Damu ya usaliti wa CHADEMA imewamaliza 2020

Damu ya usaliti wa CHADEMA imewamaliza 2020

fasiliteta

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2014
Posts
2,372
Reaction score
4,090
Ni wazi Wala Bila Shaka kwa Sasa CHADEMA na ndugu zake wamepata matunda ya usaliti wao kwa wananchi.

Msimtafute mchawi hali ya kua mmejiroga wenyewe kwa matendo yenu kwa wananchi na Wala msiangalie mlipoangukia,rudini Sasa muangalie mlipo jikwaa.

Wanachi wengi wamekata tamaa na nyinyi kiasi kwamba hawakua tayari kujisumbua kwenda kituoni kupiga kura.Hivi nikapigie kura chama ambacho;

Wabunge wao na Madiwani rahisi kununulika kwa mujibu wa wao,nitaamini vp walobaki hawanunuliki? Cha ajabu hata wale waloaminika Kama wanamadiliko Kama kina Nassari, Lijuakali, Selasini, Katambi

Mwanachi aliyevuja jasho kusimama vituoni huku akigombana na kuwekeana bifu na familia/marafiki kisa mabadiliko 2015, kisha mkaanza unga juhuudi kisa mna Uhuru wa kuhama chama muda wowote,eti Leo umtoe akakupigie kura!

Ninyi ni wabinafsi sana na hamna msaada wowote kwa wanachi huku mmekua na majibu mabovu tukiwafata Kama wawakilishi wetu kutaka misaada mbali mbali na mkitujibu nyinyi hamuhusiki tuwafate serikali (Kubenea na Bonifasi Jacob tuliwaambia na wanajua jinsi kina mama na wamachinga wakati wanawafata mpaka makwao Jimbo la Ubungo huku wakiwachenga na kujinunulia magari huku wakifaidi ubunge/umeya.

Hamuonekani majimboni huku mkijificha katika mwavuli wa marufuku ya kisiasa/mikutano mkashindwa hata kukaa vikao na Sisi wanachi wenu.

Miaka5 mnakimbizana kuanzisha miradi yenu na familia zenu kwa fedha/mikopo ya ubunge mkasahu uwakilishi wenu, Ubunge ni sehemu ya ajira zenu za kujinufaishi na kujilimbikizia mali na msiseme mnatupigania,wengine wakianzisha mahoteli,majumba makubwa na kututambia suti za gharama toka Italy na Ulaya?

Mnapiga kelele kua shule ni mbovu na kukaa kimya hamchukui hatua yoyote hata kuzisaidiq binafsi kwa kua watoto wenu hawasomi huko, tena kwa jeuri mnapeleka watoto wenu na mnatutambia wao kusoma international school.

Laiti mngewaleta kayumba school bila Shaka spirit ya mabadiliko ya hizo school ingekua kubwa maana mnge feel machungu yake. Niinyi hamjui lolote afu mnataka kujidai kutusemea,mnasema msichokijua.

Nyinyi mlikatisha tamaa sana wapiga kura wa 2015, wameshindwa kurudi tena kupanga mistari kuwapigia kura nyinyi ni wasaliti wakubwa wa nchi hii.

Mna Ndimi mbili na imekua desturi yenu na hamna anayewaamini tena;

Mlimuita na kutuaminisha Lowasa fisadi tena ni wale mafisadi papa katika viwanja vya mwembe yanga,akaja kua mgombea urais wa Chadema. Wanachi tukavunga

Mlituaminisha sumaye Ni fisadi na zero brain, badae mkambeba Tena na uenyekiti juu

Mlituaminisha Lazaro nyarandu aliruhusu Twiga,Simba na chuo kupanda ndege,badae mkambeba na ilibaki kidogo kua mgombea wenu wa urais

Mlituaminisha Wabunge/Madiwani wenu hi wapambanaji na ni watu sahihi, ghafla wakaunga juhudi.

Mkamfukuza zito kabwe na Kitila mkumbo kisa ni wasaliti

Mkamsaliti Dr. Slaa na kumuita Dr. Mihogo

Mkampa ukatibu mkuu Dr. Mashinji Leo yupo CCM, Mkampa uenyekiti vijana(Bavicha)Patrobasi Katambi na leo ni mwana CCM kindakindaki tena alikula mpaka ukuu wa wilaya na nyodo juu.

Mkatuaminisha Nasari anaonewa kuvuliwa ubunge na kupaza sauti, leo yupo CCM,

Mwita waitara naye akaunga juhudi.

Madiwani kila kona tulowapigia kura na ghafla wakaunga juhudi,nani awaamini walobaki au walotaka uwakilishi na kupigiwa kura 2020?

Ruzuku ya chama haieleweki matumiz yake na wakihoji watu mnawafukuza na kuwaita wasaliti.

Mnajiuliza kilichotokea jana

In short hamuaminiki na ni wasaliti nyinyi, waacheni wananchi waendelee na shida zao, wakichoka watanena kwa lugha zao, na si kutumia shida zao kama mtaji wa kisiasa wa Sacco's yenu hii.

Damu ya usaliti kwa wananchi itaendelea kuwatafuna mpaka mwisho.
 
Chama kinachopata ruzuku ya millioni 330 na ushee kila mwezi na kuitafuna bila wasi wasi wowote hakiwezi kuwafanya Watanzania wajinga. Hongera sana Watanzania kwa uamuzi imara na bora kabisa JPM for life!
 
Ni wazi Wala Bila Shaka kwa Sasa Chadema na ndugu zake wamepata matunda ya usaliti wao kwa wananchi.

Msimtafute mchawi hali ya kua mmejiloga wenyewe kwa matendo yenu kwa wananchi na Wala msiangalie mlipoangukia,rudini Sasa muangalie mlipo jikwaa...
Ni mapungwani (mental retards) pekee ndiyo wanaweza kushangilia eti CCM wameshinda uchaguzi huu wa 2020.
 
Wakati ule 2015 CCM wakipongezwa na wananchi kwa kukata jina la fisadi Lowasa kwenye nafasi ya urais, CHADEMA walijiharibia sana 2015 kumsimamisha Lowasa waliyemtuhumu kuwa fisadipapa kugombea urais.

Wananchi wamechagua kutokana walichokiona na kuamini, na wanachoamini ni kwamba kama chadema waliuza chama kwa Lowasa watashindwa kuuza nchi??
 
Nashangaa wale wanaoshangalia upinzani kushindwa bila kujua kwamba uwepo wa wapinzan ndio uimara wa ccm na uwajibikaji wa serikali, sasa hivi bunge lote linaenda kuwa na wabunge wa ccm sasa unajiuliza hawa wataweza kui challenge serikali? Miaka mi5 ya maumivu makubwa kwa wananchi
 
Chatoo Mpooooooooooooooooo
Mwanza mpooooooooooooooo
Dar es salaam mpooooooooooooo
Arusha....mpooooooooooooooooo
Singida mpoooooooooooo
🤣😂🤣😂🤣😂🤣😂🤣😂 Tupoooooooooo
Kwenye kunipigiaaaa Kura Mpooooooooooooo
😡😡😡😡😡😡😡😡😡😡😡 Ebu Acha Ujinga wewe nani Akupigie Kura Kibarakaaaaa Hatupooooooooooooo
 
Salute kwa watanzania. Wametuma salamu kwa mabeberu kwamba damu aliyouacha mwalimu haichezewi.
 
Back
Top Bottom