Dalili gani zinakujulisha kuwa umri umesogea?

Dalili gani zinakujulisha kuwa umri umesogea?

Kuna mama niliongea nae, aliniambia ukikutana na traffic ukawaona ni vijana wadogo au daktari hospitali ukamuona ni kama mjukuu wako. Hapo hakuna ubishi wa chumvi uliyoila duniani.
Kupishwa siti kwenye daladala na mtu ambaye ukimuangalia tu,unaona umemzidi umri.
 
kama umeacha kuwa active na mitandao ya kijamii kama facebook, instagram na mingine inayofanana na hiyo, ni kiashiria moja wapo umri wako umeanza kukutupa mkono.
 
Kuna mama niliongea nae, aliniambia ukikutana na traffic ukawaona ni vijana wadogo au daktari hospitali ukamuona ni kama mjukuu wako. Hapo hakuna ubishi wa chumvi uliyoila duniani.
When the candles in a birthday cake start to cost much than the cake itself.
 
Mi wangu nahisi utanistukiza.

Sioni dalili 🥺🥺🥺😁😁😁
 
Mie kuna siku mwendokasi inaanza nikapanda kuona likoje. Nimeingia nimekosa siti kuna mtu mzima akanipisha akaniambia kaa mzee. Nilijitathmini njia nzima na ndio ilikuwa mwisho wa kupanda mwendokasi
Haaaaahaa
 
Ukiona unapewa shikamoo nyingi kuliko shikamoo unazotoa wewe kwa siku ujue umri umeenda sana
 
Unapoanza kupokea shikamooo hata za watu usiowajua au wasiokujua just ndo Basi tena
Asee hii mimi ilikuwa inanichanganya sana , shkamoo za kutosha , mwanzo nilikuwa nashangaa Ila baadaye imenibidi tu nikubali matokeo
 
Back
Top Bottom