Dalili nane za kuonyesha unaishi kwenye malango yaliyofungwa (closed gates) katika ulimwengu wa roho

Kazi tunayo kiongozi...
Wajanja wachache wanatajirika kwa sababu wajinga ni wengi...
Acha wapigwe hela..
 
Seen
 
Nyie Ndio sababu watu wanaenda kwa waganga kutapeliwa.

Tufanye kazi jwa bidiii tu ndio dawa mihimu.

Mashetani wakiamka wakilala wewe unapiga kazi,tunza kipato chako,wekeza hata kidogo kidogo.
 
Waafrika waliteswa kama kuku kipindi cha utumwa na ukoloni halafu huo uchawi unaoaminika una nguvu haukusaidia chochote.

Mimi huwa nawaza kama kweli mtu anaweza kupaa na ungo angani kwa uchawi, Ajitokeze hadharani aonyeshe hiyo mechanism inavyo fanyika. Kisha tukuze hiyo teknolojia yake ya usafiri...

Kama mafuta ni damu, Atueleze Mechanism ya hizo Engine za ungo zinavyo tumia hiyo damu.

Kisha tutajua namna ya kukuza usafiri huo.
 
Kuna mda natamani hata nizipotezee mada za hivi ila nikikumbuka kipindi nipo chuo nipo mazoezi, tulisha mpoteza mama na mtoto wakati wa kujifungua kwa misimamo ya kijinga ya familia na mama mwenyewe ,eti kisa wameambiwa na nabii mmoja maarufu, huwa naona kuna upotoshaji mkubwa sana .
 
Suluhisho ni nini sasa mkuu?
Umtafute huyo mganga akutapeli yaani yeye apande kifedha wewe uporomoke. Ukumrudia kuwa mambo yamekwama Bado atakuletea story ingine akung'oe kibunda Tena.
Mafanikio ni kuwa uwelewa wa kazi, uwe pahala na wakati mzuri kwa mafanikio yaani right person au skills, right place and right time.
 
Haya mambo ya kufungwa kiroho yapo
Mimi Nina experience
 
Mi huwa natafakari kwanini tusitumie huo uchawi tushinde kombe la dunia, waitwe wachawi na waganga wa jadi nchi nzima waweke nguvu moja, tufuzu kombe la dunia na hatimaye tushinde.

Lakinimatokeo yake utaona wanaoshinda si bahati wala uchawi, unaona ni timu zenye kujituma katika mazoezi, wachezaji wenye vipaji... in short juhudi binafsi...

Haya mambo watu wasahau.
 
Mtu ana upungufu wa damu badala kumpeleka Hospital, wanampeleka kwa mchungaji..
 
Halafu mtu ukimwambia kwamba hakuna uchawi anakataa.

Unakuta mtu anakomaa kusema kuna uchawi, ila ukimwambia atumie huo uchawi au ushirikina atajirike hawezi.
 
Uzi umeuweka hapa kuwatisha watu, oyaaa wanangu tupambane tu na tuondoe uoga nothing comes easy, ondoa aibu, do what is right. Keep your faith positive. Maana wengi wanajihisi kama wamerogwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…