Daniel Chongolo awa Katibu Mkuu CCM

Daniel Chongolo awa Katibu Mkuu CCM

DANIEL CHONGOLO APENDEKEZWA KUWA KATIBU MKUU CCM

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Ndg. Daniel Chongolo kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho

Kwa sasa, Chongolo ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar.

Huyu anakijua sana chama.na chama kiko damuni toka zamani.kumbe ccm wanawajua walio wa kwao
 
DANIEL GODFREY CHONGOLO Alikuwa Makao Makuu ya Chama Enzi Ya Akina Nape, Chongolo alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma kilichokuwa chini ya idara ya Sera na Uenezi(Kitengo cha Propaganda).
Kumbe jamaa mzoefu kwenye Chama.
 
Wacheni Mungu aitwe Mungu,Makonda aliwahi kumkoromea vibaya sana huyu jamaa, sasa leo hii Makonda alitaka kumuona lazima aombe appointment.View attachment 1769200
Hapa ndiyo namkumbuka marehemu Ruge mutahaba alipotamka kuwa "ogopa Mungu na teknolojia " , Sasa kazi iliyobaki ni kuumbuka. Aidha JK alishawahi kuwaasa viongozi kuacha kuwanyanyasa na kuwadharirisha wenzao sababu huwezi jua kesho watakuwa nani!, Makonda nafikiri amepata funzo kwa ujinga wake
 
Mshikaji amekulia eneo fulani linaitwa Twico kwenye kiwanda cha mbao cha Sao hill- Mafinga.

Ametoka kwenye media akiwa mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru. Amejitahidi kutatua changamoto za ardhi akiwa Longido kbl ya kuhamishiwa Dar.

Yupo humble, si mtu wa majidai, mwenye uwezo fulani wa kutatua changamoto.

Tukiondoa ujuaji uliopo CCM kwamba wapo wenye CCM yao dogo anaweza kumudu!

KILA LA KHERI
kwani Bashiru Ally Kakurwa anasemaje?
 
Nikiangakia hii clip yaani mtu mzima unadhihakiwa mbele ya camera. Mke na Watoto wanakuona na ndugu na marafiki. Achilia mbali dunia nzima. Kila kiongozi alijiona Mungu mtu katika kiti chake kuanzia wa kisiasa hata wale watendaji kwenye Taasisi. Haya yote wakichukua kwa baba yao.
Watanzania huu siyo utamaduni wetu.

Hakika Mungu alisikia masononeko yetu. Mungu akaamua iwe kweli tena kwelikweli. Au nasema uongo ndugu zanguni? Hebu piga kelele za Shangwe kwa Mungu.
Hallelujah!!!!!
 
Nyalandu alikuwa outsider ndiyo maana tulimnyima kura kugombea Urais. Chadema ipo tena ipo sana. Kwa mataahira tu ndiyo wanaona kama wewe
Sababu ya upepo wa Lissu, vinginevyo angepewa kugombea. Kwani kwa Lowassa ilikuaje?
 
Back
Top Bottom