyo nikaacha kuvaa pensi kwenye mitoko yangu.
 
Siku nilipoambiwa na kulazimishwa kuongoza kikao cha ukoo kama mwenyekiti, asee nikajua nishajumuishwa kwenye orodha ya wazee wa ukoo. Tangu Siku nikaacha kuvaa pensi kwenye mitoko yangu.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Siku nilipoambiwa na kulazimishwa kuongoza kikao cha ukoo kama mwenyekiti, asee nikajua sasa nishajumuishwa kwenye orodha ya wazee wa ukoo. Tangu Siku hiyo nikaacha kuvaa pensi kwenye mitoko yangu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
unapokuwa na ka notebook kwa ajili ya kumbukumbu
mzee wangu ni mtu wa mambo hizi matukio ya miaka ya 70's anayo kwa notebook

tukio la jana simba kuifunga al ahly leo asubuhi nimepita kumsalimiaia namkuta analiandika pia.
 
1) Kuanza kujali ratiba zako na muda wako.......

2) Kujiepusha na maugomvi na malumbano yasiyo na msingi......

3) Utaanza kuona thamani na maana na umuhimu wa kuoa au kuwa na familia......

4) Kuwa makini na aina ya mavazi na kauli zako.......

5) Afya yako ya mwili na akili inakuwa kipaumbele chako baada ya fedha na mali......

6) Kuanza kuletewa kesi nyingi za kifamilia kwa ajili ya usuluhishi......

7) Kukumbuka mambo ya zamani mara kwa mara........

8) Kuanza kuwa makini na matumizi yako ya fedha na kuwa mkali kwenye matumizi mabovu ya fedha.....

NB;
Hii ni kwa wale wanaojua kuwa wakati ni ukuta.......na kuishi kulingana na nyakati......
Aisee ..mbona huyu ni mimi kabisa😀
 
mzee wangu ni mtu wa mambo hizi matukio ya miaka ya 70's anayo kwa notebook

tukio la jana simba kuifunga al ahly leo asubuhi nimepita kumsalimiaia namkuta analiandika pia.
Mi pia ninazombili za mambo ya kawaida na mambo ya muhim
 
Siku nilipoambiwa na kulazimishwa kuongoza kikao cha ukoo kama mwenyekiti, asee nikajua sasa nishajumuishwa kwenye orodha ya wazee wa ukoo. Tangu Siku hiyo nikaacha kuvaa pensi kwenye mitoko yangu.
hahahaa nimecheka hadi vimachozi vimetoka
 
Palo napoona hata umuhimu wa buku... Inanionyesha kabisa mambo yameanza kuharibika
 
Back
Top Bottom