Uchaguzi 2020 Dalili ya mvua ni mawingu. Vyama vya upinzani vimekubali kushindwa kabla ya mtanange kupigwa

CCM inashindana na mtu aliyepigwa pingu na yuko kifungoni. Hakuna haja ya tambo na majivuno. Washindani wamekuwa jela miaka yote mitano kutokana na marufuku za kufanya siasa. Tume ya uchaguzi, sheria na kanuni za uchaguzi, mahakama na vyombo vya usalama vyote vinaibeba CCM. Kwa hari hii uko sahihi 100% kwa CCM kuendelea kutawala - watu watake au la.
Uchaguzi utafanyika 2025:
> Kutakuwa na Katiba Mpya,
>Itaongezeka idadi ya wapiga kura vijana wasomi,
>idadi ya wapiga kura wazee wajinga wafia ccm itakuwa ndogo, na
>wanachi watakuwa wameamka kisisa.
 
2025 Ccm itakuwa imefanya makubwa sana zaidi ya haya maradufu. Upinzani utakuwa umekufa kabisa.
 
Hakuna cha kulazimisha matokeo ni kwamba wananchi wa wamekubali mziki wa Ccm. Uchaguzi wa serikali za mitaa mlisusa. Hizo habari zingine ni visingizio vya kushindwa.
Mkuu sina mengi ya kukueleza ila nina jambo moja tu."Nchi hii ni mali ya Watz na siyo ya ccm"
 
Wahenga walisema ukiona wingu zito limetanda angani ujue kuna mvua kubwa inakuja kunyesha hivyo chukua tahadhari na tafuta mahala salama ujikinge. Siku zinazidi kuyoyoma na wapinzani wa CCM ndio wanazidi kunywea maana wanajua kwenye uchaguzi wanaenda kukutana na kichapo cha ukweli.

Ninajua wanajiuliza majukwaani watanadi sera gani? Wanakosa majibu. Wanajiuliza tukisimamisha wagombea wa ubunge wanakosa majibu nani atafaaa au nani atarudi tena. Wamekuwa wa baridi na hatusikii hata dalili za watia nia wao maana kila jimbo ni kama kuna shoti ya umeme na wanaogopa kuweka mkono.

Lakini nini hasa sababu ya haya yote? Ni uadilifu, uchapakazi na uzalendo wa JPM ndio umeipa nguvu na kiburi CCM na sasa ina uhakika wa kuchukua kiti cha ubunge au udiwani katika eneo lolote. Maana ni ndani ya miaka minne tu, watu wameshuhudia mabadiliko makubwa sana.

Sekta ya afya, elimu, miundombinu na ulinzi na usalama zote zimeimalishwa. Wapinzani uchwara wanaona aibu tu kukubali na kukaa kando. Lakini wangekuwa na busara wangetulia na kukaa kando.
MBONA WAPINZANI WAKIFANYA MIKUTANO WANADAKWA...

ova
 
Kwa jinsi ratiba ya uchaguzi itakavyokuwa "tight" mwaka huu, huku wapiga kampeni ikiwapasa kuwafikia wapiga kura sehemu mbalimbali za majimbo yao ya uchaguzi hapa nchini.

Nami pia naungana na Mkuu Chagu pia kuziona dalili za baadhi ya vyama, kwa kuleta visingizio za sababu za kiafya za wagombea wao, wataweka mpira kwapani na kifufua tena suala la tishio la mlipuko mpya wa COVID-19 hapa nchini, ili kuhalalisha sababu za kuuhairisha uchaguzi wa mwaka huu.
 
2025 Ccm itakuwa imefanya makubwa sana zaidi ya haya maradufu. Upinzani utakuwa umekufa kabisa.
Jadi ya mjinga, kwa maana ya asiyeelewa, ni kuwafanya wenzake watu wengine wajinga.
Lowasa, akingali PM, aliwahi kuonya kuwa ukosefu wa ajira ni bomu la kitaifa. Wapenda mabadiliko wanashukuru kuwa kilichofanyika mpaka sasa kujenga shule za Kanumba maana nazo zimeongeza jeshi la wanamabadiliko.
CCM inatia huruma. Flyovers, SGR, barabara za lami, umeme, nk. vimecheleweshwa na CCM. Ni vitu vya kawaida kabisa nchi kama Kenya, Ethopia, nk. Mradi wa Stieglers wa wat 2000 unaimbwa si lolote kulinganisha na SA wa10,000.
Viwanda 100 kwa @ wilaya viliishia wapi?
 
Kwa jinsi ratiba ya uchaguzi itakavyokuwa "tight" mwaka huu, huku wapiga kampeni ikiwapasa kuwafikia wapiga kura sehemu mbalimbali za majimbo yao ya uchaguzi hapa nchini.

Nami pia naungana na Mkuu Chagu pia kuziona dalili za baadhi ya vyama, kwa kuleta visingizio za sababu za kiafya za wagombea wao, wataweka mpira kwapani na kifufua tena suala la tishio la mlipuko mpya wa COVID-19 hapa nchini, ili kuhalalisha sababu za kuuhairisha uchaguzi wa mwaka huu.
Adui muombee njaa.
 
Kama uliyosema ni kweli,
Kwanini CCM dola haitaki wapinzani wafanye kampeni?
Na kwanini serikali hii unayodai inapendwa saaaaana na wananchi,ilikimbilia Bungeni tena kwa hati ya dharula kutunga sheria ya kinga ya kushitakiwa kwa viongozi wote wakuu,kama mnapendwa,kinga za nini?mnaogopa nini?
Asili ya Jinga ni UOVU. Ukiona mtu anapenda KINGA NI MUOVU KAMA WAOVU WENGINE TU.
 
Mkutano wa ndani uligeuzwa ukawa wa kampeni. We hujaona wale akina mama wanakata mauno alafu Zitto anachekelea?
Kampeni huwa zinafanyikia kwenye kumbi?Wakikaa wanachama wa chama kimoja cha siasa ukumbini wanayoyaongea yanawezaje kuwaathiri watu ambao siyo wasikilizaji wa hizi hoja?Msiwapangie kwenye vyama vyao agenda za vikao vyao,siyo sahihi na ni matumizi mabaya ya raslimali za Taifa.Kuwakamata watu wasio na hatia kama majambazi na kuwasafirisha kwa misafara na baadaye wanaonekana hawana makosa.Huu ni ufasadi.
Itafikia hata kuongea mambo ya ndani ya familia mtataka kuyapanga ninyi?
 
We ile clip hujaiona?
 
Wahenga walisema ukiona wingu zito limetanda angani ujue kuna mvua kubwa inakuja kunyesha hivyo chukua tahadhari na tafuta mahala salama ujikinge. Siku zinazidi kuyoyoma na wapinzani wa CCM ndio wanazidi kunywea maana wanajua kwenye uchaguzi wanaenda kukutana na kichapo cha ukweli.

Ninajua wanajiuliza majukwaani watanadi sera gani? Wanakosa majibu. Wanajiuliza tukisimamisha wagombea wa ubunge wanakosa majibu nani atafaaa au nani atarudi tena. Wamekuwa wa baridi na hatusikii hata dalili za watia nia wao maana kila jimbo ni kama kuna shoti ya umeme na wanaogopa kuweka mkono.

Lakini nini hasa sababu ya haya yote? Ni uadilifu, uchapakazi na uzalendo wa JPM ndio umeipa nguvu na kiburi CCM na sasa ina uhakika wa kuchukua kiti cha ubunge au udiwani katika eneo lolote. Maana ni ndani ya miaka minne tu, watu wameshuhudia mabadiliko makubwa sana.

Sekta ya afya, elimu, miundombinu na ulinzi na usalama zote zimeimalishwa. Wapinzani uchwara wanaona aibu tu kukubali na kukaa kando. Lakini wangekuwa na busara wangetulia na kukaa kando.

Chini ya Magufuli hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Naona unachanganya mada. Hakuna kinga ya viongozi wasishitakiwe. Watashitakiwa ila kupitia kwa Ag. Fuatilia mambo kwa undani.

Madictator wote hawako tayari kushitakiwa. AG Ni mteule wa rais anawezaje kukubali rais ashitakiwe?
 
Masharti yapi
Mbona wakiwa kwenye mikutano yao ya ndani wanavamiwa

Ova
Walitakiwa wajadili masuala yao sio kukata viuno na kuichamba Ccm. Maana huko ni kuhatarisha amani je wafuasi wa Ccm wangewapopoa mawe?
 
Madictator wote hawako tayari kushitakiwa. AG Ni mteule wa rais anawezaje kukubali rais ashitakiwe?
Kuna kesi ngapi ambazo serikali inashitakiwa na Ag anasimama kwa niaba ya serikali?
 
Chini ya Magufuli hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Hizo ni hisia zako. Maana wananchi hawawezi kuchagua walevi wa konyagi wakaacha kuchagua watu watakao watumikia.
 
hakuna anaye weza kujipima ubavu na RAis Magufuli, hata hao wagombea wa upinzani wanaenda kugombea kama ushahidi tu.....lkn mbele ya JPM wametepeta kabla mechi haijaanza
 
Back
Top Bottom