Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
DAR: Wakili Peter Madeleka akizungumzia kitendo cha Mwanasiasa Dkt. Wilbroad Slaa kukwama kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kueleza kuwa Jeshi la Magereza limeshindwa kumfikisha mshtakiwa huyo Mahakamani kwa madai kuwa kuna changamoto ya magari.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada Mahakama Kuu Tanzania, Masijala Kuu Dar es Salaam kuagiza shauri linalomhusu Dkt. Slaa lirejeshwe Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake.
Wakili Peter Madeleka akizungumza na Wanahabari ametoa maoni kuhusu utendaji wa taasisi kadhaa ikiwemo utendaji wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) pamoja na kumtaja Steven Wasira ambaye ni Makamu Mwenyekiti Bara.
Amesema hayo wakati akizungumzia mwendelezo wa Shauri la jinai Namba 993 ya Mwaka 2025 lililofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Mwanasiasa Dkt. Wilbroad Slaa.
Pia soma ~ Dkt. Slaa ashindwa kufikishwa Mahakamani kutokana na changamoto za usafiri