Shaheed zinatumika kwa wingi kwa sababu Urusi ilipewa licence production yake na Iran, na kabla ya hapo Urusi ilizinunua nyingi sana. Ukraine haina hela nyingi kununua TB2 nyingi.
TB2 nimekuelezea na matumizi yake
•Kuvamia Snake island zilitumika kushambulia sehemu ina AD systems za Urusi na video zipo ukibisha nazileta.
•TB2 ilitumika kuiona Moskva cruiser ndio ikazamishwa
•TB2 zimetumika na vikosi vya serikali ya Libya dhidi ya Khalifa Haftar, zimepiga Pantsir AD za Urusi. Evidence zipo
•Uturuki ina videos nyingi ambapo TB2 zinashambulia mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi kule Kaskazini mwa Syria.
•Azerbaijan ilizitumia TB2 kwenye Nagorno-Karabakh na ikapiga AD systems za Armenia zilizoundwa Urusi. Videos zipo
Shaheed na TB2 haviendani hizo sio drones sawa. Ila overral kwenye drone tech Iran ni mtoto mdogo sana mbele ya Uturuki, ndio maana Iran ilikaa siku mbili bila kumuona Rais wao kaanguka wapi, Uturuki ikatumia masaa mawili. Iran hana drone ambayo Uturuki hana, Uturuki ina drones ambazo Iran hana.
Ni hivi, Iran iliiomba Uturuki ilete drone yake kumtafuta Rais wao.