Dalili nane za kuonyesha unaishi kwenye malango yaliyofungwa (closed gates) katika ulimwengu wa roho

Hapa unafundisha watu wawe machawa
 
Sawa Mkuu, tufanyeje Sasa?
 
Sema na na ndoto zinazoashiria mafanikio au milango ya mtu imefunguliwa?
Nyie ni kuwapa tu watu hofu, always ni kuonyesha watu wana shida...

Siamini katika haya masuala.
Hayo mambo yapo Afrika mababu zetu walikuwa wanategemea sana miungu wakawekeana hata maagano Fulani kujikabidhi kwa mizimu ndio hivyo Ile miungu inaendelea kufuatilia kizazi Hadi kizazi
 
Hakuna ulimwengu wa roho wala bibi yake malango ya adui.

Hakuna malango ya baraka.

Matatizo na shida nyingi za waafrika hasa watanzania husababishwa na:

1-Ujinga.
2-Ukosefu wa maarifa.
3-Imani Uchwara za Mungu, Miungu, Shetani, wachawi, mapepo, mizimu, majini na ushirikina.
4-Utawala mbovu/bad governance/ failed state. Nchi iliyojifia tayari.
5-Umaskini.
6- Uvivu wa kufanya kazi.
7- kutegemea miujiza badala ya uhalisia.

Ukiwa na taifa la watu wenye mawazo mgando kama haya. Kupata Maendeleo ni sawa na ndoto za ndaria.
 
Hayo mambo yapo Afrika mababu zetu walikuwa wanategemea sana miungu wakawekeana hata maagano Fulani kujikabidhi kwa mizimu ndio hivyo Ile miungu inaendelea kufuatilia kizazi Hadi

👏👏👏
 
Hapa panachangamoto kubwa hizo tabia ni ngumu kuzivua tunarud pale pale kusali sana na kujituma kuvua hizi unaweza jua makosa ukaja ukasahau yaliyo kupata ukarudi tena
 
Kama Africa na tanzania kila linalofanyika halifiki mwisho na changamoto zinajirudia, nayo imefungwa na huyo adui ?
Hatma ya maisha yako ni wewe mwenyewe, hakuna uchawi wala kusingizia watu...
"Tabia", kitu kinaitwa "tabia", tabia yako ndio mwanzo wa kukuzika au kukufanikisha....

Ukisoma story za watu kama Jack Ma, ingekuwa kibongo bongo jamaa angesema karogwa na angetafuta mchawi, jamaa alikuwa hapati kazi, akaenda hadi KFC kutafuta kazi akakosa, imagine KFC, kwa nchi za nje kufanya kazi KFC au McDonald's au Subway(migahawani) ni kazi kiasi flani zinadharaulika , wanaona ni worst job....

Sasa Jack Ma kakosa kazi hadi KFC, out of 24 applicants jamaa akakosa kazi, mnaenda watu 24, wooooote wanapita kwenye kazi we pekee unakosa.....
Aka apply kazi tofauti 30 zote kakataliwa.

Jamaa ikabidi awe mwalimu wa kiingereza pale China, huko ndipo akaanzisha Alibaba ambapo leo hii ni billionaire...

Imagine angekuwa anaishi bongo..
 
Waafrika hasa watanzania wana imani mgando na mawazo ya kijinga kuhusu suala zima la mafanikio na maendeleo.

Mtu asipofanikiwa wala hajiulizi na kujitathmini kwa nini hajafanikiwa.

Anaanza kuamini kwamba kalogwa, mwingine ana amini ana gundu, nuksi, mikosi, laana na vifungo vya kiroho.

Kumbe ni ujinga wake tu, pengine hana vigezo na ujuzi wa kutosha wa kazi fulani.

Badala ya kwenda kujiongezea value, anaenda kwa wachungaji uchwara kutafuta upako au kwa waganga uchwara kusafisha nyota.
 
Hayo mambo yapo Afrika mababu zetu walikuwa wanategemea sana miungu wakawekeana hata maagano Fulani kujikabidhi kwa mizimu ndio hivyo Ile miungu inaendelea kufuatilia kizazi Hadi kizazi
Hao mababu na wao walikuwa mafala tu, kwanza akili yenyewe hawakuwa nayo, wale wazee walikuwa wajinga, elimu hawakuwa nayo, mtu unazaa albino wanasema mkosi, kazi kukeketa wanawake, inachinjwa kuku wanasema mtoto mwiko kula firigisi, mara paja la kuku ni mwiko mwanamke kula... vizee fala sana vile...

Ndio maana hata wazungu waliwauza sana utumwani, vilikuwa vijinga.. japo si wote.
Kinjekitile na yeye kawakorogea wenzake maji kwamba wakinawa risasi hazitowadhuru...

Huo uchawi wetu Africa ulitusaidia nini kupambana na ukatili na uonevu wa wakoloni, walishindwa kuwaroga wazungu..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…