Damascus: Waasi wa HTS wauzingira mji wa Homa nchini Syria

Damascus: Waasi wa HTS wauzingira mji wa Homa nchini Syria

Hezbollah,Iran na Urusi zilizokuwa nguzo za Assad zote zina matatizo ya kuyakabili hamna mwenye hamu na Assad.

Ndege za Urusi zinawashambulia ila wanazidi kuteka maeneo tu.... kiufupi Assad hana jeshi la kushikilia mji
Hawawezi kumchoka kwa sababu Syria ni muhimu sana kwao kimkakati hivyo Asad ni muhimu sana kwao.

Kama ambavyo Asad anawahitaji Iran, Urusi na Hizbullah kwa ajili ya kulinda madaraka yake ,ndo hivyo hivyo kwa Urusi,Iran na Hizbullah wanavyo muhitaji Asad kulinda masilahi yao.
 
Moja ya agenda ya Marekani ni kupitisha bomba la mafuta na gesi toka central Asia huko kwenda Europe nchi moja nadhani ni Azerbaijan kama sikosei , wamejaribu miaka mingi imeshindikana na ndio maana wana ugomvi na Assad miaka yote ,kwa sababu aligoma , na pia Russia hawezi ruhusu hii kitu ,kwa sababu analinda soko lake la nishati hapo Europe ,na pua USA ana interest ya mafuta kwenye baadhi ya territories humo Syria , pia Saud anachuki ya muda mrefu na Syria kwa sababu amekuwa mtiifu kwa IRan na kuwa na ushirikiano nao ,Saud ni kiongozi wa Sunni Muslims so ugomvi wake na Iran malipizi no kufund mercenaries WA ugaidi huko Iraq na Syria na ndio sababu ya IRan kuamua kutengeneza Shida militias za kupambana na hawa washenzi , Israel ni supporter wa hawa magaidi pia na yeye inajulikana lengo lake ni ili kuleta chaos karibu na IRan , Turkey naye ana support hawa magaidi akiamini wakiingia madarakani atakuwa na upper age ya kuwazima wakurdi kitu ambacho ni ndoto
Kumbuka IRan ni lazima atumie Syria na Iraq kama buffer zones dhidi ya hujuma za Israel na kutumia kama conduit ya kusafirisha silaha kwenda kwa Hezbollah ambao ni proxy wake ili kujilinda na threats za Israel
Wewe umekuja na habar za ndani kabisa
 
Uturuki ni mwanachama wa NATO hilo ni hakikisho la usalama la kudumu.

Uturuki ina uwezo wa kuzuia hiki kinachofanywa na waasi hapo Syria ikitaka, ila haitofanya hivyo Ili kuendelea kuwaweka Urusi, Iran na Assad kwenye shinikizo.
Lakini upepo utakapo anza kubadilika atapoteza mazima maana hawa waasi mwaka 2020 walikuwa wamesha zidiwa kabisa na walikuwa wanakaribia kuangamizwa lakini Uturuki akawalaghai Iran na Urusi wakubali kusaini mkataba wa amani kumbe ilikuwa ni mbunu ya kujipanga upya.
Sasa iwapo waasi wakizidiwa tena unategea Uturuki atatumia ushawishi gani kuwalaghai tena washirika wa Syria wamuelewe?
 
Iran, sijui Al jazeera, Assad, Ayatola, Uturuki, Tahariri ya shama, Hawa wote ni wahuni tu wanatumia mgongo wa dini kupigania maslahi binafsi.

Jiulize Utawala wa kiislamu wa Iran unamuunga mkono Assad mwenye utawala wa kisecular, halafu unawapinga waasi wanaotaka kuanzisha utawala wa kiislamu!

Huu si ni uhuni tu.

Halafu akina Ritz wanatokwa povu kila siku kushabikia ujinga.
Hapo hakuna mgogoro wa kidini bali huo ni mgogoro wa kugombea madaraka acha ujinga.
 
Saud unamwonea tu hapo

Yeye ashaga sema anajenga nchi yake hataki ugomvi na mtu
Saudi anatoa hela ili ku fund hilo group!

Msaudi anagombea ukaka mkubwa hapo mashariki ya kati na Iran. Kete turufu anayoitumia ni ya kimadheheb ya kidini ili atimize malengo yake.

Huo mgogoro hapo Syria ni mkubwa kuliko watu humu wanavyoshadadia kwa kidini!

Russia hapo Syria analinda maslahi yake kuzuia bomba la gesi linalotaka kupitishwa na Marekani kuelekea nchi za ulaya ili kuudhofisha uchumi wake. Baada ya Assad kukataa huo mpango wa Marekani nchini mwake ndipo akaundiwe zengwe hilo!

Iran anapitisha silaha zake Syria kuelekea kwa Hizbullah, ambao Israel anaona kwake ni tishio la usalama wake hivyo naye na kaka yake Marekani wapo kuzuia hilo!

Turkey kwa upande wake ni kuhusu kuwadhibiti wa kurdi.

Iran naye kama Marekani alivyoanzisha axis yake na Iran naye vivyo hivyo ili aweze kujilinda dhidi ya USA na Israel na vibaraka wengine hapo mashariki ya kati.

Syria ipo eneo la kimakakati, ndiyo wakubwa wanalinda maslahi yao. Hivyo hao magaidi ni wa kutengenezwa.
 
Usitishe watu huyo urusi na yy anasubiliwa vilevile akijichanganya watu wanampelekea moto kwani hao waasi safari hii hawajaja kizembe wanazo hadi drone za kutungulia ndege kwahiyo urusi ajishkilie,

Mfupa wa ukraine umemkwama hawezi tena kujigawa maana vita imechukua muda mrefu na resources zimeanza kukata so aamue aende akamsaidie asada na ateme bungo ukraine

Yaani hii tunaita ugali moto mboga moto
He siku hizi kuna drone zinatungua ndege hili ni jipya.
 
Israhell si anaripua silaha za Iran kila siku sasa analia lia nini israhell kuingiza jeshi kwa sasa sioni ikitokea ila acha tuone kubwa atakua wanashambulia kama anavyo shambulia kila leo hizbullah haijafa kiasi cha kushindwa kuisaidia Syria yaani ili Syria ianguke basi Iran na Russia wambwage hapa Assad hapindui ila kinyume na hapo Syria itaendelea kua chini ya Assad sana mwaka ule vita ilipaganwa mpaka Damascus yaani Assad alikua kabakiza mji mmoja tu ambao ni Damascus pekee ila ikapigwa vita ya kufa na kinyama ambayo nakumbuka wakati ule waliifananisha na vita ya hitler na ussr ambayo majeshi ya German yalitoa dozi mpaka Moscow ila mwisho mambo yakabadilika kikatoka kipigo hapo brek ikawa Berlin ndio kama hii ya mara hii tuone kama hatimae sehemu kubwa ya Syria itarudi kwa Assad kama mara Ile ama ngoma ndio finito ragaso ila ngoja tuendelee kuona nipo pamoja na mwanangu Assad ila usichelewe kutuma maombi rasmi pale Tehran unangojewa wewe tu ila hii inapoelekea
Waislam mnapenda/mnafundishwa kuwa Delusional sana.

Ni jambo halitaki ujuzi mkubwa kutambua, Jeshi la Assad linacollapse kuliko walivotarajia, Hezbollah viongozi na makamanda wake wengi wamekufa au ni vilema na Bado wako standby Lebanon kuona kama Israeli itaenda ndani zaidi ya Lebanon, pia Israel ilishambulia Hadi benki za Hezbollah, na vyanzo vingine vya mapato hivyo Iran na Assad wameumiziawa mashirika wao mkubwa sana.

Assad, Iran na Urusi hawawezi Kuisaidia Assad kwa muda mfupi zaidi ya kutafuta uwezekank wa Kuigawa Syria kwenye vitaifa vidogo vinavyowaunga mkono.

Hapo Syria kwa sehemu kubwa ni vita ya Kidini Kati ya Waislam na Waislam hawagombei Democracy au Uchumi now Wanapigana kulipa Kisasi na kueneza Ushia na Sunni.

Hata kama hawasemi popote pande zinazopigana Zinatamani Israel iwe upando wao, Kwa Assad/Iran/Hezbollah wanatamani msaada wa Israel kuzuia advances za Waasi na wao wawe kama buffer state Kati ya Israel na hao Wasunni ambao wametokana na ISIS.

Same Wasunni wanatamani Israel iendelee kuishambulia Syria na Hezbollah wao waziri kusonga mbele.

Hapa itakavokuwa kuna Chance kubwa Israel kuingia Syria upande wa Golan, na Hata kuzungumza na Waarabu wa Druze waunde Nchi Kati ya Israel na Damascus
 
Saudi anatoa hela ili ku fund hilo group!

Msaudi anagombea ukaka mkubwa hapo mashariki ya kati na Iran. Kete turufu anayoitumia ni ya kimadheheb ya kidini ili atimize malengo yake.

Huo mgogoro hapo Syria ni mkubwa kuliko watu humu wanavyoshadadia kwa kidini!

Russia hapo Syria analinda maslahi yake kuzuia bomba la gesi linalotaka kupitishwa na Marekani kuelekea nchi za ulaya ili kuudhofisha uchumi wake. Baada ya Assad kukataa huo mpango wa Marekani nchini mwake ndipo akaundiwe zengwe hilo!

Iran anapitisha silaha zake Syria kuelekea kwa Hizbullah, ambao Israel anaona kwake ni tishio la usalama wake hivyo naye na kaka yake Marekani wapo kuzuia hilo!

Turkey kwa upande wake ni kuhusu kuwadhibiti wa kurdi.

Iran naye kama Marekani alivyoanzisha axis yake na Iran naye vivyo hivyo ili aweze kujilinda dhidi ya USA na Israel na vibaraka wengine hapo mashariki ya kati.

Syria ipo eneo la kimakakati, ndiyo wakubwa wanalinda maslahi yao. Hivyo hao magaidi ni wa kutengenezwa.
Asante sana sirudii tena kuulizia chanzo cha mgogoro na hii comment naitunza kabisa
 
Siyo kwamba hiyo ni jihad hao jamaa wanataka wasimike utawala wa kiislamu ndo maana wanapigana ili wamwondoe kafiri Assad
Kama wao ni sunni wasingekuwa wanauwa sunni wenzao!

Wameuwa sunni kibao hapo Syria mfano mwanawazuoni wa kiislamu mkubwa hapo Syria anaitwa Sheikh Bouti. Wamemuuwa akiwa msikitini anatoa darasa kwa bomu la kujitoa mhanga.

Wamechinja sunni kibao huko Iraq. Wameuwa Sunni kibao huko Yemen mfano mwalimu wa Sheikh Al Habib Ally ibn Jifry ambaye ni Sunni. Tena huyu Sheikh ni kitukuu wa Mtume ila wamemuulia sheikh wake.

Hao watu ni mpango maalumu wa wakubwa! Kuna kipindi walipigwa wakaenda kutibiwa Israel na Netanyahu akaenda kuwatembelea.

Sasa jiulize hao waislamu ni wa aina gani ambao wanaonekana ni watata sana halafu wanafanya hivyo kwenda kutibiwa Israel? Au hata sikumoja hata kwa bahati mbaya hawajawahi kurusha kombora hata Israel?

Mbona Houth anarusha? Wao kipi kinawazuia? Hao ni project maalumu ya wakubwa.

Vikundi vya wana mgambo kutokea Iraq wanaenda kupambana nao huko Syria, Marekani anatumia helicopter zake kuwashambulia ili wasiende Syria, hapa unapata picha gani?

Yaani Marekani inawasidia magaidi?!
 
Marekan, ufaransa hawa nawajua kabisa kuwa ni magaid tokea zaman
 
Hujui dunia inavyojiendesha mkuu we tulia. Jiulize kwanini marekani na Israel imeshambulia makundi ya washia waliotoka Iraq waliokuwa wanavuka mpaka kwenda kumsaidia Assad. Na wamerud nyuma.
Nimeona hii kitu daah haipaswi kuonyeshwa....
 
Tafuta kitabu kinachoitwa Refuting ISIS!

Kimeandikwa na Sheikh kutoka Syria ambaye ni kitukuu wa Mtume Muhammad S.A.W, anaitwa Sheikh Muhammad Al Huda Al Yaaqoubi. Ni sunni huyu Sheikh.

Sheikh Muhammad anakuambja hao wote ni motoni. Hakuna muislam hapo!

Saudi Arabia masheikh ambao wanaopinga mwenendo wa serikali kwa mambo wanayoyafanya wapo gerezani wamefungwa.
 
Breaking News Wakuu,habari zinasema mapigano ni makali sana usiku huu kwenye viunga vya Mji wa Homs, habari nyingine zinasema Waasi wameshazivunja Ngome za Jeshi la Syria Arab Republic.

Habari nyingine zinasema Ndege za US na IDF zinashughulika na Shia Millitias waliongia kutokea Iraq.

Source:Aljazeera
 
Waislam mnapenda/mnafundishwa kuwa Delusional sana.

Ni jambo halitaki ujuzi mkubwa kutambua, Jeshi la Assad linacollapse kuliko walivotarajia, Hezbollah viongozi na makamanda wake wengi wamekufa au ni vilema na Bado wako standby Lebanon kuona kama Israeli itaenda ndani zaidi ya Lebanon, pia Israel ilishambulia Hadi benki za Hezbollah, na vyanzo vingine vya mapato hivyo Iran na Assad wameumiziawa mashirika wao mkubwa sana.

Assad, Iran na Urusi hawawezi Kuisaidia Assad kwa muda mfupi zaidi ya kutafuta uwezekank wa Kuigawa Syria kwenye vitaifa vidogo vinavyowaunga mkono.

Hapo Syria kwa sehemu kubwa ni vita ya Kidini Kati ya Waislam na Waislam hawagombei Democracy au Uchumi now Wanapigana kulipa Kisasi na kueneza Ushia na Sunni.

Hata kama hawasemi popote pande zinazopigana Zinatamani Israel iwe upando wao, Kwa Assad/Iran/Hezbollah wanatamani msaada wa Israel kuzuia advances za Waasi na wao wawe kama buffer state Kati ya Israel na hao Wasunni ambao wametokana na ISIS.

Same Wasunni wanatamani Israel iendelee kuishambulia Syria na Hezbollah wao waziri kusonga mbele.

Hapa itakavokuwa kuna Chance kubwa Israel kuingia Syria upande wa Golan, na Hata kuzungumza na Waarabu wa Druze waunde Nchi Kati ya Israel na Damascus
Kuunasibisha mgogoro wa Syria na masuala ya dini ni kipimo cha ukosefu wa akili.
Mgogoro wa Syria kuna Urusi,Iran, Uturuki, Marekani, Israel, Ufaransa, Uingereza,Mataifa yote ya ghuba kwahiyo hayo mataifa yote yanapigana kwa ajili ya dini?
 
Back
Top Bottom