Damu sio nzito kuliko maji

Damu sio nzito kuliko maji

Sikubaze kwenye mantiki mkuu, et uhalisia wa hayo maneno, nimelenga jinsi msemo ulivyo na madhaifu kwenye jamii...

Kweli ndugu ni icon na chanzo zha identity, ila linapokuja swala la kuaminiana na kukubaliana na ndugu hata kama wamekosea, kwa kuzingatia damu ni nzito kuliko maji kumesababisha watu wengi kushikilia watu toxic kwenye maisha wakaharibu mipango yao kisa hao ndugu wa damu. Blood line sio kigezo cha kuamini mtu.

watu wengi hasa waafrika wameathiriwa pakubwa na hii dhana. Sikatai uwepo wa ndugu, ila kudhani ndugu ni mtu muhimu kwenye safari ya maisha.
Dunia hakuna kitu au jambo liko perfect
Hata wewe hauko perfect sio mkamilifu
 
Wewe ndo umetumia hisia.

Hisia ndo zinawafanya wengi watumbukie shimoni.

Usi attach hisia hapo angalia uhalisia wa mambo. Usitumie kigezo cha hakuna binadamu mkamilifu kukubaliana au kupinga hoja. Huko ni kutumia vibaya upeo ulopewa na muumba.
Wewe sio mkamilifu na hakuna mtu ambaye ni mkamilifu
Wewe unaweza ndo ukawa wa kwanza kuwafanyia ndugu zako ubaya
 
Neno ndugu linamkanganyiko mkubwa sana hasa kama ukiliamini asilimia 💯. Ndugu wa kweli sio yule wa damu bali ni yule ambaye ajengae mahusiano yenye afya nawe. Kama mtu umuitaye ndugu wa damu na ndo chanzo cha wewe kukosa furaha basi huyo si ndugu! Neno ndugu lapaswa liangaliwe vizuri watu wengi wameingia kwenye matatizo.
Neno ndugu halina mkanganyiko wowote, ila mtazamo wako juu ya neno 'ndugu' ndio lina mkanganyiko mkubwa sana.

Msemo wa 'damu nzito kuliko maji' unamaana tofauti na unavyotumia wewe.

Damu nzito kuliko maji maana yake usimwage damu kama unavyomwaga maji maana damu ndio unabeba uhai.
 
Hamna kitu umeandika hapo
Bifu lako na ndg zako usifanye kubali misemo mema ya wahenga !! Eti walikunywa gongo kati Yao na wewe nani mlevi?

Kwa akiri ya kawaida tu kati ya maji na damu kipi kizito?.

Mimi binafsi ndg awe mbaya au mzuri Bado halibadiriki neno ni ndg tu. Iwapo ataoneka ni mbaya kwangu basi nitaishi nae Kwa tahadhari.

Lakini mtu Baki hata akikusaidia namna Gani unavyotaka Bado hawezi kuwa ndg wa damu!
 
Ni mawazo yako pia, sina cha kukuelewesha zaidi.
 
Misemo hii huundwa kwa mantiki ya neno halisi la msingi.

Je damu na maji kipi kwa uzani ni kizito kuliko kingine?

Ukitoka hapo sasa anza hizo blah blah zako.

Ndugu ndiyo 'icon' yako ujue.

Hata ukifa leo cha kwanza watu watakachouliza: ... 'hivi ndugu zake wako wapi? '

'Ndugu' ni hadhi ambayo haivuliwi wala kutenguliwa kwa sababu ni watu walio kwenye 'blood line' moja.

Hiyo ya undugu kwa sababu ya misaada ni habari nyingine.

Watu wanaokusaidia ama kuelewana nao ambao siyo ndugu wana majina yao katika jamii huitwa 'marafiki' ama 'ndugu wa nia'.
Umempa ukweli, yeye kakumbana na ndugu wahuni anafanya mjumuisho!
 
Neno ndugu halina mkanganyiko wowote, ila mtazamo wako juu ya neno 'ndugu' ndio lina mkanganyiko mkubwa sana.

Msemo wa 'damu nzito kuliko maji' unamaana tofauti na unavyotumia wewe.

Damu nzito kuliko maji maana yake usimwage damu kama unavyomwaga maji maana damu ndio unabeba uhai.
Hio pia ni maana nyingine ya jinsi ya kutumia huo msemo ambayo ni sahihi pia. Ila maana yake kubwa ni hii ambayo tunaijadili humu. Kama bado hujaitambua basi ila wengi tunaijua.
 
Ndugu atabaki kuwa ndugu hata iweje nakumbuka 2002 kuna ndugu yangu nilimpa kazi ya kusimamia shamba na mifugo
Sasa si akaharibu kwa kunitia hasara asikwambie mtu niliumia sana na tuliachana kwa viapo vikali sana, mwaka 2004 nikaja kukutana naye kwenye hizi harakati za maisha ndugu yangu kachoka eeee bwana wewe nilishikwa na huruma isiyo na kifani chozi la huruma lilinitoka nilimfuata ndugu yangu, nilimkubatia kama dakika mbili tulimaliza tofauti zetu tukasameheana maisha yakaendelea
Damu yako ni damu yako tu hata iweje
 
Hawa wazee jau sana, wanakwambia HARAKA HARAKA HAINA BARAKA ukiwa na jambo lako, wakiwa na jambo lao wanatumia NGOJA NGOJA YAUMIZA MATUMBO.
 
Ndugu Yako ni Ndugu tu damu ni damu ndiyo maana ukifa watauliza Ndugu zake wako wapi....? Usidharau Wala kutweza hata kama huelewani nao Wana umuhimu mno mno....
 
Ndugu atabaki kuwa ndugu hata iweje nakumbuka 2002 kuna ndugu yangu nilimpa kazi ya kusimamia shamba na mifugo
Sasa si akaharibu kwa kunitia hasara asikwambie mtu niliumia sana na tuliachana kwa viapo vikali sana, mwaka 2004 nikaja kukutana naye kwenye hizi harakati za maisha ndugu yangu kachoka eeee bwana wewe nilishikwa na huruma isiyo na kifani chozi la huruma lilinitoka nilimfuata ndugu yangu, nilimkubatia kama dakika mbili tulimaliza tofauti zetu tukasameheana maisha yakaendelea
Damu yako ni damu yako tu hata iweje
Hakika ila isiwe kigezo cha wewe, kuhisi ndugu ndo kila kitu. Ingawa ulimhurumia na kumsaidia baada ya kumkuta maisha yamempiga, kumbuka pia huyohuyo ndo alikutia hasara kubwa. So kama ni kmpenda na kumjali sawa ila usimrudishe kwenye mipango na malengo yako kisa ni ndugu wa damu.
 
Ndugu ni ndugu tu jamani
Utofauti wetu ni kwenye masuala ya kijamii lakini mioyoni mwetu ni nduguzetu Bado na WA muhimu kwetu
Ni kweli ila, isiwe ndo uwaruhusu kuingilia mipango yako kama hawana nia njema na wewe. Kuna ndugu wengine hawana huruma na moyo kama wako. Love them from a distance and wish them well.
 
Back
Top Bottom