Damascus: Waasi wa HTS wauzingira mji wa Homa nchini Syria

Damascus: Waasi wa HTS wauzingira mji wa Homa nchini Syria

Breaking News Wakuu,habari zinasema mapigano ni makali sana usiku huu kwenye viunga vya Mji wa Homs, habari nyingine zinasema Waasi wameshazivunja Ngome za Jeshi la Syria Arab Republic.

Habari nyingine zinasema Ndege za US na IDF zinashughulika na Shia Millitias waliongia kutokea Iraq.

Source:Aljazeera
Wamarekani nao wanashiriki kupigana jihad?

Cc ITR
 
Usipate taabu op. 3 inakuja general wa Iran kahakikishia waandishi juzi walimuuliza, May be anasuburi silaha za trump ndio aziangamize huwezi jua kwenye hili tumwachie Ayatollah mwenyewe ndio anajua nini kitafaa Kwa muda Gani. Israeli ni wajinga wanahisi wao watakaa Kwa utulivu Kwa haya wanayoyafanya Lebanon siku wakipata AD systems Ngoma itakua tamu Sana ya hizbollah
Anachelewa sana.kipindi kile alisema ilikuwa ndani ya week moja sasa miezi inaenda miwili. Na alishajipandishia red flag. Kile kitendo walifanya wazayuni kilikuwa cha kudhalilisha sana.... Yaani wanawake wanaingia Iran wanalipua sehemu za silaha halafu wanaondoka? Nikiwaza naumia sana.
 
Hawa Waasi wa Kisunni HTS wananishangaza mimi, nijuavyo ni "Ragtag Guerrilla Millitias" lakini wanavyopiga Atillery kwa ufanisi na kwakutumia GPS ni Bullseye kila mara mpaka wamewachanganya Makamanda wa Jeshi la Serikali ya Syria.
Sijui wamefundishwa wapi? Daah!!
 
Katika hi vita usitegemee aljazeera kama chanzo chaku kikuu kukupa taarifa kwasbb iko pro-waasi wa kisunni nikama BBC kwa vita ya Ukurain na Russia.
Serikali ya Sytia ina firing power ya ndege kutoka Russia na Iran sio rahisi kuteka mji na kuutawala wakati ndege zinarusha mabomu.
Ndege haziteki Miji
 
Kuunasibisha mgogoro wa Syria na masuala ya dini ni kipimo cha ukosefu wa akili.
Mgogoro wa Syria kuna Urusi,Iran, Uturuki, Marekani, Israel, Ufaransa, Uingereza,Mataifa yote ya ghuba kwahiyo hayo mataifa yote yanapigana kwa ajili ya dini?
Wewe Ndio mjinga... Kwa Nini wameshindwa kuutatua huo mgogoro miaka zaidi ya 10 sasa.

Wakati wanaenda kutatua mgogoro wa Ukraine na Russia ambao vita yake ni kubwa zaidi na hatari?

Syria yenyewe bila mtu yoyote kuingilia imegawanyika kimatabaka... Sababu maandamano na Vita ni kumtoa Assad, sababu ya kumtoa ni Kuwa Wasyria wengi ambao ni Waarabu wa Kissuni kutoridhiswa na Serikali yao inayotokana na Jamii ya Watu Kabila/dhehebu la Kishia linaloitwa Alawiites.

Kumtoa Assad ikachukuliwa kama kitendo kisichokubaliwa na Jamii za Kishia Mashariki ya Kati.. Iran, Hezbollah na Wapiganaji wengine wa Kishia wakaanza kuingia Syria kumlinda Assad dhidi ya Wasyria wengine ambao ni Wasunni.

Uturuki anasababu kuu mbili za Kupigana au kuchagua upande.

Uturuki Ndio nchi iliyopokea Wakimbizi wengi sana, kwa hiyo ni obvious lazima itafute utaratibu wa kupambana na changamoto hiyo, jambo la pili baada ya Hii vita Jamii ya Wakurdi Syria wakatumia Nafasi hiyo kuunda nchi ndani ya Syria hii ni hatari kwa Uturuki sababu inawapa Hamasa Wakurdi wa Uturuki kudai nchi yao pia.

Israel kwa upande wake hataki Syria iwe base ya Iran, pia hataki Silaha ziende Lebanon, pia hataki ISIS wame karibu na mipaka yake Ndio maana lazima aingilie

Russia ana base ya navy Syria ambayo inaisaidia sana kwenye bahari ya Mediterranean, so kama Waasi wakimuhakikishia itakuwepo hata kesho hana nia ya kumsupport Assad
 
Hii habari si mpya!

US aliisaidia ISIS pakubwa miaka ya nyuma ila walifikia wapi? Wote walipelekwa jikoni!

US hana maisha marefu hapo Syria. Ajiandae kuondolewa.
Endelea kuishi kwa kukariri na historia mfu
 
Wewe Ndio mjinga... Kwa Nini wameshindwa kuutatua huo mgogoro miaka zaidi ya 10 sasa.

Wakati wanaenda kutatua mgogoro wa Ukraine na Russia ambao vita yake ni kubwa zaidi na hatari?

Syria yenyewe bila mtu yoyote kuingilia imegawanyika kimatabaka... Sababu maandamano na Vita ni kumtoa Assad, sababu ya kumtoa ni Kuwa Wasyria wengi ambao ni Waarabu wa Kissuni kutoridhiswa na Serikali yao inayotokana na Jamii ya Watu Kabila/dhehebu la Kishia linaloitwa Alawiites.

Kumtoa Assad ikachukuliwa kama kitendo kisichokubaliwa na Jamii za Kishia Mashariki ya Kati.. Iran, Hezbollah na Wapiganaji wengine wa Kishia wakaanza kuingia Syria kumlinda Assad dhidi ya Wasyria wengine ambao ni Wasunni.

Uturuki anasababu kuu mbili za Kupigana au kuchagua upande.

Uturuki Ndio nchi iliyopokea Wakimbizi wengi sana, kwa hiyo ni obvious lazima itafute utaratibu wa kupambana na changamoto hiyo, jambo la pili baada ya Hii vita Jamii ya Wakurdi Syria wakatumia Nafasi hiyo kuunda nchi ndani ya Syria hii ni hatari kwa Uturuki sababu inawapa Hamasa Wakurdi wa Uturuki kudai nchi yao pia.

Israel kwa upande wake hataki Syria iwe base ya Iran, pia hataki Silaha ziende Lebanon, pia hataki ISIS wame karibu na mipaka yake Ndio maana lazima aingilie

Russia ana base ya navy Syria ambayo inaisaidia sana kwenye bahari ya Mediterranean, so kama Waasi wakimuhakikishia itakuwepo hata kesho hana nia ya kumsupport Assad
Narudia tena kuunasibisha mgogoro wa Syria na udini ni dalili ya kuwa na funza kichwani.
Hivi hujiulizi ni kwa nini vita ya Syria ili simama zaidi ya miaka 4 mpaka ilipo kuja kulipuka tena juzi?
Ni kwasababu ya makubaliano kati ya Uturuki , Urusi na Iran baada ya makubaliano ya hawa watu vita ikasimama na baada ya kuhitirafiana vita imeanza tena hii inatosha kabisa kukuonesha kuwa mgogoro wa Syria unaendeshwa na Mataifa kutoka nje na sio ndani ya Syria.
 
Waasi wanao endesha mashambulizi mmiliki wake ni Uturuki sio Israel .
Jiongeze,hivi tangu Israel aivamie Lebanon na kuisambaratisha Hezbollah ulishaona Erdogan na Turkey yake wakipiga domo zidi ya Israel?
 
Breaking News Wakuu,habari zinasema mapigano ni makali sana usiku huu kwenye viunga vya Mji wa Homs, habari nyingine zinasema Waasi wameshazivunja Ngome za Jeshi la Syria Arab Republic.

Habari nyingine zinasema Ndege za US na IDF zinashughulika na Shia Millitias waliongia kutokea Iraq.

Source:Aljazeera
Popcorn na ghahawa tafadhali
 
Back
Top Bottom