Dalili za awali za mke/mume mwema

Kabisa mkuu, mabinti wote hawafanani hata kama utandawazi utakuwa vipi, kwani kila binti ana malezi aliyolelewa
Umesema kweli kabisa, baadhi ya watu wanachukulia malezi ya jamii yao wanadhani vijana wote wamelelewa hivyo. Bado wako wazazi wenye hofu ya Mungu wanaosimama na watoto wao mwanzo mwisho
 
A million dollars advice. Tunaposikia haya toka kwa wanawake wenyewe inaleta nguvu ya ajabu hata kwa mabinti wanaosoma humu. Ndugu zangu nawasihi sana, msidanganywe na tamaduni za kimagharibi zilizoshindwa tayari, hizo zimelenga kuharibu mfumo wa maisha ya ndoa.

Asante sana mkuu kwa neno hili, Mwenyezi Mungu akujalie kila jema unalolitamani.

Amina
 
Amen
 
Kwangu mke ni yule anayependa nipate furaha tu, izo nyingine ni mbwembwe
Kumbuka mkeo ndiye atakayelea watoto wako, sasa wewe oa kwa kutafuta kujifurahisha. Majuto ni mjukuu...
 
Kwangu mke ni yule anayependa nipate furaha tu, izo nyingine ni mbwembwe
Hapo utapotea mkuu. Hatuoi ili mke atupe furaha, tunapaswa kuwa na furaha ndipo tuoe. Ingia kwenye ndoa ukiwa na furaha, usimpe mtu mwingine jukumu la kukupa furaha utafeli vibaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…