Dalili nyingi mwilini na vipimo sijapata

Joined
Jan 16, 2018
Posts
18
Reaction score
0
Dooo doctor mimi sasa hii yapata mwezi na nusu naona dalili za ambazo zinanitisha, mwazoni kabla nilikua nasumbuliwa na homa za hapa na pale nikaendae mnazi mmoja nikapata vipimo vya kawaida sina kitu wala ukimwi, pima sana, nilipata antibiotic nikatumia, lakini sasa hii sasa hii inanitisha hua nasikia mifupa inaniuma, kidonda Chang hiv nimeweka dawa baada ya kua wiki 3 na siku 4 hakiponi, uchovu wa ajabu, nawashwa mda mwingine, joto kupanda, tumbo dalili nyingi zinanitishia maisha, gharama za vipimo vikubwa siwezi kuzimudu, nina miaka 23 , watu ninaowaeleza wananitisha wanasema itakua kansa ya damu, sina raha tangu mwaka umeanza, mi mwenyewe nasoma ufundi na sijamaliza, naomba msada wako dr
 
Pole sana dogo,, nenda lugalo ama palestina,,
 
Tumia juice ya mtafeli unapoendelea na ushauri mwingine kwa kutumia majani ya mstafeli na kusaga kwa slender pole sana ndugu
 
Unaoma ufundi gani maana aina ya kazi pia inaweza kusababisha ugonjwa fulani
 
Tumia juice ya mtafeli unapoendelea na ushauri mwingine kwa kutumia majani ya mstafeli na kusaga kwa slender pole sana ndugu
Juice ya stafeli kwan ansumwa nini hasa?.....au ndio mambo ya wasiojulikana kila sehemu....UNAUMWA UGONJWA ISIOJULIKANA UNAKUTANA NA DAKTARI WASIOJULIKANA NAO WANAKUPATIA TIBA ZISIZOJULIKANA....ahahaaa
 
Maumivu ya mifupa ni moja Kati ya dalili za kansa ya mifupa, nakushauri uwahi hospitali kucheck Afya. Jitahidi Sana hata Kama gharama Ni kubwa, ugonjwa ukiwa chronic gharama zitakua kubwa zaidi.
 
Juice ya stafeli kwan ansumwa nini hasa?.....au ndio mambo ya wasiojulikana kila sehemu....UNAUMWA UGONJWA ISIOJULIKANA UNAKUTANA NA DAKTARI WASIOJULIKANA NAO WANAKUPATIA TIBA ZISIZOJULIKANA....ahahaaa
Wewe mwenzio anaumwa alafu wewe unakuja kujichekesha chekesha hapa km gasho. Kuwa na busara
 
pomoja na ushauri wa juu hapo, ni antibiotics gani hizo ulizotumia mpaka sasa?
vipimo gani umepima?

hicho kidonda ulichoweka dawa kilitokana na nini na unacho tangu lini?
 
Typhoid, malaria, UTI, HIV, basi, na kidonda kina wiki 3 na nusu, antibiotics nilitumia mwaka jana nilipokutwa sina magonjwa hayo inaitwa amoxlin cavvana kama sikosei, na mkojo Wang ni mchafu haubadiliki tangu mwaka jana
 
Ndugu kurudi tena hospitali kwa uchunguzi na matibabu zaidi ni muhimu maana kwa maelezo yako inabidi daktari achukue historia yako na afanye physical examination in details then akufanyie vipimo vitakavyosaidia kujua tatizo ni nini. Kama hali haitaonekana bado unayo nafasi ya kutumia utaratibu wa kuwaona mabingwa.....jitahidi kushirikisha ndugu na jamaa ili usaidiwe kipesa, maana kuishi bila kujua unaumwa nini pia ni ugonjwa tosha.
 
Ha
Ulipima kisukari?
Hapana, ila mazoezi na kucheza mpira nilikua nafanya kilasiku, niliamua kuacha baada ya kuanza kujisikia vibaya nilipoludi mazoezini na kidonda ambacho alinichea lafu mwezangu, na mguu wa pili nao nilikuja kuvimba mazoezini, cha ajabu uvimbe ulichelewa kupona ambapo sio kawaida yangu, nilipona baadae ila umeniachia kinundu kidogo ambacho ninacho kwa mguu
 
Nenda kapime kisukari
 
Ndugu kurudi tena hospitali kwa uchunguzi na matibabu zaidi ni muhimu maana kwa maelezo yako inabidi daktari achukue historia yako na afanye physical examination in details then akufanyie vipimo vitakavyosaidia kujua tatizo ni nini. Kama hali haitaonekana bado unayo nafasi ya kutumia utaratibu wa kuwaona mabingwa.....jitahidi kushirikisha ndugu na jamaa ili usaidiwe kipesa, maana kuishi bila kujua unaumwa nini pia ni ugonjwa tosha.
Asante bro, ila hali yetu kwa sasa sio nzuri, nikimwambiaga mama yang tatizo langu huwa analia sana tukiwa tunasali maana yeye ni mkristu , hiv nakunywaga dawa za maumivu panado kunipunguzia homa,
 
Back
Top Bottom