Tetesi: Dangote kusimamisha kazi zake Tanzania

Tetesi: Dangote kusimamisha kazi zake Tanzania

Status
Not open for further replies.
Wewe Mtu kutoka Nairobi (Nairobian) kufukunua mambo ya Tz na kuja na tetesi zako za ajabu ajabu una sababu gani haswa? Hata kama atakifunga wewe utafaidika na kipi? Kwa taarifa yako Dangote alishapewa rukhusa ya kuwasiliana moja kwa moja na JPM kuhusu tatizo lo lote la kuhisiana na kiwanda chake and it will be solved by the president himself. Hilo tatizo la makaa ya mawe mbona dogo sana. Kama sasa hivi bado ni tatizo kuyapata toka Songea, kwani unafikiri hawezi kuruhusiwa kuyapata nje ya hadi pale atakapoweza kuyapata smoothly na kwa bei nafuu zaidi kutoka Songea?

Kwa nini usi concentrate na mambo ya nchi yenu ambayo kwa sasa iko kwenye kipindi nyeti kuelekea uchaguzi mkuu? Kuna kipindi mlisema Dangote anataka kukihamishia Nairobi kiwanda chake cha Mtwara, hebu acheni wivu wa ngedere.
 
Mleta mada uwe unafikiri vyema!!
Sasa kama ulivyoandika hapo "can't transport coal from songea to expensive and very far" ina maana kusafirisha makaa kutoka nje na kutoka songea wapi mbali na panapohitaji gharama zaidi?


Sent using Jamii Forums mobile app
Hushangai sukari ya Brazil ni rahisi kuliko ya Kilombero?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuagiza makaa ya mawe toka songea ni gharama kubwa lakini kuagiza toka afrika ya kusini ni gharama nafuu!!!! Uongo mwingine hata shetani hajawahi kuufanya! Na aondoke! Hatukuanza maisha baada ya Nangote kuja Tanzania na maisha hayatakoma baada ya Dangote kuondoka Tanzania!


Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe usiseme hivyo. Kumbuka sukari ya nje inasafirishwa maelfu ya kilometa ni rahisi kuliko ya Kilombero. Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unaposema makaa ya mawe yanatoka nje nakuwa sikuelewi na pia watu wa kule songea watakushangaa maana kila siku asubuhi wanapishana na mamia ya malori ya dangote yakisomba makaa kupeleka kiwandani.

Vile vile nilichokisikia mimi ni malipo madogo sana kwa madereva wa hayo malori tofauti na mishahara mikubwa wanayolipwa raia wa kigeni
Leo umeongea point
 
Dangote ana kiwanda ZAMBIA pia mfuko mmoja ni tsh 12000 Bongo mfuko mmoja 15000 + mazingira magumu ya uwekezaji , Yani mtu ameajiri watu karibia 4000 alafu unamletea mchezo

Sent from my Blackberry DTEK70 using JamiiForums mobile app
 
Hajasema kafunga. Hujamuelewa mtoa mada nafikiri
Alipoongopa ni hapa mkuu .."Kwa sasa kiwanda hicho kinatumia genereta na makaa kidogo ya mawe yaliyoagizwa kutoka nje ambayo nayo yanaelekea kuisha".....wakati malori yanapita hapa yamesheheni mkaa wa mawe kutokea Songea. Mtu anayeishi masasi ataniunga mkono kwa hili, kesho ntawapigia picha nikitoka kijijini kusalimia
 
Uwekezaji mkubwa lakini walishindwa kuforecast running costs na kinachotokea ni kutafuta public sympathy ili wapewe favor
Sidhani kama hawaku-forecast. Tatizo ni sera mpya ya nchi ambayo Rais huamua kila jambo ikiwa na kukulazimisha uchukue wapi raw materials au inputs nyingine. Biashara ni ushindani. Kwa nini umlazimishe mwenye kiwanda atumie makaa ya mawe toka Songea wakati ni aghali kushinda yanayotoka SA? Dhamira ni njema lakini approach ni mbovu.

Kama unataka watumie makaa ya Songea, wawekee mazingira hao wazalishaji wa Songea ya kuwafanya wawe na uwezo wa kushindana na wale wa South Africa. Jamaa anafanya jitihada kubwa kuturudisha tulikoondoka kwa gharama kubwa. Na sass, naona zaidi anatarget kundi lenye upeo mdogo ili awamezeshe kila alitamkalo hata kama halina uhalisia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ana viwanda vingapj nchi ngapi ili leo atafute sympathy. Utetezi wako ni kipenda roho ....

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa na viwanda vingi siyo hoja. Unaweza ukawa na wake wanne lakini siyo kwamba kila ukienda kwa mkeo kulingana na ratiba uliyojiwekea basi performance itakuwa ileile, la hasha haiwezi kuwa sawa.
Capitalist kama wengine wanaopenda kupata super profit kupitia migongo ya Wakuu wa nchi.
 
Hivi huwa mnapata faida gani mnapoleta uongo wa aina hii

Unajificha kwenye neno tetesi ili kueneza uongo.

Unafaa kupigwa ban ya mwaka kwa sababu unafanya hisa za dangote zishuke kwenye soko la hisa kwa sababu ya kueneza uongo.
Is Dangote Cement company listed in DSE? If so; unaweza kutuonyesha kwa number kuporomoka huko kwa hisa zao baada ya jamaa kuandika maneno hayo? Msema Ukweli
 
Walisha focus sana kwny Cost Tatizo tumeingiza Mambo ya Ujamaa kwa kuwachagulia wapi wakanunue Nishati!

Style ya Uchumi wa Kijamaa ulligharimu sana Nchi wakati wa Nyerere na JPM analazimisha kurudia hilo kosa

Ni sawa na ile ya kulazimisha kila anaetaka kusafirisha Mahindi Basi asafirishe unga kutokna na kukariri kwetu kuwa Matumizi ya Mahindi ni kukorogea Uji na kusongea ugali pekee!
Nimekuelewa
 
Inawezekana ni dalili za kufilisika hakuna ajabu si hata ethieopia nako amefunga!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom